Uchaguzi 2020 Bulendu: Kanuni na Sheria za Uchaguzi zimetungwa kuwa Muathirika wa kanuni hana Haki ya kudai haki inayovunjwa. Tunatengeneza Magaidi wenyewe

Uchaguzi 2020 Bulendu: Kanuni na Sheria za Uchaguzi zimetungwa kuwa Muathirika wa kanuni hana Haki ya kudai haki inayovunjwa. Tunatengeneza Magaidi wenyewe

Tuna sheria za kijinga sana zilizotungwa na watu wajinga wenye dhamira ovu.

Sheria kama hizo, zinatakiwa kukataliwa, kutofuatwa na kupuuzwa na kila mwananchi. Hizo kanuni za kijinga namna hiyo, Tume wakazitumie kuendeshea familia zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyerere aliasisi ile sheria ya NEC ikishatangaza matokeo ya Urais hakuna nafasi ya kupinga mahakamani au kwenye chombo chochote kingine. Alifanya hivyo kwa nia ya kuhakikisha chama alichokiasisi haking'oki madarakani. Athari ya Sheria hiyo ilianza Zanzibar katika uchaguzi wa mwanzo wa vyama vingi pale ambapo "mpira ulishavuka msitari wa goli" lakini refa ( ZEC)) baada ya kimya cha siku kadhaa akaibuka na kusema SIO GOLI!!! Na huo ndio umekua utaratibu

Baada ya Mwalimu waliofuatia wamekua "wakiboresha" sheria na kanuni hizo kwa lengo la kuhakikisha uchaguzi unakua ni ile kamari maarufu ya "CHEUSI CHEKUNDU". Yaani cheza uchezavyo, fanya lolote lakini kamari ile HUWEZI KUSHINDA! Anayeshinda ni mchezeshaji tu na ukileta hoja zako unaweza kutobolewa macho maana wanakua ni genge la maharamia wa kuibia watu
Kumbe watu wanajua kabisa kinachofanyika! Sasa tunatokaje hapo? Maana kuna genge fulani la wahuni linatuchezea sana kila mara
 
Mtoa mada umeandika ukiwa umetulia!! Kuna maprofessor wa sheria wengi tu ,wengine ni wandamizi serikalini inaskitisha sheria za ovyo namna hii zmeangaliwa na maprofessor hawa kwa muda mrefu pasipokuangalia mstakabar wa Taifa letu.

Sheria mbofumbofu znazotudhalilisha kama Taifa Znaendelea kutumika katika maisha yetu zikitunyanyasa wenyewe na Wasomi wa sheria wapo!!Hivi nini mana ya usomi namna hii. Ninani yuko nyuma ya Sheri mbofumbofu hizi?

Na wasomi wa sheria na mabaraza yenu Mumeifanyia nini Nchi hii? Kwanini wanasiasa Wamehodhi ufahamu wenu kiasi hiki? Taifa lolote msingi wa ustaarabu huanzia kwenye mifumo imara ya utawala na mfumo mzuri wa upatkanaje wa mamlaka ya wananchi ndy msingi wa Taifa lolote makin.

Je, Wasomi wetu wa Sheria nani amechukua akili zenu?
Ndiyo maana mtu kama Kibudu, ni profesa wa hovyo kuliko jambazi la kuiba kuku. Ametumia elimu yake kuharibu Taifa badala ya kulijenga Taifa.

Sheria nyingi hizi za kiwendawazimu zimrkaziwa zaidi na mabadiliko mengi ambayo muasisi mkuu ni Kibudu na Jiwe. Yule mjinga wa mjengoni na wapiga vigelegele wake ni watu wa hewala mzee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kanuni na maelekezo yanayosimamia uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 baadhi yana ukakasi mwingi na kama dhana ya uadilifu kwa baadi ya watu haitaheshimika itasababisha uchaguzi huu kuwa na malalamiko mengi na hasa siku ya kupiga kura, kuhesabu na kutoa matokeo, maeneo ambayo yanashida kwa jicho langu ni yafatayo.

