Bujiku: Vodacom tumepoteza 30% ya mapato kutokana na Tozo

Mkuu japo voda imepepyngua mapato lakini ndio mtandao unaongoza Tanzania kwa nyanja zote
Nipende kutoa shukrani zangu za dhati toka niwasusie huduma zao za vifurushi week hii yote wananigea 200MB kila asubuhi na dkk 15 bure wakihisi ntawasamehe uovu wao wa kuniibia 5K toka M-PESA Mwezi wa 6
 
Ndio maana tutaendelea kukanyagwa. Mwigulu hawezi kuwa moved na hoja nyepesi kama "uchakavu wa pesa" na uwezo wa BOT "kupima uchumi wa nchi."

You think Mwigulu gives a crap about pesa kuchakaa? Si wataagiza nyingine wapige hela kwenye zabuni.

Politicians can do anything because the people do not know anything.
 
Natabiri atakuja kufuta kauli yake kuhusu tozo kama walivyofanya DStv
 
Ni sahihi inatakiwa mpoteze mapatao hata kwa asilimia 70% zile mia mia mnazoiba kwenye account zetu za salio kuu na sasa kule mpesa napo zimetosha. Endeleeni kuteseka wezi wakubwa msisingizie hata tozo
 
Funguo za kufulia unazitunza wapi?
Pesa inakatwa na benki/ kampuni ya simu, wanakata Tena Kodi kwenye hizo gharama, Bado wanaleta Tena tozo (Sijaelewa hii ni Kodi au kitu Gani?)
Hamna kodi hapo ni wizi mtupu
 
Katika hili tuko pamoja, hawa wahuni ni wezi wa hela zetu. Hilo limechangia sana ile kampeni ya kuwakataa iliamsha watu wengi na kuhamishia majeshi Zantel, Halotel na Tigo
Failures na majizi yanataka yajifiche kwenye tozo Kudanganya share holders wao 😜😜
 
Hawa jamaa wezi sana majuzi wamenikata deni la songesha mara mbili mbili kuuliza wanasema nilikopa mwaka jana
 
Ogopa sana mtu ambaye amekulia maisha ya kimasikini vijijini,akaja mjini kwa kufaulu mtihani na Bado alipofikia kimasomo amekutana na wachunga ng'ombe wenzie na wakulima kidogo.Huwa ni wajuaji sana,nadhani mumemsikia mara kadhaa akisema yeye ni Daktari wa Uchumi,msimlaumu ndiyo upeo wake ulipoishia.
Ata chura akiwa shimoni huwa anaona Dunia yake ni pana sana lakini akitoka nje ya shimo ndiyo anakuja kugundua kumbe alikuwa anajidanganya,Dunia yake ni ndogo.
"Mwanangu Mwigulu endelea kuwanyoosha wapinzani wetu"
 

Airtel Money hakuna Tozo.
Voda watafute njia ya kujiinua as brand. Mbona haisemi kuwa imepunguza almost 40% ya matangazo wa kulaumiwa ni nani…?
 
Airtel Money hakuna Tozo.
Voda watafute njia ya kujiinua as brand. Mbona haisemi kuwa imepunguza almost 40% ya matangazo wa kulaumiwa ni nani…?
Vodacom iko listed ndio maana taarifa zake ziko wazi, Airtel watakuwa wanaugulia moyoni..
 
Tatizo la mkuu wa state kuwaamini wapigaji bila yeye kusimama kidete.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…