Sikia mkuu, ikiwezekana wewe zinunue mbovu, zenye hitilafu, tengeneza, rekebisha, kisha uza tena(sambaza kwenye maduka ya vifaa vya umeme)
Unanunua yale mabovu kwa mafungu, mfano taa 10 kwa elfu 1, kila moja hapo umeinunua kwa 100, rekebisha weka buku lako la ufundi na 400 kama usafiri, we wasambazie wauzaji kwa 1500, ye akiuza elfu 2 sawa, na kama zinakuwa zinatoka we hata ukiwauzia kwa buku buku tu bado itakuwa vema kuliko kukaa kusubiri wateja walete taa zao mbovu.
Kwanza kuna watu wapo mbali sana, mfano we unaweza ukawa chanika mie tegeta, ngumu kukuletea taa zangu 2 uzitengeneze, sababu ya nauli, muda na kitu chenyewe kipya nakipata kwa bei chee,
Ila wewe ukikusanya mbovu utazipata za watu wa tegeta, mbezi, kigamboni, kisha we unarelebisha unasambaza wananunua,
Hapo unakuwa umemtengenezea wa tegeta kwa namna nyingine