BRYANSK: Makombora ya Ukraine yaua watu wawili katika kijiji kimoja ndani ya Urusi

MTZ 255Dar

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2018
Posts
1,149
Reaction score
3,963
Watu wawili wameuawa ikiwa ni matokeo ya mashambulizi kutoka Ukraine yaliyokilenga kijiji kimoja ndani ya mkoa wa Bryansk ndani ya Urusi. Hayo yamesemwa na Gavana wa mkoa huo kama alivyonukuliwa na chombo cha habari cha Urusi TASS.

Mashambulizi hayo yalikipiga kijiji cha SUZEMKA kilichopo mashariki mwa mpakani mwa nchi hizo mbili. Gavana wa mkoa huo, Alexander Bogomaz alisema siku ya jumapili kwa mjibu wa TASS-Chombo cha habari kinachomilikiwa na Serikali ya Urusi. Kwa mjibu wa tathmini ya kiusalama iliyofanyika, jengo moja la makazi ya Raia liliharibiwa kabisa huku nyumba zingine mbili zikiharibiwa kidogo, alinukuliwa Gavana huyo akisema.

Hayo yakijili, zaidi ya vijiji 4 katika mkoa wa mpakani wa Urusi wa Belgorod havina umeme baada ya ndege 3 zisizo na rubani kuharibu vituo 6 vya kuzalisha umeme.

Hapa najaribu kuuliza
Hivi yale maneno ya Dmitry Medvedev kwamba endapo ardhi ya Urusi ikiguswa, basi Urusi itajibu kwa Nyuklia bado yanaishi au ilikuwa ni kwara mbuzi?

Jana Jumamosi, Ukraine walisambaratisha kabisa ghala la kuhifadhia mafuta mwambao mwa Sevastopol ndani ya mkoa wa Crimea. Kama haitoshi, Ukraine ilitumia Drones 3 kuharibu vituo 6 vya kuzalisha umeme ndani ya Urusi katika Mkoa wa Belgorod na kuviacha vijiji 4 bila nguvu ya umeme. Sasa leo tena kama haitoshi Jumapili ya leo Warusi 2 wamekufa baada ya Ukraine kukishambulia kijiji cha SUZEMKA katika mkoa wa BRYANSK ndani ya Urusi. Hizo Nyuklia za Medvedev zinasubiri nini? Au hazina Mafuta ya kurukia?

Attack on village inside Russian territory follows drone raid on fuel storage facility in Russia-annexed Crimea. Ukrainian shelling of Russian village kills two, governor says
 
Na inasemekana hii spring counter offensive inakuja kushangaza sio Urusi tuu na dunia Bali na waukraine wenyewe.

Inaonekana term hii Ukraine na yeye anaenda kuteka baadhi ya maeneo ya Urusi Kama karata ya kumlazimisha aondoke kwenye mipaka yake.
May be make jana inasemekana wanajeshi wa Ukraine waliingia ndani kabisa ya mji wa KURSK ndani ya Urusi, majibizano ya risasi yalisikika na milipuko kadhaa,.
 
Uingereza apeleke yale makombora ya masafa marefu ila vita iwe na mizania nzuri, tunataka tuone Moscow ikishambuliwa.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Nchi za Magharibi katika vitu wanavyoogopa kwenye hii vita basi ni Kumubana Urusi harakaharaka. Endapo Urusi ikitaitiwa kabisa ikakosa namna basi Nchi za Magharibi zinaogopa Putin anaweza kuamuru matumizi ya Nyuklia ili wakose wote, na ndio maana mpaka hii leo unaona wanaisaidia Ukraine kidogo kidogo.
 
Ni kweli, ila hii misaada midogo midogo hamtikisi Urusi vizuri. West wanataka wamchoshe kidogo kidogo, ila wampe silaha hata chache za kuleta matokeo kwa haraka.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Na inasemekana hii spring counter offensive inakuja kushangaza sio Urusi tuu na dunia Bali na waukraine wenyewe.

Inaonekana term hii Ukraine na yeye anaenda kuteka baadhi ya maeneo ya Urusi Kama karata ya kumlazimisha aondoke kwenye mipaka yake.
Atapitisha wapi silaha kuweka teka hayo maeneo ya ndani ya ardhi ya Urusi?
 
