Bukoba mambo ya migomba yanaelekea kupotea kwenye makazi ya watu

Hakuna kitu sipendi kama hizi mbegu mpya za migomba. Roho inauma mno zile ndizi za asili zinapotea

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
 
Hakuna jipya hapo hata kule tunakojifunza ustaarabu hayo yapo labda yangetokea kila mara ndo tungeshangaa
 
Ni kweli sio nzuri lakini zinahimili mabadiliko ya hali ya hewa, ila Bukoba bado kuna sehemu nyingi zina migomba ya asili
Siyo bk ty katika suala hilo. Ni kote aisee. Halaf kwa wangoni unaambiwa ndizi mshare tena wa asili mkungu elf 2 tena unabembelezewa. Kiukweli haya ya kisasa hata si matamu.

Enzi hizo moshi pekee ndo ilikua ikiilisha dar na ndizi, ndizi ilikua na thamani kweli hapa sokoni mabibo. Ila sasa hivi, kila pembe wanaleta dar.

Binafsi sitamani vijijini kwetu kabisa mazao ya ndizi yapotee na kahawa. Hakuna kitu nafurahia kama hiyo mandhari aisee. Yaan vikaja potea na mimi siendi tena kijijini. Kuna raha gani sasa. Sema nyie hapo bk ndo makao makuu ya mkoa sijui kama mtaweza handle hii hali ya kukata migomba na mikahawa aisee. Sisi moshi mjini paache pabaki na hekaheka ila jioni watu huenda lala milimani kwenye hewa safi ya mimea.

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…