Bunge: CCM pekee ndiyo imewasilisha jina la Mgombea wa nafasi ya Naibu Spika

Bunge: CCM pekee ndiyo imewasilisha jina la Mgombea wa nafasi ya Naibu Spika

Bunge limesema zoezi la uteuzi limekamilika, na hadi kufikia muda huo Chama kimoja (CCM) ndicho kimewasilisha jina la Mgombea nafasi ya Naibu Spika iliyo wazi baada ya Dkt. Tulia Ackson kujiuzulu na kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge

Jina la Mgombea litawasilishwa mbele wa Wapiga Kura kesho Februari 11, 2022 kwa ajili ya Uchaguzi

View attachment 2114972
Kuna bunge hapo sasa?
 
Ni baada ya muda wa kuwasilisha jina la mgombea unaibu Spika wa Bunge la JMT kuisha leo Alhamis saa 10 jioni bila kutokea mgombea toka chama kingine zaidi ya wa CCM, Mussa Zungu!

Nawaza;
Hivi CCM hawajiskii vibaya kukosa tofauti kati ya Bunge na Halmashauri Kuu ya Chama chao? Tazama maneno kwenye picha hii!View attachment 2115329
Hawajisiki vibaya, madaraka yana tabia ya kulevya
 
-Vile vyama vya upinzani vilivyojitokeza katika uchaguzi wa speaker mbona hawakujitokeza tena?
Swali mujarabu!
Wale walio jitokeza kule ni vile vyama oandikizi, wasindijizaji wa Ccm.
Kule bungeni walioko ni bunge la Ccm wenyewe. Hivyo wameshindwa kuweka maoandikizi kwa vile naibu spika lazima awe mbunge.
 
Back
Top Bottom