Brevis AI 250

Hapo badili tu coil spark za hiyo gari kuna moja au mbili zimekufa hapo hizo ndio zinapelekea kucheleweaha uchomaji wa mafuta
 
Bendix hiyo mzee, badili bendix kwenye starter motor
 
Gari ikilala Kwa mafundi lazima waibe Tu hata Kwa waoshaji pia unatakiwa usimamie vinginevyo wanachoma Mpaka fuse na wanaweka za kwao mbovu
Yani nimejuta sana sahizi natakiwa niingie gharama ambazo hata hazikuwa zangu. Inauma sana!!! Gari inakula mafuta kama wazimu yani sijui wameichokonoa nini yani. Gari ikikaa silencer inaweza ikakausha litre 4 za ngwese yani nimechoka.
 
Yani nimejuta sana sahizi natakiwa niingie gharama ambazo hata hazikuwa zangu. Inauma sana!!! Gari inakula mafuta kama wazimu yani sijui wameichokonoa nini yani. Gari ikikaa silencer inaweza ikakausha litre 4 za ngwese yani nimechoka.
mkuu badala nisikitike mafundi kukosa uaminifu nacheka sana maneno yako
 
mkuu badala nisikitike mafundi kukosa uaminifu nacheka sana maneno yako
Yani niliitoa gereji kwa hasira sababu ni upuuzi. Wameua kitasa mlango mmoja haufunguki nyuma, the next day nataka niichukue gari anasema boss gari haiwaki nafikiri itakuwa mafuta, nakwenda angalia nakuta ina pancha sijui hata imekuwaje kuwaje hio pancha. Nikampa hela ya mafuta pakikucha aweke kesho eti gari still haiwaki nikamwambia tu nikirudi jioni hio gari ikiwa haiwaki mjue tu kwamba mnaenda kulala polisi.
Gari imekuja nzima gereji bila kusukumwa mnasemaje haiwaki?

Kurudi nikakuta inawaka madai eti pump ilikuwa chafu ila still tatizo la kuwaka halijatatulika. Tayari inachelewa kupokea meaning kuna kitu walifanya cha tofauti.
 
Poleee aiseeee
 
Angalieni starter
 
Hii inawezekana na mimi wamenicheza nini? Kwa sababu nalo hili tatizo limekuja siku mbili baada ya kuitoa garage fulani hivi ambako niliipeleka kubadilisha brake pads
Hebu fuatilia coils mkuu, na pump ichekiwe na mtaalam. Mafundi wetu hawa wahuni sana najuta kuilaza gari pale.
 
Brevis ukiijua engine iliyopo ndani yake wala huwezi jiuliza kwa nini inakula mafuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…