BSS ina uchawi gani?mbona wengi hawafanikiwi?

BSS ina uchawi gani?mbona wengi hawafanikiwi?

brigedia mafia

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2016
Posts
2,260
Reaction score
2,279
Waungwana leo kwenye pita pita yangu nilikutana na miongoni mwa washiriki wa BSS aliyekuwa miongoni mwa waliofanya vizuri (jina kapuni) akiwa kachoka sana mpaka nikamuonea huruma, sasa nikawa najiuliza hivi hili shindano lina manufaa gani? Kwa nini washiriki wengi hawafanikiwi na majina yao hufifia baada ya muda mfupi?

Tuchukulie mfano mtu kama Jumanne Idd mpaka leo hajulikani halipo alkadharika Walter Chilambo, Kayumba , AngelMarry Kato , Steven Lupenza, Nasibu Fonabo nk ni miongoni mwa vijana ambao wana uwezo mkubwa sana wa kuimba lakini cha ajabu hawafanikiwi kulinganisha na washiriki wengine kama vile Harmonize ingawa alitoka mapema na kuonekana si chochote leo hii katudhihirishia kwamba yeye ana uwezo gani

Si harmonize tu pia nina mdogo wangu nisingependa kumtaja jina kwa sababu zangu binafsi ,naye pia alitolewa kwa maneno ya shombo na Salma Jabir kwa kuambiwa hajui kuimba bora akafuge kuku ndio kazi anayoiweza lakini leo hii ni msanii mkubwa tu

Hawa ni baadhi ya washiriki wa bss ambao washapotea kwenye ramani ya mziki

1475701087496.jpg
huyu ni kayumba junior

1475701151748.jpg
huyu ni Nasibu Fonabo

1475701206857.jpg
huyu ni Favolii

1475701275823.jpg
huyu ni Stev Lupenza

1475701335244.jpg
Emmy Wimbo

1475701435570.jpg

1475701531678.jpg
Angermarry Kato

1475701630282.jpg
Frida Amani AKA queen fifi

Ujue muda mwingine mpaka nawaza, hivi hawa vijana wanafataga mpunga tu au? Maana huwa siwaoni kabisa shindano likiisha ,maana hupotea maziiiiiiima
 
Attachments

  • 1475701575126.jpg
    1475701575126.jpg
    128.1 KB · Views: 12
Wameshakatishwa tamaa na kile kitambi cha mwenzao Peter Msechu.

BSS = Kitambi turubai
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Safi
Kwanza ni jambo la kujiridhisha kuwa si BSS tuu bali hata huko nje shows kama za the voice, SA idols, xfactors, na Got talents za nchi nyingi, ni watu wachache sana walio shinda mashindano ya aina hii wame make ki muzik.
Kwanini!!?
1. Lengo la mashindano, waandaji huwa wanaandaa kwa ajili ya faida yao na kupata wadhamini, na mara nyingi wakisha maliza shindano hawawekezi kwa nguvu kubwa kwani kuna shindano la mwakani inabidi waandae tena, hawana time na wewe
Pia washindanaji lengo lao kubwa zaidi ni kupata yale mamilioni tuu, wakisha pewa kuna msemo unasema easy come easy go
2. Mashabiki wa mashindano, askudanganye mtu, watanzania wanao fuatilia BSS ni chini ya milioni 10, wanao piga kura ni chini ya laki moja, kwa hiyo kama msanii ukishinda unakuwa hujapata fan base kubwa bado isipo kuwa ki portion kidooogoo cha wale walio angalia na wakajisumbua hata kupiga kura,,na wengi wanai piga kura huwa wanaanza kwanza kukuonea huruma ya kimaisha mfano unakumbuka Jumaanne Idd kwa hiyo Raymond akitoa wimbo mmoja uka hit anapata fan base kubwa kuliko wewe mshindi
3. Mziki ni zaidi ya kukopi nyimbo za watu, angalia yule mshindi wa mwaka jana kayumba alishnda kwa kuimba imba taarab za kina isha mashauz sasa je akitoka BSS ana uweza huo mziki!!? Mpaka yeye mwenyewe hajui afanyeje yaani

