Bro, timiza unayoyaweza , Dunia wala haipo Kasi ni walimwengu tu

Jack Daniel

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2021
Posts
4,951
Reaction score
19,766
Salaam jamiiforum.

Ni April 19 leo mwaka 2026,
Siku zinakimbia, yaani bado siku kadhaa tu iadhimishwe siku ya wafanyakazi,bado wiki chache kufikisha nusu mwaka.
Ama kweli siku hazigandi.

Cha ajabu maisha ni kama yamesimama ,mishe hazisogei,mipango haitimii, anyway kila kitu kina wakati wake. Mpango wangu wa kulima ekari 50 za mpunga ulishafeli kabla sijaanza ,kwani miezi ya mavuno imekaribia lakini nimeishia kufanya research ya shamba na kukodi tu ila hakuna trekta wala harrow ilifanikiwa kuingia kwenye hilo shamba. any way asiyekubali kushindwa si mshindani nitajaribu next year.

Kelele nazisikia,sijui zinatoka wapi? ,ambazo zinataka nipambane lakini nashangaa kwanini nakimbizana kiasi hiki wakati naweza relax nakunywa bia tu na life likaendelea,sina watoto wengi ,na wengine tayari Wana uwezo wa kujisimamia wenyewe.
Nakuja kugundua mob socialism nayo inaniharibu najikuta mtu wa kusikiliza kelele za watu ambazo sijui ni za kina nani.

Lakini pia, aliyenishauri nianzishe mpango wa Kujenga lodge mkoa x huku akinipa hesabu sizizolipa, Mungu anakuona 😂 ni afadhali ungenishauri tunywe bia kutwa nzima Kwa aina ya bia zetu local tusingemaliza laki mbili ,tungefurahi tungeongeza siku za kuishi,lakini robo ya utajiri wangu imelala kwenye kitu sina uhakika nacho.

My bro sikiliza akili yako ta ndani,timiza unayoyaweza na si kuanzisha makubwa yasiyowezekana.

Japokuwa makosa ni yangu si yako,ina sasa mwaka wa tatu lodge ipo kwenye Renta haijulikani itaisha lini! yajayo yanafurahisha.

Mpendwa na mdau wa jamiiforum,
Najua unapenda maendeleo,najua unahitaji kukua kivyovyote ,
Iwe kiuchumi,ushawishi na kuwa na fame fulani kwenye jamii inayokuzunguka na hiyo ni ndoto ya watu weeeengi mno.

Ushindani ni mkubwa,
Yaani badala ya mtu atimize malengo yake,anajikuta anaathirika na presha za marafiki na wadau kadhaa na kuingia kwenye mtego wa kiushindani.

My bro,maisha si kukimbizana,
Maisha ni mipango,mifereji uliyoitengeneza ndiyo yenye kukuletea unachotaka na si kutishika na mafanikio ya wengine na kukaribisha magonjwa yasiyotibika.

Huu mwaka uishe tu,😂
Mengi nishafeli Acha nisubiri kuangalia kombe la Dunia tu,kisha nitajaribu mwakani.

Japo naumia jumapili iliyopita nilikaribishwa na mtu ambaye ni mdogo wangu Sana nimemzidi miaka 11 ,amesoma Kwa kiasi fulani ,na ana ufahamu fulani lakini hajawahi kufanya kazi Kwa mtu ,kifupi hajawahi KUAJIRIWA.

yaani hajui furaha unayopata mtu pindi mshahara ukiingia,hajui sauti inayobadilika na kuanza kumpelekesha wife akimbizane supermarket kwakuwa tu umepata mshahara,hajui ndita zinavyokunjwa pindi tu ukimlipa Kodi mwenye nyumba Kwa mbwembwe😂

But mdogo wangu yeye alichagua kujiajiri,yaani alipe watu, yaani hata ukimlipa mtu elfu 10 tayari wewe ni boss.

Kwa kufupisha stori Acha tu ,tulitumia masaa manane akinitembeza kwenye miradi na baadhi ya mafanikio yake,mmmh ama kweli
PESA HAITAKI KELELE.

Dogo hanywi pombe,
Dogo si mtu wa mademu,
Dogo yupoyupo tu

Sasa angekuwa Daniel,yaani msingekunywa maji yakapita ,watoto wazuri wote mngenijua Mimi nani.

Yaani dogo ulininidharau Sana najua si mtu wa mitandao ila hili bandiko ukiliona jua brother D kaandika ,

Yaani gari nane,semi trailer Scania zote , hujui uliniumiza moyo halafu ulivyo mpole ningekuwa Mimi madereva wasingekunywa hata pombe,weeee boss hatumii kilevi iweje dereva?

Nazeeka sasa,kanisani sijaenda castle lite zinafanya yake huku chumbani
 

Attachments

  • IMG_20260419_094629.jpg
    221 KB · Views: 30
Kuna jambo nilikua naambiwa kipindi Cha nyuma kuhusu kupata mafanikio na kukaa huko juu ...nlipinga sana ...nmekuja kuelewa baadae sana. anyway kila mtu afanye anavyoweza kama mdau ulivyoamua kujipa raha mwenyewe
 
Kuna jamaa kaanzisha duka la dawa, sehemu ambayo kuna watu si wengi na tayari kuna maduka ya dawa kama mengi tuu.

Nakaa namshangaa tuu ila mimi mwenyewe sina kitu chochote cha maana.

Kuna vitu tunafanya kwa sababu ya pressure tunaipata kutoka kwa watu wanaotuzunguka.
Kitu ambacho si kizuri.
 
Uzi mzur kijana n kwel mtu asifikirie makubwa anza na madog kwanza hawenga walisema mwenda pole hajikwai,mvumilivu hula mbivu kwenye maisha yatupasa kuvumulia na kupandana ili hazina ya kesho iwe bora jiekeze ata ikiwezekana anza na kuku mmoja utaenda hivyo had banda litajaa kuku usiwe na tamaa ya wanawake tafuta mmoja wakwako ambaye hamshei penzi maana wahenga walisema kidole kimoja hakivunji chawa nguvu ya mwanaume n kuwa na mwenza ambaye mtambana kwa pamoja kwa upendo na kufanikiwa ndoa idumu milele!asanten Jf
 
Usiogope kuchukiwa,kukataliwa,kukejeliw,kudharauliwa maana mti ukuwao kwenye jangwa huzaa matunda matamu yeyote apitiaye taabu bila kukata tamaa na ni mpambanaji daima hufanikiwa Diamond,Harmonize,marioo walikataliwa wakadharauliwa ila hawakuta tamaa leo hii hao n mastaa wanaojulikana kimataifa na hakuna asiye na uwezo wa kufanikiwa tatizo wengi wanakata tamaa na mwishowe wanafel
 
Nazeeka sasa,kanisani sijaenda castle lite zinafanya yake huku chumbani
Mkuu
Kama una lodge iko kwenye lenta
Na una uwezo wa kukodi shamba la ekari 50
On top of that una sehemu ya kuishi na uwezo wa kushusha castle light za baridi + una afya njema...
WEWE UKO MBALI SANA KUZIDI ASILIMIA 95 YA WATANZANIA!
Kaa, tulia shusha castle zako bila wasiwasi wowote wee huna haja ya kuwa na stress kabisa. Hayo mengine yatajiseti tuu taratibu.
 
Niuzie hilo pagale la lodge nimalizie ama nilimalizie kwa pesa zangu then tupige mahesabu namna tutagawana faida biashara ikiiva
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…