Buchosa: Wananchi walalamika kutozwa faini ya 50000 kwa kutokuwa na vyoo na bafu bila kupewa risiti

Buchosa: Wananchi walalamika kutozwa faini ya 50000 kwa kutokuwa na vyoo na bafu bila kupewa risiti

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Buchosa. Baraza la madiwani Halmashauri ya Buchosa Wilaya ya Sengerema mkoani limelaani kitendo cha ofisa afya kata ya Maisome, Robert Masubugu kutoza faini wananchi bila kuwapa risiti.

Wanaotozwa faini ni wale waliokutwa na makosa na kutokuwa na vyoo na mabafu.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne Februari 9, 2021 baada ya diwani wa Maisome, Dauson Miyaga kulieleza baraza hilo kwamba kuna malalamiko ya wananchi kutozwa faini ya Sh50,000 kila mmoja na hawapewi risiti na kuzua maswali mengi kuhusu suala hilo.

“Fedha za Serikali zinapotea watu wanaweka mifukoni mwao tunapaswa kuliangalia suala hili kwa mapana na kuokoa fedha hizi," amesema Miyaga akibainisha kuwa kuna mazoea ya maofisa wa Serikali kufanya misako kwa wananchi na kutoza faini bila kutoa risiti.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa, Crispin Luanda amesema hajui lolote kuhusu suala hilo na kuwataka madiwani kumpatia muda ili afanye uchunguzi ili aweze kuchukua hatua stahiki.

Hivi Karibu kumekuwa na malalamiko ya baadhi ya watumishi hasa wa ngazi ya kata ya vijiji kutotoa risiti na baadhi kuendesha msako wa walioshindwa kujenga choo na bafu.

Ofisa afya wa Maisome, Robert Masubugu amesema hajawahi kutoza mtu yoyote fedha akiwa na makosa ya kutokuwa na choo wala bafu, kwamba anachofanya ni kutoa elimu ili jamii itambue umuhimu wa choo na bafu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa, Idama Kibanzi amemwagiza mkurugenzi kuchunguza tuhuma hizo na ikibainika achukuliwe hatua za kinidhamu.
 
Lisemalo lipo kama halipo laja. Cha msingi uchunguzi ufanyike kujidhihirisha na jambo husika, maana wananchi kwa kuzusha mambo hawajambo. Na kwanini wasijenge choo mpaka wafuatwena maofisa wa serikali ila CCM ilipotufikisha huku yani miaka 60 ya uhuru bado tunapigana faini za kuwa na choo na tunajiita tupo uchumi wa kati.

#MaendeleoHayanaChama
 
Usukumani mna matatizo gani? Choo pia mpaka mpigiwe parapanda.

Tuna safari ndefu sana.
 
Back
Top Bottom