Mvua kubwa iliyonyesha takribani saa tatu katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, imesababisha zaidi ya nyumba 300 katika mitaa ya Omukigusha, Byekela na Nyamkazi kuzingirwa na maji huku baadhi ya barabara zikifungwa ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.