Bring back our TMK Wanaume Group

Bring back our TMK Wanaume Group

Samcezar

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
13,095
Reaction score
22,731
Aisee kama kuna kosa lilifanyika katika tasinia ya muziki wa bongo flavour itakuwa ni uamuzi wa wasanii wa kundi la TMK wanaume kujisambaratisha.

Sina taarifa za uhakika juu ya sababu za kusambaratika kwa kundi hilo ambalo hadi linasambaratishwa lilikuwa ni kundi linalobamba kuliko yote yaliyowahi kuwapo. lilibamba kuanzia uswazi maeneo ya Temeke ambapo ni makao yake makuu, Tandale, Mbagala na Ilala lakini pia hadi maeneo ya kishua kama Oyster Bay, Upanga, Masaki, Mikocheni, Mbezi na bado mikoani ambapo ilikuwa ni shida walibamba hadi basi.

Masikitiko yangu ni pale tu zilipoanza tetesi kuwa hili kundi wameshindwana na uongozi wake hivyo wakaamua kugawana mbao.

Mbaya zaidi ni kwamba baada ya hawa wasanii kuvunja kundi lao wameshindwa kukamata tena halaiki ya mashabiki kwakuwa walishazoeleka wakiwa pamoja. Ama kweli umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.

Hivi ni kwanini basi wasanii hawa wasirejee tena kwenye meza ya mazungumzo watazame wapi palikuwa na dosari kisha wafanye marekebisho na kuongezea vifungu vya sheria ili masilahi ya kundi yasichezewe tena Juma Nature, Mh. Temba, Chege na wengineo. Hebu naombeni mjirudi na kuweka ubinafsi wenu pembeni.

Kwa maana maamuzi yenu binafsi yametukosesha sisi mashabiki Burudani, mnatukosesha ile flavour halisi ya muziki huu wa bongo fllavour kutoka uswazi maana nyie ndio mlikimbiza gemu hadi hapa ilipo.

Inauma sana nikitazama video za wanaume wakitumbuiza kwenye majukwaa, askari halisi, majita, wanaumeeeeee (watu hujibu eeeeeeeeeh) masimera, walumendago, wanaskangagaaa, naumia sana.

Hebu mrudishe tena ile Brand ya wanaume maana spirit yake bado ipo hai hadi leo mrudi kama mlivyokuwa awali wekeni tofauti zenu kando sipati picha ni namna gani mtaamsha mizuka ya washabiki wenu tena.


Bring back our TMK WANAUME GROUP.


[emoji31] Wanaaaaumeeeeeeeee
 
Kila kitu kina muda wake kulikuwa na magroup mengi sasa yapo wap manzese crew,majita,eastcost,mabaga fresh,soldgrand family na mengine mengi sasa yapo wapi kila kitu kina muda wake sasa ni msimu wa hawa vijana wacha tule flavor
 
minji,
Nakazia
Big dog pose
Swahili Matola
Gangwe Mob
Kikosi cha mizinga
Solidi Family Ground nk...nk
 
Katika ngoma za wanaume TMK kuna ile nyumbani ni nyumbani, jamaa anasema kuna mchizi ameshindwa kumtambulisha mchumba yake kwao kisa ana figure ya kiume[emoji28],
Katika ile tungo napenda sana verse ya mh temba
 
Temba anajaribu kuwarudisha .. Na nadhani Fella anawasidia tena
 
Back
Top Bottom