Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

Wanaiba hadi wanasahau kuna maximum ya kufaulu, unadanganya hadi unajipa marks 130% unasahau marks za juu ni 100% hahahaha.
 

Wakishapinga wawape case za kuhujumu uchumi [emoji2359][emoji2297] ukiteleza mdomo unapewa case ya kumtukana rais [emoji23][emoji23]
 
Magufuli kawaweza CCM kawaindolea wote especially wabunge Ujasiri mbele yake hata wale waliokuwa wanakubalika

LENGO LA MAGUFULI KUHAKIKISHA WABUNGE WOTE WANAPITA NA KURA ZA WIZI LIMEWAFANYA HATA WALE WALIOKUWA NA UHAKIKA WA KUSHINDA KUKOSA UHALALI MBELE YA WANANCHI NA KUONEKANA WAMESHINDA KWA FADHILA YA RAIS


KAULI KAMA HIIZI NI KIELEEZO

“ ... sisi wote tuko hapa ; tumshukuru
muheshimiwa Rais ... bila yeye hatungekuwa hapa ...”
job ndugai
bungeni Hotuba ya rais

“ Bila mimi wewe Lukuvi na wengine hamngekuwa hapa ....”

“ mligombea Ubunge na sio Urais ..."

"mara hii nina wabunge wote..."

"waziri mkuuu hakuna uhakika kama utakaaa miaka mitano '..."

na kauli nyingine nyingi tu za dharau anapata ngvu kutoa kipindi hiki kwakua kawafanya wote waone bila yeye hawangepata ubunge

Kauli kama kuhakikishia baadhi kuwa hawawezi kuwa marais inaweEkana tu kwenye nchi ambayo ana uhakika hakuna demikraisia ya ndani na nje ya chama

Unaweza mfano kumkebehi kabudi au lukuvi hatakuwa rais lakini wanachama wakamtaka au akagombea na chama kingine wananchi wakampa

Kimsingi hatuna bunge ; bunge ambalo hadi wanakosea na kusema "muheshimiwa Mungu ..." ina maana akili na moyo ziko huko .
 
Kutokuwepo kwa wapinzani kumesaidia bei ya cement kupaa mara dufu...... Maendeleo hayana chama...... Tumeipende wenyewe, chaguo lenu wenyewe ahhh..... Acha tuisome namba......
 
Kaka yangu Pascal Mayalla , kati ya watu WANAFIKI niliowahi kuwaona, na wewe ni mmoja wao.

Ukijua sababu ya wewe kuonekana mnafiki, basi utajua kwanini Mh. Raisi hawezi kuteua upinzani kuingia bungeni.
 
Huyu si Pascal yule Wa zamani....hoja ni nzuri tatizo umepapambana sana kubalance ujumbe... Ni vigumu sana kujenga hoja nzuri wakati moyo umezungukwa na hofu ndani yake..... '' Wewe umekili kabisa Bunge hili litaharakisha maendeleo, hapo hapo unasema lina hali mbaya...Kwani faida ya Bunge ni nini ??? ....Mayala Bwana yaani point yako kubwa kutaka kambi ya upinzani bungeni... ni kuona msisimko tu..... Kwahiyo wapinzani kazi yao bungeni ni kuleta msisimko tu na si maendeleo (kwa mtazamo wako).. ''WATANZANIA WANATAKA MAENDELEO NA SI MSISIMKO" VIKO VITU VINGI VINAWEZA KUTUPA MSISIMKO.....
 
'Kushindwa' kivipi mkuu? haki ilikuwepo?
Uchaguzi umeishaje mkuu? haki ilitamalaki?
 
Kuliwahi kuwepo makada zaidi yako akina Evarist Chahali na Mange Kimambi sijui wapo wapi siku hizi?Wewe ulipouliza lile swali siku ile ukaamhiwa mayala ni njaa sasa unajaribu kuufyata mkia!Wenzako wametangaza kunyooshwa,peleka jina uteuliwe kama umeshanyooshwa.
 