Nchi za Magharibi katika vitu wanavyoogopa kwenye hii vita basi ni Kumubana Urusi harakaharaka. Endapo Urusi ikitaitiwa kabisa ikakosa namna basi Nchi za Magharibi zinaogopa Putin anaweza kuamuru matumizi ya Nyuklia ili wakose wote, na ndio maana mpaka hii leo unaona wanaisaidia Ukraine kidogo kidogo.
Ila kinachofurahisha ni uwezo wa Ukraine kuendelea shikilia Bakhmut.
 
Mkuu Urusi alisema mengi sana na alishindwa kutekeleza zile zilikuwa ndaro tu, sasaiv US na magharibi yule jamaa washamjua ndani nje kwamba anapigika vibaya sana, kabla US walifanya siri kupeleka silaha Ukrean lakini sasa ni wazi wazi tena hakuna kificho hata Poland kabla aliogopa kupeleka zile ndege lakini sasa Poland juzi alivyoenda Zelensky wako mstari wa mbele kupeleka silaha

Poland saivi ndio kuna kituo mahususi cha kufanya matengenezo ya zile Patriots zilizotoka US incase zikipata matatizo zifanyiwe matengenezo haraka ili zirudi kazini

Putini aliutisha ulimwengu kwa maneno ya mdomo jamaa walitumia sayansi ya hali ya juu kumsoma, walipoona anaivamia Ukrean kwa msafara mrefu wa vifaru vya USSR 64km long wakaanza kupata picha jamaa hana technologia hana chochote ngoja tumtie adabu

Mpango wa US ni kumshughulikia Putin kwa style wanayoitaka wao na ndicho kinachotokea. Kwisha dikteta
Attack on village inside Russian territory follows drone raid on fuel storage facility in Russia-annexed Crimea. Ukrainian shelling of Russian village kills two, governor says
 
Mkuu Urusi alisema mengi sana na alishindwa kutekeleza zile zilikuwa ndaro tu, sasaiv US na magharibi yule jamaa washamjua ndani nje kwamba anapigika vibaya sana, kabla US walifanya siri kupeleka silaha Ukrean lakini sasa ni wazi wazi tena hakuna kificho hata Poland kabla aliogopa kupeleka zile ndege lakini sasa Poland juzi alivyoenda Zelensky wako mstari wa mbele kupeleka silaha

Poland saivi ndio kuna kituo mahususi cha kufanya matengenezo ya zile Patriots zilizotoka US incase zikipata matatizo zifanyiwe matengenezo haraka ili zirudi kazini

Putini aliutisha ulimwengu kwa maneno ya mdomo jamaa walitumia sayansi ya hali ya juu kumsoma, walipoona anaivamia Ukrean kwa msafara mrefu wa vifaru vya USSR 64km long wakaanza kupata picha jamaa hana technologia hana chochote ngoja tumtie adabu

Mpango wa US ni kumshughulikia Putin kwa style wanayoitaka wao na ndicho kinachotokea. Kwisha dikteta
akili zenu sijui vipi kwa hiyo hako kashambulio kamoja ndio imekuwa habari ya mjini kwenu wakati huko ukraini ardhi inasepa mdogo mdogo mpaka huko kiev itasombwa yote .....
 
Huna akili Putini alipoivamia ukrean aliingia hadi Kyiv, jeshi la ukrane wakamtoa adui katika miji yote ya Kyiv ambapo sasa ametupwa huko pemben pemben Bakhmut ambako ni mipakani na russia na kama unazo taarifa za leo Bakhmut wale majanjaweed wa Wagner wametishia kujitoa vitani kwa namna wanavyouliwa kwa mkupuo na kuilalamikia Moscow hawana silaha za kutosha.

Ukrean sasa ndio wanarudisha ardhi yao baada ya mvamizi kuiteka alipovamia, unaambiwa eneo ambalo Urusi ilishaliteka Ukrean ni mfano wa eneo la nchi ya Newzerland sasa amefurushwa kila kona na jana Cremea vituo vya silaha na mafuta vimeripuliwa mnyama anataka kuikomboa Cremea sasa. muda utaongea
 
kaa kwa kutuliaView attachment 2605057
Screenshot_20230429-122658.jpg
 
Back
Top Bottom