A
Anonymous
Guest
Nina malalamiko kuhusu Kuanzishwa kwa Dampo (Jalala) Katika Nyumba ya Serikali, Eneo la Ntengere – Igulwa, Bukombe, katika kuliweka hili sawa kuna ushahidi wa picha zinazolionyesha eneo hili kwa hatua zaidi ambazo zitachukuliwa.
Katika picha hii ni hali halisi ya dampo, dampo hili limevuka eneo hilo la nyumba hiyo na hawa tunaowaona katika picha hii ni wanaotupa taka na wengine ni waokota makopo. Wanaotupa taka wanatupa ovyo ndio wamepelekea mpaka kufikia hali hii ya eneo hili ambalo napinga vikali hali hii ya eneo hili. Napenda kuwasilisha malalamiko haya kwa mamlaka husika kuhusu hali ya mazingira hatarishi inayojitokeza katika mtaa wa Ntengere, Kata ya Igulwa, kwenye nyumba/kota ya serikali karibu na kanisa la SOSELA ambayo hapo awali ilikuwa inakaliwa na watumishi wa umma.
Hii ni baada ya mtumishi wa mwisho aliyekua akikaa kwenye nyumba hii kuondoka, imekuwa haina mkazi lakini bado ipo katika hali nzuri nisuara la kuifanyia marekebisho kidogo na kuingia mtu, ina mahitaji yote ikiwa na umeme, uzio na kisima cha maji. Hata hivyo, eneo hili sasa limegeuzwa kuwa dampo la taka (jalala) kama mnavyoona hapo katika picha. Wamefanya kuwa dampo ambapo wanatupa taka hovyo/kiholela na wakusanyaji wa taka kutoka soko la zamani “MASANKULONI” (maarufu kwa sasa kama Kariakoo). Taka zinamwagwa bila mpangilio, na hali ya eneo hilo ni ya mbaya kimazingila na hatari kwa afya ya wakazi wa jirani.
Ni jambo la kushangaza kuona eneo la makazi ya watu likitumiwa kama dampo la taka ilhali serikali kupitia halmashauri ina uwezo wa kutenga maeneo rasmi kwa ajili ya utupaji taka. Harufu kali, uchafu uliozagaa, na hatari ya magonjwa ya mlipuko ni mambo yanayotishia usalama wa wananchi kwa sasa muda wowote. Wanasubili mpaka watu wapate madhara ndio watoke maofisini kuja kuweka matamko huku watu wamepata madhara kutokana na uchafu huu?.
Ninayo maswali ya msingi kwa mamlaka husika:

- Kwa nini dampo limeanzishwa kwenye nyumba ya serikali iliyoko kwenye makazi ya watu?
- Kwa nini taka hazikusanywi kwa mpangilio au kuziondoka kwa magari ya taka kandarasi iliyochukua tenda halmashauri iko wapi ili kuondoa hizi taka zilizozagaa kila pahala katika eneo hili?
- Serikali ina mpango gani wa haraka kuhamisha dampo hili na kulinusuru eneo hili kabla ya mvua kuanza?
HATUA ZA HARAKA ZINAHITAJIKA:
- Halmashauri ichukue hatua za haraka kuondoa taka zote na kusafisha eneo hili.
- Eneo hilo lirejeshwe kwenye matumizi yake ya awali (makazi au ofisi za umma).
- Uwekwa utaratibu wa kudumu wa usimamizi wa taka
Sisi wakazi wa eneo hili tunaendelea kuteseka, na hali hii inaweza kuwa mbaya zaidi kama hatua za haraka hazitachukuliwa.
Serikali itoke hadharani na kutoa majibu na mustakabali wa dampo hili, natarajia kusikia majibu na hatua kutoka kwa mamlaka husika ndani ya muda mfupi.
WATENDAJI HAWA WA SERIKALI HAPA USHIROMBO-BUKOMBE NDIO WANATAKIWA KUTOKA NA KUTOA SABABU NA MAJIBU ILI KUTATUA HALI HII.

- Afisa Mtendaji wa Kata ya Igulwa
- Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bukombe
- Afisa Mazingira au Afisa Afya wa Wilaya