Bunduki ni zaidi ya Corona Marekani

Bunduki ni zaidi ya Corona Marekani

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
7,672
Reaction score
9,039
Wanangu wana jamvi. Wamarekani ni watu wa ajabu sana. Wanasema kwenye nembo ya taifa lao IN GOD WE TRUST.

Ila kiukweli inapaswa iwe IN GUN WE TRUST. Wanapenda sana bunduki kiasi cha kumalizana wenyewe kwa wenyewe. Wanachukia ugaidi wa nje lakini wanafanyiana ugaidi wa ndani kwa kutumia bunduki. Hapa hujaongeza ubaguzi wa rangi. Marekani inahitaji msaada kuondokana na ugaidi wa bunduki na utegemezi wake ukiachia mbali mapenzi ya mitutu.

Kwa sasa, tishio la bunduki ni kubwa kuliko hata corona. Rais Biden ameliita hili janga au pandemic kwa taifa.

Afrika inapaswa itoe msaada kwa Marekani.
 
Mmesha sahau ule ugaidi wenu wa wasiojulikana mpaka kufikia hatua ya kutaka kutoa uhai wa Lissu?
 
Mmesha sahau ule ugaidi wenu wa wasiojulikana mpaka kufikia hatua ya kutaka kutoa uhai wa lissu?
Kwa nini huwa mnapenda kuharibu nyuzi za watu bhana?

Unatabu gani kuanzisha yakwako?

Na hata hivyo, ni watu wangapi duniani ambao wamepigwa/walipigwa risasi na makosa hawana!

Duniani, ni sehemu pa hatari, kila akifanyacho mtu, iwe kuoga, Kula, kuongea, kusafiri, n.k hivi Vyote siku ya siku hugeuka kuwa sehemu ya mtu huyo kupatwa na umauti utokanao na kazi zake mwenyewe.

Usiogope kufa, Kwani hakuna awezaye kuepuka kifo, timiza ulichokusudia
 
Mmesha sahau ule ugaidi wenu wa wasiojulikana mpaka kufikia hatua ya kutaka kutoa uhai wa Lissu?
Matukio kama Lissu yangekuwa mengi basi sasa ingekuwa yanatajwa matukio ya wengine ila naona hakuna hayo matukio na ndio maana hadi sasa Lissu ndio kabaki mfano asiye na mwenzie.
 
Wanangu wana jamvi. Wamarekani ni watu wa ajabu sana. Wanasema kwenye nembo ya taifa lao IN GOD WE TRUST.

Ila kiukweli inapaswa iwe IN GUN WE TRUST. Wanapenda sana bunduki kiasi cha kumalizana wenyewe kwa wenyewe. Wanachukia ugaidi wa nje lakini wanafanyiana ugaidi wa ndani kwa kutumia bunduki. Hapa hujaongeza ubaguzi wa rangi. Marekani inahitaji msaada kuondokana na ugaidi wa bunduki na utegemezi wake ukiachia mbali mapenzi ya mitutu.

Kwa sasa, tishio la bunduki ni kubwa kuliko hata corona. Rais Biden ameliita hili janga au pandemic kwa taifa.

Afrika inapaswa itoe msaada kwa Marekani.
Suala la bunduki Marekani ni biashara za watu.

Democrats wameshapambana sana kutunga sera ya "Gun Control" bila mafanikio.

Republican wanaamini Bunduki haziui watu, ila watu ndio wanaua watu. Hivyo hakuna sababu ya kudhibiti bunduki.
 
KATIBA BORA KABISA

Wamarekani wanatamba kumiliki bunduki kutokana na katiba yao kipengele cha kumi na tatu.

Hicho kipengele kinahusu haki ya raia kumiliki silaha kwa ajili ya kujilinda kutokana na maadui wa ndani na wa nje. Hawa maadui wanafafanuliwa kama ifuatavyo

Adui wa ndani
Hawa ni maadui kama majambazi, madictekta/tyrant. Haiingii akilini serikali kuweka udhibiti kwenye umiliki wa silaha hivyo kufanya raia wake kushindwa kujitetea pale wanapokutana na jambaxi au pale serikali inapokuwa rogue na kuanza kunyanyasa raia. Raia wakichoka mda wowote wanaliamsha

Adui wa nje
Hapa in case marekani imevamiwa na wanajeshi wa taifa lingine. Kuna watu huwa wanaponda Marekani kuwa haitaki vita ipiganiwe kwake anakuletea vita kwako sasa endapo nchi adui wa akajichanganya kupeleka wanajesh atashangaa kuona idadi kubwa sana ya raia wakiwa n silaa za kivita
 
Siku Serikali ikiamua kuingiza majeshi mtaani kupiga raia,ndio hapo umuhimu wa 2nd amendment utaonekana,rais watatoka na AR-15 kama zote kuja mtaani kupambana na jeshi.
 
Katiba yao inasema hivi..

The Second Amendment, one of the ten amendments to the Constitution comprising the Bill of Rights, states: “A well regulated Militia, being necessary to the security of a free State, the right of the people to keep and bear Arms, shall not be infringed.
 
Ni heri ukose pesa Ila si hekima.. marekani wanahitaji msaada wa hekima.
 
Matukio kama Lissu yangekuwa mengi basi sasa ingekuwa yanatajwa matukio ya wengine ila naona hakuna hayo matukio na ndio maana hadi sasa Lissu ndio kabaki mfano asiye na mwenzie.
Na wale wanaotupwa kwenye viroba kwaajili ya siasa, wanaotekwa jee na kuteswa, wanaofungwa kwenye magereza miaka zaidi ya 7 bila ya kesi
 
KATIBA BORA KABISA

Wamarekani wanatamba kumiliki bunduki kutokana na katiba yao kipengele cha kumi na tatu.

Hicho kipengele kinahusu haki ya raia kumiliki silaha kwa ajili ya kujilinda kutokana na maadui wa ndani na wa nje. Hawa maadui wanafafanuliwa kama ifuatavyo

Adui wa ndani
Hawa ni maadui kama majambazi, madictekta/tyrant. Haiingii akilini serikali kuweka udhibiti kwenye umiliki wa silaha hivyo kufanya raia wake kushindwa kujitetea pale wanapokutana na jambaxi au pale serikali inapokuwa rogue na kuanza kunyanyasa raia. Raia wakichoka mda wowote wanaliamsha

Adui wa nje
Hapa in case marekani imevamiwa na wanajeshi wa taifa lingine. Kuna watu huwa wanaponda Marekani kuwa haitaki vita ipiganiwe kwake anakuletea vita kwako sasa endapo nchi adui wa akajichanganya kupeleka wanajesh atashangaa kuona idadi kubwa sana ya raia wakiwa n silaa za kivita
Na mwisho wake wanauwana waokwawao kama kuku saivi badala ya adui wa nje
 
Back
Top Bottom