Bunge: CCM pekee ndiyo imewasilisha jina la Mgombea wa nafasi ya Naibu Spika

Bunge: CCM pekee ndiyo imewasilisha jina la Mgombea wa nafasi ya Naibu Spika

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Bunge limesema zoezi la uteuzi limekamilika, na hadi kufikia muda huo Chama kimoja (CCM) ndicho kimewasilisha jina la Mgombea nafasi ya Naibu Spika iliyo wazi baada ya Dkt. Tulia Ackson kujiuzulu na kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge.

Jina la Mgombea litawasilishwa mbele wa Wapiga Kura kesho Februari 11, 2022 kwa ajili ya Uchaguzi.

1644501471030.png
 
Hata wangewasilisha wengine bado huyo huyo wakwao ndo angekua spika. Wanafuata tu utaratibu kama ilivyo kwa matangazo ya ajira.

Tangazo linatoka kuonesha kuwa utaratibu umezingatiwa. Ila wakati mnahangaika kuomba ajira husika, kuchoma nauli mpaka UDOM na kuteseka na interview majina tayari yanakuepo na wahusika wameshaambiwa wafungue hadi account za kuwekewa mishahara na tayari wametonywa watapangwa wapi.

HATUJAISAHAU TANZANIA YETU (Tuko kwenye zama za "Who you know" na si What you know")
 
Bunge limesema zoezi la uteuzi limekamilika, na hadi kufikia muda huo Chama kimoja (CCM) ndicho kimewasilisha jina la Mgombea nafasi ya Naibu Spika iliyo wazi baada ya Dkt. Tulia Ackson kujiuzulu na kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge.....
Hapa kuna uchaguzi au upotevu wa pesa za walipa kodi?

Sijawahi ona uchaguzi wa kitu kimoja, yani upewe embe halafu uambiwe chagua.

Nonsense kabisaaaaaaaaa
 
Si rahisi mtu kutoka chama kingine kushinda unaibu spika ama uspika kwenye bunge la chama kimoja. Naona sasa wapinzani akili zimewarudia. Hata walioshiriki kugombea uspika niliwashangaa!
 
Bunge limesema zoezi la uteuzi limekamilika, na hadi kufikia muda huo Chama kimoja (CCM) ndicho kimewasilisha jina la Mgombea nafasi ya Naibu Spika iliyo wazi baada ya Dkt. Tulia Ackson kujiuzulu na kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge

Jina la Mgombea litawasilishwa mbele wa Wapiga Kura kesho Februari 11, 2022 kwa ajili ya Uchaguzi

View attachment 2114972
NAIBU SPIKA wa HALMASHAURI KUU ya Chama

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Ni baada ya muda wa kuwasilisha jina la mgombea unaibu Spika wa Bunge la JMT kuisha leo Alhamis saa 10 jioni bila kutokea mgombea toka chama kingine zaidi ya wa CCM, Mussa Zungu!

Nawaza;
Hivi CCM hawajiskii vibaya kukosa tofauti kati ya Bunge na Halmashauri Kuu ya Chama chao? Tazama maneno kwenye picha hii!
Screenshot_20220210-232839~2.png
 
Sasa uliposema LEO Ijumaa saa10 ulimaanisha nini? Maana leo ijumaa haijafika au Alhamis.
 
Ni baada ya muda wa kuwasilisha jina la mgombea unaibu Spika wa Bunge la JMT kuisha leo Alhamis saa 10 jioni bila kutokea mgombea toka chama kingine zaidi ya wa CCM, Mussa Zungu!

Nawaza;
Hivi CCM hawajiskii vibaya kukosa tofauti kati ya Bunge na Halmashauri Kuu ya Chama chao? Tazama maneno kwenye picha hii!View attachment 2115329
Mr Tozo
 
Bunge limesema zoezi la uteuzi limekamilika, na hadi kufikia muda huo Chama kimoja (CCM) ndicho kimewasilisha jina la Mgombea nafasi ya Naibu Spika iliyo wazi baada ya Dkt. Tulia Ackson kujiuzulu na kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge

Jina la Mgombea litawasilishwa mbele wa Wapiga Kura kesho Februari 11, 2022 kwa ajili ya Uchaguzi

View attachment 2114972
Ni wanasiasa pekee wasioonea aibu tabia zao
 
Bunge limesema zoezi la uteuzi limekamilika, na hadi kufikia muda huo Chama kimoja (CCM) ndicho kimewasilisha jina la Mgombea nafasi ya Naibu Spika iliyo wazi baada ya Dkt. Tulia Ackson kujiuzulu na kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge

Jina la Mgombea litawasilishwa mbele wa Wapiga Kura kesho Februari 11, 2022 kwa ajili ya Uchaguzi

View attachment 2114972
Huu ndio ukomavu wa democrasia, vyama vingine vyote vimeamua kutumia busara kutoteua wagombea kushiriki igizo jingine la uchaguzi wa Naibu Spika, kama walivyoshiriki igizo la uchaguzi wa Spika.
P
 
Huu ndio ukomavu wa democrasia, vyama vingine vyote vimeamua kutumia busara kutoteua wagombea kushiriki igizo jingine la uchaguzi wa Naibu Spika, kama walivyoshiriki igizo la uchaguzi wa Spika.
P
Leo unawaita waigizaji kesho unaomba wakuteuwe kisha unaishia kupata kura moja wewe ni vuguvugu hata Mungu hapendi watu wa aina yenu ukiamua kula magi kula broo
 
Zito amefanyaje sasa? Apeleke jina la mgombea ili kuhalalisha uchaguzi wa naibu spika kuwa umezingatia demokrasia ya vyama vingi bungeni.
 
Back
Top Bottom