BSc in Metallurgy and Mineral Processing Engineering

miikky

Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
31
Reaction score
0
Ushauri kuhusu hiyo mambo hapo juu. Kuhusu upatikanaji wa ajira mtaani
 
Ushauri kuhusu hiyo mambo hapo juu. Kuhusu upatikanaji wa ajira mtaani

hii inahusiana sana na uchimbaji na kuprocess madini vyuma!! na kama sikosei ipo udsm, katika kozi hii utajifunza chuma kuanzia uchimbaji mpaka matumizi!! ajira mara nyingi ni serikalini na secta binafsi, migodini.... Ndahani embu pita na huku...
 
Last edited by a moderator:
Soma mechanical au civil hizi habari za madini Tz zilishapitwa na wakati,most of mines life iko at the end
 
sector ya madini Tz ndio bado inaanza,kuna reserves nyingi tu ambazo bado hawajaanza kuchimba. Serikali ina mpango wa kuanza kuchimba base metals kuanzia mwakani kwa hiyo ajira zitakuwepo tu.

Dogo akisoma hiyo kitu atakuja ajute.serikali ya bongo haieleweki na haiaminiki
 
Kuna mgodi was chuma unaanzishwa kule kusini mwa TZ huu utakuhusu sana
 
Hiyo experience ataipata wapi kwanza bila kufanya kazi hapa nchini kwetu kwani elimu yetu ni theoretical zaidi so hata kama nje kutakuwa na fulsa lakini hazitamuhusu.since 2007 tuna graduates wengi tu Wa hizo fani from udsm,Dit na chuo cha madini but still most of them wapo tu mitaani na tatizo sio kiwango cha ufahulu
 
Tunao waswahili wengi wanaofanya kazi nje ya nchi Kama Congo,Mali,Msumbiji,
Ghana,bostswana na SA wengine wameenda mbali zaidi mpaka america ya kusini but wote hawa walianza kwa kupata experience hapa nchini na ndo wakapata hizo chance huko,but kwa sasa hali ni ngumu graduates wapo mitaani hizo kazi watajifunzia wapi ili nao wapate experience waweze kupata hizo fursa.in short madini industry kwa sasa ni ngumu Sana kwa vijana
 
Kwa yeyote anayefikiria kusoma chochote kile kinacho husu sekta ya madini namwomba ajifikirie mara mbili. Hii sekta kwa sasa haina kichwa mara miguu kwani sera ya ccm kwa sasa ina focus kwa wachimbaji wadodo wadogo ambao hawatoi ajira rasmi na wala hawaajiri graduates. Kwa sasa eneo lolote la utafiti likivamiwa na wachimbaji wadogo wadogo wao ndo wanasikilizwa kuliko mwenye eneo kihalali. Kwani, wao ni mabingwa wa kutoa bahasha za mlungula, rejerea suala la Nyangalata la Bwana Tuna .

Hivyo, kwa sasa utafiti wa madini nchini ni kama umesimama vile kwani hakuna anaye upa kipaumbele. Madhara yake ni kuwa Migodi iliyopo kwa sasa ikifungwa hakutakuwa na migodi mipya yakuweza kuajiri workforce itakayo temwa na hiyo migodi. Mathalani, Tulawaka imefungwa na kuchukuliwa na serikali baadhi ya wafanyakazi wakapelekwa Buzwagi wengine waliachishwa kabisa. Tangia JK ameingia hakuna mgodi mpya ulioanza kufanya kazi hivyo kwa wale graduates wapya ndani ya miaka tisa ya JK wako wapi?

Kwenda nje ni ngumu sana kwa sasa hasa unapokuwa fresh from school kwani nchi nyingi zimeanza kulinda soko la ajira la nchi zao. Botswana kwa sasa kampuni ikiajiri mgeni mmoja ni lazima iajiri wazawa watano! Hivi karibuni nilikuwa Zambia, wakati napigiwa mhui wa viza askari alisoma passport yangu alipoona nina utaalamu wa madini haraka akaniuliza kama nakuja kufanya kazi. Nilipo kata akanijibu ukifanya kazi tu tutakukamata na kukurudisha kwenu!!!

Kozi zozote za madini zilishafikia maturity na good days zimeshapita kwa sasa ni shida mtupu!!!!Hii, ni sawa na computer science Enzi zile za miaka ya tisini ilikuwa hotcake nowadays?????

FIKIRIA MARA MBILI
 
Ushauri kuhusu hiyo mambo hapo juu. Kuhusu upatikanaji wa ajira mtaani

Ajira kwa mining engineers sio mbaya sana...isipokuwa cha msingi wewe unaipenda hiyo kozi hapo juu au unataka kusoma kwa sababu ya ajira? Ajira zinaweza zikawepo leo, kesho mdodoro wa uchumi ukaja zikakimbia...what are you going to do? Haina maana ulichosoma hakitakuwa na matumizi....ila ajira ndio zinasumbua tu. Mi nafikiri usome kama unaipenda hiyo kozi na sio kusomea kuajiriwa.
 
hii inahusiana sana na uchimbaji na kuprocess madini vyuma!! na kama sikosei ipo udsm, katika kozi hii utajifunza chuma kuanzia uchimbaji mpaka matumizi!! ajira mara nyingi ni serikalini na secta binafsi, migodini.... Ndahani embu pita na huku...

Ni kweli mkuu ndio wanao extract minerals from the ores and processing/refining it to the very end.Lakini huyo bwana anauliza asome ili akaajiriwe....hapo pagumu sana kama ajira hazitakuwepo...ila kama anaipenda hiyo fani he will make it.
 

Mkuu haupo serious nchi nzima wapo 35,my be Una data za mwaka sabini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…