1. Kama kutakuwa na uhaba wa fomu za matokeo,mawakala hawatapatiwa nakala hizo za matokeo(Ubunge, Udiwani, Urais), nachojiuliza kwanini fomu zisitoshe? Tume ihakikishe kunakuwa hakuna uhaba wa fomu za matokeo ili kila wakala apewe nakala yake,hii ya kusema "kama kutakuwa na uhaba, mawakala hawatapewa nakala ya matokeo, inaweza kusababisha malalamiko yasiyo na msingi.

2. Nakala ya fomu ya kiapo (fomu namba 6) kutotumika kwa ajili ya utambulisho wa mawakala, na pia wakala aliyeapa hatapewa nakala ya fomu hizo baada ya kuapa,hii si sawa kwa mtazamo wangu.

Kwa nini si sawa,unaweza kuta mgombea ameandaa mawakala wake, wanafika asubuhi kwenye kituo wanakuta watu wengine washaingia na wasimamizi wamewatambua halafu mawakala halali walioapa wanawekwa pembeni,hii inaweza kuleta malalamiko yasiyo na ulazima,ni vizuri tume ikatumia fomu namba sita kuwatambulisha mawakala na wawe ni wale waliotambulishwa na vyama vyao ama wagombea na siyo vinginevyo.

3. Waandishi wa habari kutotambulika kama kundi linaloruhusiwa kuingia kwenye chumba cha kupigia kura, hii inaacha maswali mengi, kwa nini waangalizi waruhusiwe kuingia wakati wote kuanzia zoezi la kupiga kura mpaka kuhesanu halafu waandishi wawekwe kando?

4. Mawakala hawataruhusiwa kuingia na simu wala kutumia kwenye vituo vya kupigia kura, kwanini mawakala wazuiliwe isipokuwa msimamizi wa kituo na mlinzi pekee, kwanini mawakala wanahofiwa kuingia na simu? Kama dhana ni uchaguzi unaozingatia dhana ya uwazi,binafsi sioni tatizo kwa wakala kuingia na simu.

5. Matokeo ya Urais kutopingwa mahakamani,je nchini Tanzania Kwa nini sheria iweke katazo hili?tunaamini haitakuja kutokea matokeo ya Urais yakawa na mazongwe ambayo yanahitaji HAKI ikasakwe mahakamani?

Hata kwenye hatua hii ya utezi kumekuwa na matatizo ya Kisheria na kikanuni, mfano

1. Sheria na kanuni zake zinaposema maamuzi ya tume ya kumkata mgombea ndiyo yatakuwa maamuzi ya mwisho na hayatapingwa kwenye mahakama yeyote, kwangu hili ni tatizo,yaani leo mimi haki yangu ikibinywa na tme naambiwa sina haki ya kwenda mahakama yeyote?ila nisubiri mpaka uchaguzi utakapoisha ndiyo nitakuwa na hiari ya kwenda kupinga ushindi mahakamani?kwa niniuamizi wa tume uwe wa mwisho? Na kipindi hiki tumeshuhudia maamuzi mengi yenye utata kutoka tume.

2. Chama kutokupewa nafasi ya kubadili mgombea pale aliyepitishwa anapopatwa na shida, mfano kwa mujibu wa sheria na kanuni za uchaguzi, mgombe anatakiwa yeye mwenyewe kuwasilisha fomu yake, vipi kama atapatwa na shida ya afya? Ama kukamatwa kama ilivyojitokeza jimbo la Mtama mkoani Lindi?
Mawakala wanatakiwa kuwa na simu wao kama jicho/macho ya wapigakura na umma vinginevyo ni sawa na kupiga kura gizani.
Waandishi wa habari pia lazima wawepo ndani ya chumba cha kupigia kura. Wote hawa ni jicho/macho ya wapigakura na umma vinginevyo ni sawa na kupiga kura gizani.
Tume inapowakataa watu hao inataka kuendesha uchaguzi gizani. Haina nia ya kutenda haki.
Na ndiyo maana wanataka maamuzi tume kuhusu mshindi/washindi yafanywe gizani na yasihojiwe mahakamani.
 
Back
Top Bottom