ngunde11
JF-Expert Member
- Jan 8, 2016
- 746
- 1,025
Nakuandikia ujumbe huu kwa nia ya kuonyesha hisia zangu za dhati na pongezi kubwa kwako. Hakika umekuwa kielelezo cha mwanamke shujaa, mwenye akili nyingi, msimamo thabiti na uzuri wa kipekee uliopambwa na ujasiri mkubwa.
Usimamo wako na uwezo wako wa kujibu maswali kwa umakini na weledi mkubwa ulipokuwa kizimbani kama shahidi wa nne, umewagusa na kuwavutia watu wengi sana kote nchini. Akili yako na namna unavyosimamia ukweli vimeacha alama kubwa mioyoni mwa wengi.
Mbali na utendaji wako makini wa kazi, uzuri wako wa asili na heshima uliyonayo vimekuwa kivutio kikubwa. Wewe ni mfano bora wa mwanamke anayejua kusimamia kile anachokiamini kwa weledi wa hali ya juu. Nakuombea kila la heri katika majukumu yako na maisha yako kwa ujumla.