Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Kanuni na maelekezo yanayosimamia uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 baadhi yana ukakasi mwingi na kama dhana ya uadilifu kwa baadi ya watu haitaheshimika itasababisha uchaguzi huu kuwa na malalamiko mengi na hasa siku ya kupiga kura, kuhesabu na kutoa matokeo, maeneo ambayo yanashida kwa jicho langu ni yafatayo.
1. Kama kutakuwa na uhaba wa fomu za matokeo, mawakala hawatapatiwa nakala hizo za matokeo(Ubunge, Udiwani, Urais), nachojiuliza kwanini fomu zisitoshe? Tume ihakikishe kunakuwa hakuna uhaba wa fomu za matokeo ili kila wakala apewe nakala yake,hii ya kusema "kama kutakuwa na uhaba, mawakala hawatapewa nakala ya matokeo, inaweza kusababisha malalamiko yasiyo na msingi.
2. Nakala ya fomu ya kiapo (fomu namba 6) kutotumika kwa ajili ya utambulisho wa mawakala, na pia wakala aliyeapa hatapewa nakala ya fomu hizo baada ya kuapa, hii si sawa kwa mtazamo wangu.
Kwa nini si sawa,unaweza kuta mgombea ameandaa mawakala wake, wanafika asubuhi kwenye kituo wanakuta watu wengine washaingia na wasimamizi wamewatambua halafu mawakala halali walioapa wanawekwa pembeni,hii inaweza kuleta malalamiko yasiyo na ulazima,ni vizuri tume ikatumia fomu namba sita kuwatambulisha mawakala na wawe ni wale waliotambulishwa na vyama vyao ama wagombea na siyo vinginevyo.
3. Waandishi wa habari kutotambulika kama kundi linaloruhusiwa kuingia kwenye chumba cha kupigia kura, hii inaacha maswali mengi, kwa nini waangalizi waruhusiwe kuingia wakati wote kuanzia zoezi la kupiga kura mpaka kuhesanu halafu waandishi wawekwe kando?
4. Mawakala hawataruhusiwa kuingia na simu wala kutumia kwenye vituo vya kupigia kura, kwanini mawakala wazuiliwe isipokuwa msimamizi wa kituo na mlinzi pekee, kwanini mawakala wanahofiwa kuingia na simu? Kama dhana ni uchaguzi unaozingatia dhana ya uwazi,binafsi sioni tatizo kwa wakala kuingia na simu.
5. Matokeo ya Urais kutopingwa mahakamani,je nchini Tanzania Kwa nini sheria iweke katazo hili?tunaamini haitakuja kutokea matokeo ya Urais yakawa na mazongwe ambayo yanahitaji HAKI ikasakwe mahakamani?
Hata kwenye hatua hii ya utezi kumekuwa na matatizo ya Kisheria na kikanuni, mfano
1. Sheria na kanuni zake zinaposema maamuzi ya tume ya kumkata mgombea ndiyo yatakuwa maamuzi ya mwisho na hayatapingwa kwenye mahakama yeyote, kwangu hili ni tatizo,yaani leo mimi haki yangu ikibinywa na tme naambiwa sina haki ya kwenda mahakama yeyote?ila nisubiri mpaka uchaguzi utakapoisha ndiyo nitakuwa na hiari ya kwenda kupinga ushindi mahakamani? Kwa niniuamizi wa tume uwe wa mwisho? Na kipindi hiki tumeshuhudia maamuzi mengi yenye utata kutoka tume.
2. Chama kutokupewa nafasi ya kubadili mgombea pale aliyepitishwa anapopatwa na shida, mfano kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi, mgombe anatakiwa yeye mwenyewe kuwasilisha fomu yake, vipi kama atapatwa na shida ya afya? Ama kukamatwa kama ilivyojitokeza jimbo la Mtama mkoani Lindi?