PostGE2025 Brenda: CCM wanahangaika kutugawa CHADEMA, tuna ushahidi CCM wanawalipa watu Tsh. Milioni 3 kutuchafua

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Katika mahojiano yake na Kituo cha Redio cha East Africa radio, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA Taifa, Brenda Rupia Jonas, amedai kuwa wana ushahidi wa kutosha, ikiwemo rekodi za sauti, za viongozi waandamizi wa CCM wakiwalipa watu kiasi cha shilingi milioni tatu ili kufanya mikutano na waandishi wa habari kwa lengo la kuichafua CHADEMA.

Aliongeza kuwa ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA iko wazi kupokea malalamiko yoyote rasmi kwa maandishi kutoka kwa wanachama, lakini hadi sasa hakuna lalamiko lolote lililowasilishwa kupitia taratibu za chama, jambo linalothibitisha kuwa shutuma hizo hazina ukweli wowote.

CHADEMA mnatakiwa kuwa makini kwenye kila kitu. Msifikirie ccm watawatendea wema. Mwenyekiti wenu mpaka sasa anashikiliwa gerezani akiwa hana hati yoyote! Mnategemea nyinyi huku uraiani mtatendewa wema?
 
Sisi tunao tuu mpaka watuambie miaka 60+ ya Uhuru wanatuahidi zahanati huku migodi na Mali asili zote wakiwa wameuza watatuambia
 
Katika mahojiano yake na Kituo cha Redio cha East Africa radio, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA Taifa, Brenda Rupia Jonas, amedai kuwa wana ushahidi wa kutosha, ikiwemo rekodi za sauti, za viongozi waandamizi wa CCM wakiwalipa watu kiasi cha shilingi milioni tatu ili kufanya mikutano na waandishi wa habari kwa lengo la kuichafua CHADEMA.

Aliongeza kuwa ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA iko wazi kupokea malalamiko yoyote rasmi kwa maandishi kutoka kwa wanachama, lakini hadi sasa hakuna lalamiko lolote lililowasilishwa kupitia taratibu za chama, jambo linalothibitisha kuwa shutuma hizo hazina ukweli wowote.

Wawapeleke mahakamani japo sina imani na mahakama zetu ni vizuri wakaimbe huko mahakamani.
 
Back
Top Bottom