Asante kwa majibu na estimate hiyo. Kwa uhakika nyumba ni nzuri. Ila kweli inabidi mtu kujiandaa haswa ukitaka kitu kizuri. Maana niliambiwaga finishing ya nyumba inagharimu almost sawa na gharama ya kujenga boma. Kwa maana hiyo nyumba kama hiyo mpaka ikamilike ni kama 300M. Dah! Ila ipo siku ndoto yangu ya kujenga itatimia. Inaweza isiwe ghorofa kama hilo, lakini nyumba isiyo ya ghorofa lakini nzuri. Nimeanza kuwekeza, na so far niko kwenye 60M. Mdogo mdogo tu na Isnhaalah ipo siku mtaniona ofisini kwenu. Nimependa kazi zenu.