Brenda Rupia Pongezi kwa Ujasiri uzuri na uwezo wako

ngunde11

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2016
Posts
746
Reaction score
1,025
Nakuandikia ujumbe huu kwa nia ya kuonyesha hisia zangu za dhati na pongezi kubwa kwako. Hakika umekuwa kielelezo cha mwanamke shujaa, mwenye akili nyingi, msimamo thabiti na uzuri wa kipekee uliopambwa na ujasiri mkubwa.

Usimamo wako na uwezo wako wa kujibu maswali kwa umakini na weledi mkubwa ulipokuwa kizimbani kama shahidi wa nne, umewagusa na kuwavutia watu wengi sana kote nchini. Akili yako na namna unavyosimamia ukweli vimeacha alama kubwa mioyoni mwa wengi.

Mbali na utendaji wako makini wa kazi, uzuri wako wa asili na heshima uliyonayo vimekuwa kivutio kikubwa. Wewe ni mfano bora wa mwanamke anayejua kusimamia kile anachokiamini kwa weledi wa hali ya juu. Nakuombea kila la heri katika majukumu yako na maisha yako kwa ujumla.
 
Ka dada kanaakili nyingi sana .... mtulivu na anaeendana na kasi ya sasa ya uongozi wa CHADEMA na ni mzuri kweli ki uumbaji
 
Chadema haijawahi kukosea kuchagua viongozi walio imara vichwani mwao!
Kuna kile chama kinachagua Four form failure, kinakoelekea, watabaki wazee wale wanatoa macho kama wanakufa,Mwandri + Wassira+ Kabudi.
 
Chadema haijawahi kukosea kuchagua viongozi walio imara vichwani mwao!
Kuna kile chama kinachagua Four form failure, kinakoelekea, watabaki wazee wale wanatoa macho kama wanakufa,Mwandri + Wassira+ Kabudi.
 

Attachments

  • 1000024076.jpg
    45.1 KB · Views: 8
  • IMG_0830.jpeg
    184.2 KB · Views: 8
  • IMG-20260415-WA0001.jpg
    53.5 KB · Views: 9
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…