BUKAVU: M23 yakuta mlango wa mji wazi

BUKAVU: M23 yakuta mlango wa mji wazi

MBOKA NA NGAI

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2025
Posts
350
Reaction score
576
Habari zilizopo kwa sasa, ni kwamba baada ya wanajeshi wa Burundi na FARDC kukimbia uwanja wa ndege na kukimbilia mjini Bukavu, yawezekana M23 tayari ilikuwa mjini ikiwachora tu. Tofauti na Goma, M23 imewatangazia maeneo ya wazi wanaohitaji kutoka mjini humo, na kweli wanajeshi wa serikali wakachukua magari na kusepa. Baada ya muda, ndipo jeshi la M23 likaonekana likikalibishwa kwa shangwe na raia.

Haya

Baada ya rais wa DRC kuapa hatokaa kuzungumza na M23, wanamkumbusha kuwa safari yao itaishia Kinshasa.

Kwa kasi hii, huko maporini na kwenyewe kutaachwa silaha kama za Kivu kaskazini na kusini? maana M23 inazoa kama hazina mwenyewe

Usafiri sasa, ndo usiseme.Kila aina ya gari,lipo. Wakisamehe, Kivu inajitenga.Wakisonga,basi uwezekano wa mzee Felix kubaki huko huko ulaya ni mkubwa.

1739560182107.png


View: https://x.com/i/status/1890440659594535334


View: https://x.com/i/status/1890446842187641041
 
Kwahiyo Makomandoo wa Burundi wamelala mbele?!😆😆😂😂

Halafu Raisi wa Burundi juzi juzi alikuwa anapiga mkwara mzito sana.
We mkalio weka kwenye benchi, macho kwenye kioo cha simu au computer. Nakuletea kila kinachoendelea.

Kuhusu swali lako, wapo waliotangulizwa mbele ya sijui niite haki, wapo wengine waliojisalimisha, wengime wamezingilwa na kukamatwa.

Si unajua kule aliyeshindwa kupigana na M23, kesi yake kifungo kidogo ni miaka 30!!! Wengine wanahukumiwa maisha. Hapo nani arudi sasa! Inaonekana General Neva nae ameanza kujikaanga kwa mafuta yake mwenyewe.
 
1739561057160.png


Plan hapa ni kuhakikisha M23 wanaingia mlangoni mwa Burundi. Kwa maana adui yao wa kuingia Burundi,labda apitie Zambia.
Inaelekea kuna watu wamecheza na wanajeshi wa kongwe, huku wao bado watoto kwenye mchezo. Je, wanajeshi elfu 10 wa Burundi wanaenda kuwasubilia M23 Bukavu, au watakubali wafie jela!!!
 
Tunakuaminia mwanetu kwa habari nzuri

Vip jeshi la Tanzania haliko huko?
Jeshi la Tanzania lipo kwa ajili ya UN, hilo halijihusishi na vita. Maana moto unaowaka huko kuuota si mchezo.
Pili, rais nae ana hesabu zake. Vifo vinavyoendelea huko,majibu ya kwa nini amewapeleka huko anayo?
Tatu, serikali yenyewe haina msimamo, viongozi wakubwa ni walafi na wasaliti! Hilo jeshi unaliungaje mkono.
Nne, mpaka sasa,kuhusu ule mgogoro kuna pande mbili. Wapo wanaoiunga mkono M23, na wengine wapo upande wa DRC.
Tano, limeshaingizwa swala la ukabila. Unadhani yeye yupo tayari kuhusishwa na mauaji ya kikabila? Amewaachia warundi kwanza wenye ubavu wa kupigana vita.

Ni maoni yangu binafsi lakini
 
Nimesikia Askari wengi Burundi wenye asili ya Kitutsi walikataa kupigana na M23 idadi yao ilikuwa imefikia 250 wamekamatwa kwa kukaidi Amri.
Si kweli.
Hao wapatao 250 kwa sasa wapo na kundi la RED-TABARA. Kusini huko kama unaelekea Lubumbashi, na M23 ndo inaelekea huko. Ukimuona rais wa Burundi ana wasiwasi, ujue kuna jambo, usalama kwake ni mdogo na yeye.

Waliokaidi wamehukumiwa vifo, na miaka 30 mwenye kifungo kidogo. Kwa hiyo, kuna mawili
; Kuwa mfungwa wa vita, au kujiunga na aliekuwa adui ili usogeze siku.

Elfu nne, waliyuma kuhakikisha uwanja wa ndege wa Kavumu haukamatwi. Unadhani kinachowasubiri ni nini?

Ukisikia idadi ya vifo Goma, wengi wakiwa wapiganaji upande wa serikali, ndo ujiulize sasa huko kusini hali ikoje!!! Kwa taarifa zilizopo, baada ya rais kuonyesha nia ya kumaliza kabila la watutsi, M23 inampa ujumbe wa uhakika(Hakika umenielewa).



Usisahau!!! Jeshi la DRC ndo linashikilia nafasi ya 8 ya majeshi bora balani Afrika.

Ngona nikasake habari nyingine ntarudi
 
Sultan Makenga na wenzie kuanzia Bosco "terminator", Mti mkavu aka pastor na wengine wamekulia kwenye hayo mapoli toka enzi za RPF na kamanda wao PK chini ya Babu yao M7 kifupi hao vijana na wazee wa M23 ni war machines, huwezi kuwamaliza na wakiamua kwa hilo jeshi la DRC mapema tu wanafika Kinshasa.

Kinshasa wamefunga anga maana wanajua hao Mulenge Wana roho ngumu wanaweza kushushwa hata karibu na Mbuju Mai wakaanzia hapo kuifuata Kinshasa, wakiishika Bukavu, Ben sio issue maana inapakana na Babu yao M7 siku moja tu wanaiteka then wanakuwa wameizunguka Kisangani, Kisangani inapigwa kutokea Bukavu na Beni, wakimaliza wanaifuata Mbadala kwenye hiyo border na Congo Brazavile asubuhi tu wako Kinshasa, ukumbuke wana airport Goma na hapo Bukavu, ukiruka unaruka low altitude kutokea UG au RA supply ya kutosha.
Vikosi vya DRC supply lazima ifike Kisangani ili kuihami Kisangani wakati huo huo huna ammunition za kutosha kuihami Kinshasa, sasa utachagua kuweka buffer Kisangani ili ikianguka Kisangani iwe imeanguka Kinshasa au urudi ucheze kamari kuihami Kinshasa halafu upige counter attack, lazima yakukute ya Mobutu otherwise uifilisi nchi ukawachukue the retired berets uwamwage Kisangani wapige offensive kuelekea Ben then uirudishe Bukavu.

Pole sana Mr Idiot aka the big fat, uliingia maagano usiyoyaweza, Mulenge are your night ghosts.
 
Back
Top Bottom