Bujibuji na Mshana Jr, wanamtongoza mpenzi wangu Kichawi

Habari zenu wakuu,

Nimeingiwa na wasiwasi sana, nina mpenzi wangu nampenda sana, lakini hivi karibuni ameanza kubadilika.

Kila muda nikionana naye ananipa stori za mshana jr na Bujibuji, anadai amewafahamia JF. Anataka eti wamfundishe kujikinga na wachawi, hivyo anawatafuta. Kumbuka hajui kama mimi nipo JF, wala hajui kama najua wanavyoleta thread za kichawi.

Anadai eti anamtafuta Bujibuji ili ampe dawa ya kuona wachawi na kugundua nyoka wa Kichawi.

Mshana anataka ampe dawa na kujikinga na majini. Wiki mbili sasa akilala anaweweseka, anaota na kutamka maneno kwa Sauti. Kilichofanya niandike hapa, ni baada ya jana kuota na kusikia maneno akitamka kabisa BUJI, ikabidi nimuamshe, akasema nimemsikia vibaya alikua anaota akinywa Uji.

Mke wangu mwenyewe kila siku namuona kule MMU.

Naombeni msaada ili mpenzi wangu asichepuke kwani bado nampenda. Na hawa watu wanaomtongoza kwa dawa nawaogopa sana.
Unamaanissha mpenzi au mke?
 
Mwambie hizo wanazofundisha wakina Mshana jr na Bujibuji ni theory tu.
Akitaka ukombozi wa ukweli amtafute bingwa wa matatizo yote asiyeshindwa kitu anakwenda kwa jina la Yesu Kristo.
 
Mkeo kapost hapo juu kwa Id tofauti,,,kashajua mama wote mpo huku
 
Nasikia mshana anaweza kuja ucku akala mzigo kisha akasepa bila ya wew kumuona..!! Nakushaur uwaombe suluhu hawa jamaa..!
 
Huyu mleta mada atakuwa mtoto wa kiume.watu kama hawa ndo wanasababisha wanaume wa dar tudharaulike.
 
Back
Top Bottom