Hi Kiranga;
I have a lot to learn from you, though I likedebating with you; I, at the same time enjoy reading your articlles, especially the positive ones! Why do not you switch back to your earlier JF days articles manner? Napenda sana kusoma makala zako ila sana sana zile tu ambazo ni positive!
Penya positive pana negative, penye juu pana chini, penye kulia pana kushoto. Haya ni mambo ya asili.
Watu wengi hawaelewi ninavyoandika na wanaona kwamba niko negative. Kuna msemo kwamba waandishi wa habari hawaandiki habari nzuri za kutosha, pengine ni kweli.
Lakini ukiangalia kwa mfano kazi ya uandishi, habari ya kumwambia mtu kashinda zawadi na ile ya kumwambia mtu kwamba nyumba yako inaungua moto, anza kuuzima, ipi ni ya haraka zaidi? Mimi naona hii ya kuzima moto ni ya haraka zaidi na hivyo naweza kuipa umuhimu.
Sisi by nature ni positive people, wageni walivyokuja (waarabu, wareno, wajerumani, waingereza) tuliwakaribisha kwa kuwa positive, wakatulaghai, kutuibia na kutuua. kwa sababu ya kuwa positive sana.
Tulipopata uhuru tukaendelea kuwa positive na umasikini wetu wote, tunawapigia kura watu walewale miaka nenda miaka rudi, tunatumaini mambo yatatengemaa yenyewe.
Migodi inaanguka na kufukia watu, rais wetu badala ya kutafuta sababu za kisayansi ili kuboresha migodi, anatupa maneno positive, kazi ya mungu hiyo tu, tuko too positive.
Tunamuhitaji Kiranga atuambie kwamba dunia si positive tuu, ina positive na negative, kuna majambazi, funga mlango.Kuwa macho, linda chako, usiamini amini watu tu siku hizi kuna matapeli n.k, n.k
Kwa hiyo unaponiona nakuwa na maswali mengi sana ambayo unaweza kuyaona negative, ni ukweli kwamba nyakati zetu zimebadilika, huwezi kuwa positive positive tu, ukiwa positive positive tu hata hutavaa mpira kujikinga, utaenda kuwa positive kweli kweli na HIV.
This is a time to test negative, not positive.