Briefcase zilikuwa zinatumika kubebea nini?

Briefcase zilikuwa zinatumika kubebea nini?

Zurie

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2014
Posts
2,012
Reaction score
5,571
Hello wakuu,

Leo nimekumbuka enzi za utoto wangu wanaume walikuwa wanabeba briefcase. Kwa wasiozijua naomba mzingatie picha. Wanaume walikuwa wanaenda na kurudi nazo kazini.

Najua hata sasa mabegi yanabebwa ila kwa siku hizi "laptops" zimekuwa common hivyo wengi wanabeba laptops kwenye backpacks zao au mabegi ya laptop ya mkononi.

Sasa briefcase walikuwa wanaweka nini kilichokuwa lazima kutembea nacho? Au ilikuwa urembo tu na kuna mambo ya kwenye movie?

71TifNYie6L._AC_UL1500_.jpg

man-with-metalic-briefcase_1149-1210.jpg
 
Dar miaka ya mwishoni mwa tisini iliingia fasheni ya wadada kubeba midoli......unakuta mdada kabeba bonge la doli anasubiri dala stendi......sijui iliishia wap hii fashen!
Duuuh.Si mchezo hiii [emoji3][emoji3]
 
Mzee wangu alikuwa anabebea laptop siku akaja kuibiwa laptop yake akaacha kuibeba sasa hivi inawekewa tu makaratasi lipo ndan ya kabati😁😁😁
 
Aisee kama upo na Mimi Baba yangu(Marehemu ) alikuwa hasafiri bila hiyo kitu hata kama atabeba begi jingine.
Na tulikuwa ukitaka kujua kama amesafiri tunaitafuta Briefcase, tukiikosa tunakuwa tayari tuna uhakika amesafiri.
Hahaha ndio sisi tulikuwa tunaenda kuichungulia kama ipo, au ukimuona anaanza kuitanguliza ujue hapa kuna safari wazee maboss wa enzi hizo hapa nazungumzia 80's. Hata sijui alikuwa anaweka nini labda documents maana laptop hazikuwepo😁
 
Hello wakuu,

Leo nimekumbuka enzi za utoto wangu wanaume walikuwa wanabeba briefcase. Kwa wasiozijua naomba mzingatie picha. Wanaume walikuwa wanaenda na kurudi nazo kazini.

Najua hata sasa mabegi yanabebwa ila kwa siku hizi "laptops" zimekuwa common hivyo wengi wanabeba laptops kwenye backpacks zao au mabegi ya laptop ya mkononi.

Sasa briefcase walikuwa wanaweka nini kilichokuwa lazima kutembea nacho? Au ilikuwa urembo tu na kuna mambo ya kwenye movie?

View attachment 1461019

View attachment 1461022
Briefcase zilibeba analogy na sasa laptop zinabeba digital.
 
Aisee kama upo na Mimi Baba yangu(Marehemu ) alikuwa hasafiri bila hiyo kitu hata kama atabeba begi jingine.
Na tulikuwa ukitaka kujua kama amesafiri tunaitafuta Briefcase, tukiikosa tunakuwa tayari tuna uhakika amesafiri.
Itakua mlikua watundu sana! Mkithibitisha kasafiri mnaanza umafia wenu

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom