Brenda Rupia :Tunafuatilia kukamatwa kwa Zakaria Obadi polisi wafuate sheria

Brenda Rupia :Tunafuatilia kukamatwa kwa Zakaria Obadi polisi wafuate sheria

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Brenda Rupia Jonas, amesema chama hicho kimeshatuma wawakilishi wake katika vituo vya polisi jijini Mwanza kwa ajili ya kufuatilia hatua za kisheria baada ya kukamatwa kwa Katibu wa CHADEMA Kanda ya Victoria, Zacharia Obadi, nyumbani kwake majira ya saa 9 usiku.

Taarifa kutoka kwa Gaston Garubindi kuhusu kukamwatwa kwa Zacharia obadi

Jeshi la Polisi wilaya ya Kahama linamshikilia Katibu wa Kanda ya Victoria Zacharia Obad baada ya kuvamia nyumbani kwake jana usiku majira ya saa nane kwa tuhuma ambazo bado hazijajulikana.
Kwa sasa, Zacharia Obad yupo kituo cha Polisi Kahama, akisubiri kuchukuliwa maelezo.

Wakili Alex Dotto Massaba yupo mjini Kahama kutoa msaada wa kisheria kwa Obad.
Obad Zacharia ni kiongozi mkubwa, angeitwa Polisi kama wanashida naye angefika kuliko kutumia utaratibu wa kuvamia makazi yake Kahama mjini usiku wa manane na kusababisha taharuki.
Obad zqcharia anakuwa mwanachama wa mwanachama wa tano, kukamatwa ndani kipindi kifupi. Wengine waliokamatwa na Polisi ni Mkurugenzi wa Organization na Mafunzo John Pambalu, aliyekamatwa Arusha na kusafurishwa hadi Dar.

Wengine ni Mwenyekiti Bavicha Mkoa wa Kigoma Coletha Ntidyicha aliyekamatwa Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Bavicha kanda ya Victoria Fred Masele, aliyekamatwa Mwanza , Edson Malyo Mliyinga huyu alikamatwa mkoani Iringa, Fadhili Benedict Mbeya alikamatwa Dar Es salaam na Doris Msigwa aliyekamatwa Arusha.
Tafadhali, watuhumiwa hawa wafikishwe Mahakamani kwa mujibu wa sheria za nchi yetu

Chanzo: landdwellers

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Brenda Rupia Jonas, amesema chama hicho kimeshatuma wawakilishi wake katika vituo vya polisi jijini Mwanza kwa ajili ya kufuatilia hatua za kisheria baada ya kukamatwa kwa Katibu wa CHADEMA Kanda ya Victoria, Zacharia Obadi, nyumbani kwake majira ya saa 9 usiku.
Chanzo: landdwellers

Ok.
hakikisheni mamluki wote walikua wakiishi Nairobi hotelini wakishashakanyaga ardhi tukufu ya Tanzania, waliyoitukana kila aina ya tusi, waliyoizushia na kuinenea kila ubaya na kila aina ya uovu, wanajisalmisha kwa hiyari au vyombo vya ulinzi na usalama vitawafuata kokote watakapokua wamejificha nchini. Uovu na uharibifu walioufanya kwa makusudi Oct 2025 lazima walipe kwa gharama kubwa sana korokoroni.

hatuwezi kuvumilia watu waovu namna hiyo tena vijana kabisa katika taifa letu 🐒
 
Wewe mkata viuno Bora sana wa Lumumba buku7 mbona huachi kujitoa ufahanu kumbuka haya yana mwisho siku ZOTE mimi hupenda kukusanua hawa madikiteta uchwara mwisho wao unakalibia Sasa muda ukifika usijage ukaanza kutupigia kelele oh mimi mwana chadema sema TU sijui shetani hatutakuelewa we kata sana viuno uzuri tunafahamiana vyema
 
Back
Top Bottom