- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Brenda Rupia ni mkurugezi wa mawasiliano na uenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye pia ni katibu wa Bawacha mkoa wa Kinondoni jijini Dar es salaam.
Kumekuwepo na kipeperushi chenye muonekano wa Gazeti ambacho kimekuwa kikisambazwa mtandaoni kikiwa na taarifa inayosema 'Brenda Rupia ajiuzulu ukurugenzi CHADEMA'
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani, hakuna taarifa iliyotolewa na CHADEMA au Brenda Rupia mwenyewe kuhusu kujiuzulu kwenye nafasi hiyo.
Aidha Rupia ameendelea kutekeleza majukumu yake kama mkurugenzi wa mawasilino na uenezi ambapo Agosti 15, 2025 alisaini taarifa kwa umma iliyotolewa na chama hicho kuhusu mchango wa milioni 100 uliotolewa na Yanga SC kwenda kwa Chama cha Mapinduzi.
Akizungumza na JamiiCheck, Brenda Rupia amekanusha taarifa hiyo na kwamba si ya kweli. "Sio kweli mimi nipo msibani Songea kumzika kamanda mwenzetu MC Mwingira"