Bukoba: Watu 8 wafariki dunia na 6 kujeruhiwa katika ajali ya gari eneo la Rwamishenye

Bukoba: Watu 8 wafariki dunia na 6 kujeruhiwa katika ajali ya gari eneo la Rwamishenye

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Watu sita wamefariki dunia na wengine tisa kujeruhiwa katika ajali ya gari, linalofanya safari zake kati ya Kemondo na Bukoba Mjini, ajali hiyo imetokea maeneo ya Rwamishanye Bukoba..( dakika 14 zilizopita )

Chanzo: Habari Leo Online


--UPDATE--


Watu nane wamefariki dunia na wengine sita wanapatiwa matibabu katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera baada ya gari walilokuwa wanasafiria kukatika mfumo wa breki kabla ya kutumbukia shimoni.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, Revocatus Malim basi hilo dogo linalofanya safari zake Kemondo na Manispaa ya Bukoba limepata ajali katika barabara ya Uganda, Mtaa wa Rwamishenye.

Ameeleza kuwa gari hilo aina ya Toyota Hiace lenye namba za usajili T471DCG lilikuwa linatokea Kemondo na kwenda Bukoba Mjini jana.

Alisema kuwa Polisi wanamshikilia dereva wa gari hilo, Ismaili Rashid.

Kemondo.jpeg

-----
Siku zingine Watani zangu muwe mnajitahidi tu kabda ya Kusafiri muwe mnahakikisha kuwa mmeshatambika katika hiyo Migomba yenu na hizo Ndizi.
 
Waliofariki ajali ya gari aina ya Hiece namba T 471 BCG Mkoani Kagera usiku wa kuamkia leo wafikia nane miongoni mwao akiwemo mwanamke mjamzito aliyepoteza maisha baada ya kufikishwa kwenye eneo la Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Kagera kwa ajili ya matibabu.
 
So sad,

Pale Rwamishenyi kuna mteremko mkali sana na watu wanafanya biashara barabarani ni vema madereva wakawa waangalifu jamani.
Mungu azilaze roho za marehem mahali pema
 
pole kwa ndugu zetu watanzania, tunawaombea wapumzike kwa amani.
 
Back
Top Bottom