Bundi katua Msimbazi

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
4,445
Reaction score
4,707
Hakika nimeshangazwa na Hamis Kigwangalla kuanzisha Mjadala wa Bil 20 za Mo kwenye Mitandao ya Jamii.

Bado ameendelea kusema katumwa na Baadhi ya Wajumbe wa Bodi Eti Ahoji. Najiuliza kwanini iwe sasa wakati suala hili lina Miaka 3 sasa.

Pili, kwanini asilipeleke Ofisi za Simba na pia Hao Wajumbe wa Bodi waliomtuma mbona wanaingia kwenye Vikao vya Simba na Mo akiwemo kwanini hawamhoji?

Huyu Kigwangalla ana Mchango gani kwa Klabu? Kwanini haulizii na Zile hisa 51 za Wanachama? Viongozi na Wanachama Wapinga Maendeleo na Mafanikio wameanza kazi; kuweni Makini na kina Kigwangalla.
 
Kumbukeni alikuwa na shida na pikipiki 25.Na anasema amezinunua kwa cash.Nina wasi wasi hizo zilikuwa pesa za GSM.
Nashangaa kiongozi analipwa pesa nyingi na serikali,dili nyingi alipiga kipindi cha jk,na bado fursa anazo,anakuwa na roho ya kichawi hivi,angekuwa maskini huyu mtu si angekuwa tatizo kubwa sana kwa jamii
 
Huyu kingwangala ndio walewale tu, mbona zile nyingi 51% haziulizi, aende akazinunue yeye
 
Amini Kigwagwala Kahoji kitu ambacho wengi walitamani kuhoji, Kigwa ni prominent figure na Minister ivo kitendo cha kuhoji tu kime draw attention ndio mana Mo amemjibu, Mo ni mjanja mjanja fulani
 
Mawaziri wa Magu wanatesa sana wafanyabiashara kwenye hizi kampeni zao, wanalazimisha wafanyabiashara wawakopeshe/wawachangie hela wakati watu wamepitia miaka5 migumu sana katika biashara zao. Na wakikataliwa wanaweka bifu.

Cha ajabu rais halioni hili, au kama analiona basi analifumbia macho.
 
Huyu Kigwa ajiangalie sana hata Uwaziri wenyewe anaweza asiupate, kama kapewa Pikipiki na GSM kwa ahadi ya kuwavuruga Wanasimba amekwamba pakubwaaaaa! Tunaaanza na Ihefu leo kukuonyesha umekwamaaaa!
All in all tunakutakia kampeni njema na Ushindi wa Ubunge lkn Uwaziri kwa Mzee wa Romboooo toka Jalalani Varcity.
 
zamani viongozi wa serikali hatukujua hata timu zao wanazoshabikia, leo kila waziri anabisgania timu yake
 
Kigwangala amejiacha uchi...Waziri wa Wizara nyeti kwenda kukopa kwa matajiri? So angeende Bank.Sasa kwa njaa hizo akiambiwa "hizo pikipiki nakupa bure nakuongeza na 75 nyingine na pesa kadhaa...ili nami niwinde Twiga kadhaa"atakataa Huyo kweli? Maana anaonyesha anauchungu na Mo siyo Simba...Hapo ndo nawaza Nyerere aliona mbali kwenye Azimio la Arusha kuhusu kuchanganya uongozi na biashara...so kwa tamaa hizo kwa kweli.
 
Amini Kigwagwala Kahoji kitu ambacho wengi walitamani kuhoji, Kigwa ni prominent figure na Minister ivo kitendo cha kuhoji tu kime draw attention ndio mana Mo amemjibu, Mo ni mjanja mjanja fulani
Kwanini aulize kwenye mitandao asiende Ofisini ?
 
Kigwa ni mnafki,katumwa na Utopolo kuchafua tumbo la Simba s.c.ili Simba ianze kuharisha.
 

Eeeh!! Kigwangala rudisha budi hifadhini kwani bundi maliasili ya taifa, na wewe ni waziri wa maliasili.
Achana na mambo ya chuki baada ya kunyimwa mkopo wa bodaboda. Nenda ukachukue hizo bodaboda kule Ngororngoro na TANAPA.
 
Kuna mambo muhimu ya kujiuliza
1. Je, alijua hayo alipoenda kuomba pikipiki za kampeni kwa MO ?
2. Je, angepewa pikipiki na misaada mingineyo angeongea hayo ?
3. Je, huu ndio mtindo wake wa uongozi ?
4. Je, anayetakiwa kununua au kulipia hisa ni MO peke yake ?
5. Na, kwanini wakati huu muhimu wa kampeni ?
 
Kuna mambo muhimu ya kujiuliza
1. Je, alijua hayo alipoenda kuomba pikipiki za kampeni kwa MO ?
2. Je, angepewa pikipiki na misaada mingineyo angeongea hayo ?
3. Je, huu ndio mtindo wake wa uongozi ?
4. Je, anayetakiwa kununua au kulipia hisa ni MO peke yake ?
5. Na, kwanini mtu mwenye dhamana ya uwaziri kufanya haya wakati huu muhimu wa kampeni ?
 
Ndiyo mfumo wa utawala wa ccm wa kupora wafanya biashara.

Hata wakuu wa mikoa hufanya hivyo hivyo ndiyo maana wafanya biashara wengi wanajifanya kuwa wanaccm ili kulinda biashara zao.
 
Kufanya biashara hapa nchini shida sana.
Kila siku Rostam Azizi anaitwa mikutanoni na ktk nyuma za ibadai ili atoa michango tena kwa lazima.

Matajiri wanaporwa sana pesa zao, ndio maana wameamua wote kujitoa katika shughuri za kisiasa.

Leo tumemsikia Kigwa tu lakini hatujui ni viongozi wangapi wa vyama wanapishana kwenye ofisi za Matajiri kwa nia ya kuwakopa au kuwachangisha kwa lazima.

Kama mkopo ni kitu Cha kawaida mbona huyo HK anapandwa na jazba baada ya Kuambiwa ukweli wake.
Na alikataliwa kwakuwa Wanasiasa wakikopa hawataki kulipa, wana madeni hadi kisogoni.
Kama angeonekana mlipaji asingenyimwa hizo Toyo.

Ni aibu tupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…