*sababu ni nyingi lakini kikubwa ni wasanii wajiamini wajue uwezo wao ni zaid ya kuimba BSS, ndio maana mara nyingi unakuta wanao fanikiwa ndio wale walio shika u tano, au ukumi, kwa kuwa it takes more than to win BSS ili kuwa msanii

Sor gazeti refu kidogo
 
Safi
Kwanza ni jambo la kujiridhisha kuwa si BSS tuu bali hata huko nje shows kama za the voice, SA idols, xfactors, na Got talents za nchi nyingi, ni watu wachache sana walio shinda mashindano ya aina hii wame make ki muzik.
Kwanini!!?
1. Lengo la mashindano, waandaji huwa wanaandaa kwa ajili ya faida yao na kupata wadhamini, na mara nyingi wakisha maliza shindano hawawekezi kwa nguvu kubwa kwani kina shindano ka mwakani inabidi waandae tena, hawana time na wewe
Pia washindanaji lengo lao kubwa zaidi ni kupata yale mamilioni tuu, wakisha pewa kina msemo unasema easy come easy go
2. Mashabiki wana mashindano, askudanganye mtu, watanzania wanao fuatilia BSS ni chini ya milioni 10, wanao piga kura ni chini ya laki moja, kwa hiyo kama msanii ukishinda unakuwa hujaoata fan base kubwa bado isipo kuwa ki portion kidooogoo cha wale walio angalia na wakajisumbua hata kupiga kura,,na wengi wanai piga kura huwa wanaanza kwanza kukuonea huruma ya kimaisha mfano unakumbuka Jumaanne Idd kwa hiyo Raymond akitoa wimbo mmoja uka hit anapata fan base kubwa kuliko wewe mshindi
3. Mziki ni zaidi ya kukopi nyimbo za watu, angalia yule mshindi wa mwaka jana kayumba alishnda kwa kuimba imba taarab za kina isha mashauz sasa he akitoja ana uweza huo mziki!!?

*sababu ni nyingi lakini kikubwa ni wasanii wajiamini wahue uwezo wao ni zaid ya kuimba BSS, ndio maana mara nyingi unakuta wanao fanikiwa ndio wale walio shika u tano, au ukumi, kwa kuwa it takes more than to win BSS ili kuwa msanii

Sor gazeti refu kidogo
sawa sawa mkuu Iceman uko sahihi kabisaaa
 
Ujanja ujanja mwingi wa waandaaji.Wanalenga kupata wadhamini kisha wakimaliza show hakuna muendelezo.
 
Huwez kuwa msanii kwa kuimba nyimbo za wenzako mwanzo wa mashindano hadi mwisho wa mashindano...kila mtu aimbe nyimbo binafsi Ili awe na uwezo baada ya bss
 
Hawa jamaa wangefanya washiriki wawe wanaimba nyimbo zao wenyewe na sio za watu maana inaonekana washiriki wengi wa BSS wana vipaji vya kuimba nyimbo za watu na sio kutunga zao wenyewe.
Kwan lengo la shindano ni kusaka mtunzi bora?
Maana nijuavyo mtu unaweza kuwa mtunzi mzuri na usijue kuimba na viceversa is true.......
So kuna wengine ni mastaa wakubwa na hawajui kutunga mashairi rejea recho,linah wa tht ila wana sauti za kuimba....hiyo ni mifano tu ila wapo wengi sana...
Hao wanapotea kwasababu shindano lenyewe limejaa figisufigisu kama siasa za bongo..anayeshinda hastahili na anayeshindwa hastahili pia....

