Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?

Swali kwako Pasco utawaleta vipi bungeni wapinga maendeleo?

Pili ukiweka gunzi katikati ya betri tochi itawaka?

Mimi nadhani ni vizuri miaka hii mitano aachiwe Magufuli peke yake na wabunge wake bila gunzi ili tuone maajabu ya maendeleo na tuone kweli wapinzani walikuwa ni kikwazo cha maendeleo.

Natalajia kuiona Mtera kama Oslo Norway
 
AS a Tanzanian foremost : hata bunge lililo pita sikuweza kuona policy alternative zikiwekwa na sisi Wapinzani hata katika maeneo japo ya wizara kivuli nne tuu, acha kusema katika kila wizara kivuli.

This time tuongeze nguvu ya kuimarisha upinzani katika utendaji kazi wake ili waweze kutoa michango yenye uzito kwenye public policy alternative.
 
Makovu kutoka kwa nani? Nani aliwatia vidonda? Pili upinzani walicheleweshaje maendeleo? Ili bungen hoja ipite huamliwa na kura sasa upinzani walichelewesha vipi? Je mbona hayo maendeleo hayakuonekana 1992- ambapo ni ccm watupu
 
Eti NEC iteuwe..Hivi kuna ibara ipi inayoipa mamlaka NEC kuteua yenyewe wabunge?
 
Maadam Mama kaonyesha nia Njema na dhamira Njema, kwenye kulitibu taifa hili, Mnaonaje tukimshauri:, kama ikimpendeza, afanye na hili, na kwa vile saa hizi nafasi zimeisha jazwa anaweza to create at least 2, Mbowe na Zitto, wakaingia!.
Hili mnalionaje?.
P
 
Waendelee kupindisha Sheria na Katiba?

Haya basi "Akipendezwa"

Wataua Upinzani.
 
Maadam Mama kaonyesha dhamira Njema, ikimpendeza, afanye na hili, na kwa vile saa hizi nafasi zimeisha jazwa anaweza to create at least 2, Mbowe na Zitto, wakaingia!.
Hili mnalionaje?.
P
Awatoe kwanza wale 19 wasio na chama, na wasitetewe wana kesi ipo mahakamani, ile kesi ni ya uongo, ilitengenezwa makusudi ili kuchelewesha suala lao lakini kimsingi hawana haki yoyote, kwani wao hawana tofauti yoyote na wasaliti waliowatangulia wakashughulikiwa kwa taratibu zile zile na chama chao.
 
Hawezi kuingilia muhimili mwingine kule bungeni Samia hahusiki totally hata hivyo kesi ipo mahakamani japo mahakama yenyewe niyaccm lakini ngoja tuone
 
Just imagine vichwa hivi vingekuwa Bungeni leo kungetokea nini kwenye kupitishwa kwa mkataba huu?.

Kati ya mboga ambazo mboga kidogo, unakula ugali mkubwa, ni mboga ya mpenda!. Bunge linapokuwa mlenda, mambo ndio kama hivyo!.
P
 
Sikujua kama kulikuwa kuna vikao vya bunge vikiendelea..

Nimeshangaa sana kumbe kuna bunge, tena kubwa kabisa kuelekea bajeti.

Inashangaza sana.

Hata zile clips kutoka bungeni siku hizi hazipo tena.
Karibu, Bunge jipya lina hali mbaya! Serikali itafanaje kuliokoa Bunge ili kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni?
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…