Brother, haya ndio yatakuwa mambo ya muhimu kwako katika siku zijazo

Jaji mkuu huko taifa la Mexico huwa anapigiwa kura kama vile mbunge anavyopigiwa kura.

Nadhani tukifika hatua hiyo itasaidia. Tuhaja ya kuunda mfumo upya.

Na pia tuwe na kitabu cha AIBU ambacho kitaandika viongozi walioharibu taifa na ushahidi wa matendo yao ya kuhujumu taifa ili mtu akitaka kuharibu ajue aibu ya matendo yake itawaandama watoto wake na wajukuu.
 
Huwa nikirudia kusoma huu uzi napata shida sana kuamini kama Tumia akili hana ushawishi tena kwenye the state maana soon huyo Brother aliyetajwa hapa nafasi yake inaenda kushikwa na mwingine. Je ina maana haya aliyotuambia hapa TA yakikuwa fake au alizidiwa nguvu
 
Huu uzi ulinirudishia sana matumaini juu ya mstakabali wa taifa letu. Ila mpaka sioni uwezekano wa Brother kuyatekeleza aliyotakiwa kuyafanya baada ya kubaki bila kuondoka. Zimebaki kama siku 30 tu Brother aondoke na huku mama akichukua ngwe nyingine isiyo na chembe ya matumaini kwa taifa.

The state imeshindwa kabisa nguvu na Ccm mtandao, maana wanachanja mbuga kuliko wakati mwingine wowote katika taifa huku wakibagaza na kubananga rasilimali za nchi na kutindinganya mambo kama anavyosema ndg HHP.

Najiuliza kama waliweza kumla kichwa Magu pamoja na kuwa hakuwa mbaya kama alivyofikia huyu mazeri ni kipi kinawakwamisha kupindua meza kwa uongozi huu. Nimeamini wahuni wana nguvu isiyomithilika katika taifa hili. Gwajiboy kaufyata mbaya hajulikani hata alike kwasasa.

Anyway ipo siku Mwenyezi Mungu aziyeshindwa kitu atatenda jambo litakalowaacha midomo wazi wanamtandao.
 
Swali fikirishi.
Hivi rais mstahafu anawezaje kutekeleza execution ya incumbent bila incumbent kujua wakati yeye ndio mwenye vyombo?

Swali fikirishi.
Wakati BMe anasimamia mission according to HP hakujua kwamba punde tu mission ikiwa accomplished nayeye atafungiwa fundo?
 
Swali fikirishi.
Hivi rais mstahafu anawezaje kutekeleza execution ya incumbent bila incumbent kujua wakati yeye ndio mwenye vyombo?
Mizizi mirefu amejichimbia mnoo kwenda chini, yupo ulingoni kitambo, ana loyal disciples wa kutosha kila pahala.

Swali fikirishi.
Wakati BMe anasimamia mission according to HP hakujua kwamba punde tu mission ikiwa accomplished nayeye atafungiwa fundo?
Kwamba jasusi alifanyiwa ujasusi na mwamba aliekuwa na alibi ya kuwa kwa nduguze kiduku?

Mambo 'yalibadilika sana' kiasi hicho toka kuwa his candidate 2015 hadi kumfanyia ujasusi?

Sio kwamba kambi ya mdeni wa jasusi mbobevu ilimjasusi ili kupotezea deni na kujipa faraja kwa ujasusi wa 2021 uliofanywa na jasusi mbobevu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…