Kwani wakati wanafanya ujinga wao hawakuliona jambo hilo kwamba kambi rasmi ya upinzani bungeni itakosekana,jiwe na watu wake hawajafanya ujangili kwa bahati mbaya bali kulikuwa na some sort of premeditation
 
Mkuu nimekuelewa vizuri sana natumaini ingetulia vizuri ungeandika kitu kizuri Sana na huyu Mayala angenonyeza like kitufe cha thanks
 
One of my best comment big up bro

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kuna viti vya upendeleo kutokana na wingi wa kura za wapinzani sasa ni wao wenyewe wenye kuamua kusuka ama kunyoa,pia mkuu wa nchi ana nafasi 10 anaweza kuwapa hata 5 za buure,hata Mbatia ambaye tulimsahau alikuwa mbunge baada ya JK kumteua
 
Mkuu fundimchundo , nimeguswa na bandiko lako hili, mimi ni realist, ma realists wote, hata kama hau support kilichofanyika, lakini when kumetokea kitu kilichotokea, and there is nothing anyone can do to change the situation, ma realists wote tunakubali matokeo, katika muktadha wa appreciating the situation and suggest the best way forward out of the situation.

Vyama vya siasa sio mali ya watu, viongozi, ni mali ya umma, hivyo maamuzi yoyote yatafanywa kwa kutanguliza maslahi ya umma.
Kwenye hili, maslahi ya umma ni kwa wapinzani hao wachache waliopata fursa ya kuingia Bungeni, waingie waka salvage what is left of opposition in Tanzania.

P
 
Mkuu Drifter, kwanza asante kwa mchango wako, very objective, kiukweli tangu nimepandisha uzi huu, wewe ndio mtu wa kwanza kunielewa, kwasababu, kiukweli kabisa, hii jf ya sasa, tuna watu wachache sana, wenye kuweza kusoma bandiko na kisha kujiuliza what is the motive behind.

Chama cha Mapinduzi ni chama cha ukweli na haki, kiliasisiwa na Mwalimu Nyerere, mpenda haki na mtenda haki. Baada ya Mwalimu, CCM ilipitia mageuzi na kuishiwa kuhodhiwa na wenye fedha, hivyo kuzalisha kada kubwa ya makada wa CCM ambao ni makada maslahi, na kwenye uchaguzi, wanakuwa wako tayari kutumia mbinu zozote kushinda uchaguzi. JPM alipoingia, amekuja kuibadili CCM kuirudisha ile CCM ya Nyerere. Sasa ndani ya makada wa CCM, kuna makada wa aina mbili, kuna "CCM Die Hard", hawa ndio wanaotaka kuhakikisha CCM inaupondaponda upinzani na kushinda kwa asilimia 99.9% kwa kutumia mbinu zozote.

Tupo sisi makada "Modern CCM" ambao kutokana na good track ya kazi nzuri ya JPM, CCM innashinda kwa mshindi mzuri safi na clear victory, kushinda kwa haki bila kufanya figisu figisu zozote.

Kwa vile Bunge letu ni Bunge la vyama vingi, mimi naamini kuna baadhi ya wana CCM very genuine, hakupenda kuona baadhi ya wapinzani wakishindwa akiwemo mtu kama Zitto!. Lakini kutokana na wapinzani kukataliwa na wananchi, ili Bunge lichangamke, zile kamati 2 za oversight committee, PAC na LAAC, lazima ziongozwe na wabunge wa upinzania ambao ni vichwa vya ukweli, kwenye hao wabunge wote sijaona watu wa kalibre hiyo ndio maana kila siku, tunamuomba Mwenyekiti wetu, JPM, katika zile nafasi zake 10, awateua wapinzani 4, Zitto, JJ Mnyika, Mbatia na kale kabinti Queen Sendiga.

Ili CCM itawale vizuri inahitaji Upinzani makini, ndio maana kila uchao, naibalasa Chadema humu na ACT Zanzibar, waache ujinga wa kususa. Ili kusasa kwa akili ni kususa kama kwa kususa huko utaachieve something, lakini kususa tuu for the sake of kususa, huku you won't achieve anything huu ni ujinga!.

Karibu tena.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…