Ex Spy
JF-Expert Member
- Jan 15, 2007
- 222
- 1,827
Mwili wa raia pekee wa Uingereza aliyefariki ndani ya ndege ya Precison Air, unasafirishwa leo kwa gari kuelekea Mwanza.
Baadaye usiku wa leo, mwili huo wa Jonathan Rose, utasafirishwa kwa ndege kuelekea Dar es Salaam ambako mipango ya kuupeleka London, Uingereza inaendelea.
Nimepata taarifa za uhakika kuwa Muingereza huyo alikuwa mtumishi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) na alikuwa akielekea Bukoba kwa mara ya kwanza.
Aidha, mebainika kuwa jeneza lenye mwili wa Muingereza huyo liliondoshwa chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospital ya Rufaa ya Bukoba saa 3.44 asubuhi.
Ubalozi wa Uingereza wanazo taarifa za kutokea kwa kifo cha raia wao na kwamba unashiriki kikamilifu kuhakikisha mwili wake unafikishwa kwa familia yake haraka iwezekanavyo.