Bundi atua msimbazi, wanachama waandamana kutaka uongozi uachie ngazi

Bundi atua msimbazi, wanachama waandamana kutaka uongozi uachie ngazi

mimi nilikuwa shabiki na mwanachama wa yanga lakini LUNYAMILA alipoacha kucheza mpira mimi nilihamia ulaya poleni simba nimesikia mnaitwa wa MATOPENI so sad
 
Mashabiki wa simba lazima waelewe kuwa mafanikio hayaji siku moja na kujenga timu ya ushindani si kazi rahisi, siyo mchezaji amekosea kidogo tuu nyie mnafukuza!
mjinga nini
 
Hahah! Mikia bana eti wakiharibu wamatopen wanasema mpira wa bongo kwan mpira wa bongo ndio simba ?
Mpira sio Simba wala timu gani; mpira wa tanzania ni ligi zote zinazochezwa chini ya usimamizi wa TFF. Kama migogoro haitatuliwi hatuwezi kupiga hatua.
 
nilikuwa najiuliza mbona simba walikuwa wanacheza vizuri sana nakupata ushindi mpaka kuongoza ligi lakini ghafla tu wamekuwa kimeo timu haina morali kabisa na wachezaji wanacheza kama wamelazimishwa tunachapwa mpaka na Toto daa kumbe hata mishahara hawajalipwa! Wachezaji ni wavumilivu sana lakini mpaka hizi habari zimetoka nje naamini hali ni mbaya sana. Hivi kuna haja gani ya mtu kujiita kiongozi halafu ikifika tarehe 25 ya mwezi unashindwa kwenda kukopa mahali (hata kwa riba kidogo) uwalipe wachezaji mishahara kwa wakati halafu pesa TBL zikija hata kama ni tarehe 10 mwezi mwingine unazirejesha. Haya hata kutoa pesa za Okwi na Samata uwalipe wachezaji mshahara halafu TBL wakileta uzirudishe nayo imeshindikana. Hivi hii nayo viongozi mfundishwe halafu tunategemea matokeo mazuri na maendeleo ya klabu; simba tutasubiri sana. Nafikiri simba sasa inahitaji viongozi aina ya kina Kaduguda kwani hata mimi nilikuwa na imani sana na friends of simba lakini leo nimeamini pesa sio kila kitu kinachohitajika ni ubunifu katika kuongeza mapato na uwekezaji, uwezo wa kuongoza na moyo wa kuwahudumia wachezaji na kuipenda simba yenyewe. Pesa zitakuja zenyewe baada ya timu kufanya vizuri kwani wapenzi watakuja uwanjani, wadhamini wataongezeka (kumbuka hamna mdhamini atakayekubali kudhamini timu inayofanya vibaya), jezi na vifaa mbali mbali vyenye nembo ya simba vitanunuliwa n.k. Ngoja niache kuendelea kuandika kwani kadiri ninavyoendelea kuandika napata maumivu zaidi hata ya Gentamycine!
 
Back
Top Bottom