Buberwa: Watawala wanaamini kwasababu wao wana silaha, wanaweza kumkamata Raia wakati wowote, hii haimalizi tatizo

Buberwa: Watawala wanaamini kwasababu wao wana silaha, wanaweza kumkamata Raia wakati wowote, hii haimalizi tatizo

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mchambuzi wa masuala ya siasa Kaiza Buberwa amebainisha kuwa nchi inaendelea kukabiliwa na changamoto za kisiasa kwa sababu watawala wamekuwa wakiahirisha matatizo badala ya kuyapatia ufumbuzi wa kudumu.

Amesisitiza kuwa Katiba ni mamlaka ya raia kuweka mwongozo wa jinsi nchi inavyopaswa kuongozwa, ikijumuisha mfumo wa kisiasa, sheria, na utawala, lakini bado kuna ukosefu wa mawasiliano na uelewa wa pamoja kati ya raia na watawala kuhusu mamlaka haya.

 

Screenshot_20260404-111943~2.png
 
Kweli kabisa. Nilishangaa sana Kuna mwanaccm anasema Heche apewe kesi ya uhaini, kisa anaiponda serikali.
 
Back
Top Bottom