Uchaguzi 2020 Bunda: Haijawahi kutokea Esther Bulaya avunja rekodi akusanya watu kwa maelfu,Wazee wa mji wasema niyeye tu Bunda Mjini Oct 25

Uchaguzi 2020 Bunda: Haijawahi kutokea Esther Bulaya avunja rekodi akusanya watu kwa maelfu,Wazee wa mji wasema niyeye tu Bunda Mjini Oct 25

Safi sana, kudo kwake! Na hili linatokea hapa hapa Tanzania? Sasa mwingine atasema "upinzani unazuiliwa kufanya mikutano ya nje"...
By Happiness Tesha, Mwananchi htesha@mwananchi.co.tz
Kigoma. Wakati mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe akizuiwa kufanya mkutano wa hadhara na Jeshi la Polisi mkoani Kigoma leo Ijumaa Januari 17, 2020, katibu mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ameanza ziara ya siku tatu mkoani humo.
Polisi mkoani Kigoma kupitia barua ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kigoma, M.R Mayunga yenye kumbukumbu namba KIG/A.24/60/VOL.1/114 ya Januari 16, 2020, wamemzuia Zitto kufanya mkutano wake leo kwa sababu za usalama na taarifa za kiintelijensia.
Akizungumza na Mwananchi leo katibu wa CCM mkoa wa Kigoma, Kajoro Vyohoroka amesema baada ya kuwasili mjini Kigoma, Dk Bashiru ataelekea eneo la Kazuramimba Wilaya ya Uvinza kwa ajili ya vikao vya ndani na viongozi wa chama na jumuiya zake.
“Jumamosi Januari 18, 2020 Katibu mkuu atapokea taarifa ya utekelezaji wa ilani na kazi zilizofanyika kwa kipindi cha miaka minne katika jimbo la Kigoma Kaskazini inayoongozwa na Peter Serukamba (CCM),” amesema Vyohoroka.
Kwa mujibu wa katibu huyo, Jumapili Januari 19, 2020, Dk Bashiru aliyetokea katika ziara mkoani Tanga na kuwapokea madiwani wanane wa CUF waliojiunga CCM, atakuwa na kikao cha ndani na mabalozi wa CCM na viongozi wa chama hicho tawala na jumuiya zake.
Akizungumzia kuzuiwa kwa mkutano wa Zitto, katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano na Umma wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu amesema sababu zilizotajwa na polisi hazina mashiko na zinalenga kumzuia Zitto asitekeleze majukumu yake halali ya kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo.
Pia Soma
 
Huyu binti ni jembe kweli kweli, ni mwanamke wa shoka, tena mimi najisikia very proud kum spot toka kitambo!, angalia tarehe ya bandiko hili

P
Pascal Mayala,wewe ni bonge la ndumilakuwili...si mtu wa kuaminika hata kidogo!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kwenye huo uzi uliounukuu kuhusu Bulaya, Pascal Mayalla ulijua kuiponda CCM bhana, duuh...we jamaa noma. Ila sasa hivi tangu uende Bungeni naona umebadiri upepo. Hongera, ulimtabiria vzr na imekuwa. Ila Nawe basi uwe na msimamo kama Alivyo shujaa Bulaya.
Huyu binti ni jembe kweli kweli, ni mwanamke wa shoka, tena mimi najisikia very proud kum spot toka kitambo!, angalia tarehe ya bandiko hili

P

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana, kudo kwake! Na hili linatokea hapa hapa Tanzania? Sasa mwingine atasema "upinzani unazuiliwa kufanya mikutano ya nje"...
Wewe nawe punguani la wapi wewe? Hujawahi kusikia watu wakizuiwa kufanya mikutano? Majitu mengine yakoje lakini?
 
Duh.. !, sii mchezo!.
Huyu binti toka longi ni mwanamke wa shoka

Ila pia usidanganywe na makundi ya watu.

P
Wewe Paskali na wewe wacha kuuma na kupuliza! Hebu mwambie huyu zumbukuku wako aruhusu uchaguzi huru uone vumbi lake! Kwa ufupi maccm hayapendwi na wananchi!
 
Wewe Paskali na wewe wacha kuuma na kupuliza! Hebu mwambie huyu zumbukuku wako aruhusu uchaguzi huru uone vumbi lake! Kwa ufupi maccm hayapendwi na wananchi!
Hawapendwi nao wanalifamu hilo.Ndiyo maana hawaishiwi viroja na hawapo tayari kwa Tume Huru ya uchaguzi.
 
Back
Top Bottom