The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Makada nane wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Jimbo la Buchosa wamekihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Hatua hii imetokana na kuridhishwa na kazi zinazotekelezwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo.
Miongoni mwa waliokihama CHADEMA ni Salum Herman, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Katwe, na Thobias Dema, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA Jimbo la Buchosa.
Pia soma: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Wakizungumza kwa pamoja, wamesema wameamua kujiunga na CCM baada ya kushuhudia kasi ya maendeleo chini ya uongozi wa Rais Samia. Aidha, wameeleza kuwa kwa sasa CHADEMA haina hoja za msingi za kuikosoa serikali kutokana na utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo nchini.