NIlinunua gari kutoka kampuni ya Budget Holdings ya Japan, nikafanya malipo mwezi wa sita, hadi sasa hawajaweza kunitumia gari, nilipoona wameshinda kununua gari lile nililotaka, nikawaambia wanirudishie pesa yangu. Hapo ndipo imekuwa ubabaishaji, nimepiga simu na kuwaandikia email, lakini wanatoa ahadi ambazo wameshindwa kutekeleza, ninaona kuna hatari mbele. Je kuna hatua gani naweza kuchukua ili kupata pesa zangu? Naomba msaada katika hilo.