Kala jeremia,peter msechu, hawakushinda ila wanafanya vzr sana wale washindi wote kapuni hakuna hata mmoja aliyetoboa

Aibu kwao waandaaji....
 
Huwez kuwa msanii kwa kuimba nyimbo za wenzako mwanzo wa mashindano hadi mwisho wa mashindano...kila mtu aimbe nyimbo binafsi Ili awe na uwezo baada ya bss
Uwezo wa kutunga nyimbo sio muhimu sana, Rihanna ni msanii mkubwa lakini mpaka leo hajawahi kutunga wimbo wowote tangu aanze kuimba ,yeye anatungiwa tu ,kazi yake yeye kuimba basi
 
Uwezo wa kutunga nyimbo sio muhimu sana, Rihanna ni msanii mkubwa lakini mpaka leo hajawahi kutunga wimbo wowote tangu aanze kuimba ,yeye anatungiwa tu ,kazi yake yeye kuimba basi
Ni kweli mkuu anatungiwa lakini ni nyimbo mpya hazirudiwi nyimbo za watu.. vjana hawajengwi kisaikolojia kuwa after bss kuna gem la competition zaidi so ni easy kuwapoteza...
 
BSS za Tz huwa naona mizaa ni mingi sana na watu hawako serious, sijui wanatumia vigezo vipi kuwapata washiriki.

Mtu anakuja kushindana anaanza kutoa mkate anakula, mara mwingine kaja na nyoka, mara mwingine anaanza kumtamani Salama na ujinga ujinga mwingi unaofanana nahuo.

Nadhani hawachagui kweli wale wenye vipaji vyao kuimba na kutunga nyimbo zao badala wanachagua wengi wenye vipaji vya kuimba nyimbo za wenzao. Na hii ndio hupelekea wengi kupotea kusiko julikana hata kama walishinda.
 
Safi
Kwanza ni jambo la kujiridhisha kuwa si BSS tuu bali hata huko nje shows kama za the voice, SA idols, xfactors, na Got talents za nchi nyingi, ni watu wachache sana walio shinda mashindano ya aina hii wame make ki muzik.
Kwanini!!?
1. Lengo la mashindano, waandaji huwa wanaandaa kwa ajili ya faida yao na kupata wadhamini, na mara nyingi wakisha maliza shindano hawawekezi kwa nguvu kubwa kwani kuna shindano la mwakani inabidi waandae tena, hawana time na wewe
Pia washindanaji lengo lao kubwa zaidi ni kupata yale mamilioni tuu, wakisha pewa kuna msemo unasema easy come easy go
2. Mashabiki wa mashindano, askudanganye mtu, watanzania wanao fuatilia BSS ni chini ya milioni 10, wanao piga kura ni chini ya laki moja, kwa hiyo kama msanii ukishinda unakuwa hujapata fan base kubwa bado isipo kuwa ki portion kidooogoo cha wale walio angalia na wakajisumbua hata kupiga kura,,na wengi wanai piga kura huwa wanaanza kwanza kukuonea huruma ya kimaisha mfano unakumbuka Jumaanne Idd kwa hiyo Raymond akitoa wimbo mmoja uka hit anapata fan base kubwa kuliko wewe mshindi
3. Mziki ni zaidi ya kukopi nyimbo za watu, angalia yule mshindi wa mwaka jana kayumba alishnda kwa kuimba imba taarab za kina isha mashauz sasa je akitoka BSS ana uweza huo mziki!!? Mpaka yeye mwenyewe hajui afanyeje yaani

*sababu ni nyingi lakini kikubwa ni wasanii wajiamini wahue uwezo wao ni zaid ya kuimba BSS, ndio maana mara nyingi unakuta wanao fanikiwa ndio wale walio shika u tano, au ukumi, kwa kuwa it takes more than to win BSS ili kuwa msanii

Sor gazeti refu kidogo
Umeeleweka vzur sana brother,,,
 
Back
Top Bottom