Bunge kumthibitisha Ndejembi leo Agosti 28, 2026 kuwa Makamu wa Rais

Bunge kumthibitisha Ndejembi leo Agosti 28, 2026 kuwa Makamu wa Rais

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Bunge la Tanzania leo Ijumaa, Agosti 28, 2026 litapokea na kumthibitisha uteuzi wa Deogratius Ndejembi kuwa Makamu wa Rais.

Kwa mujibu wa orodha za shughuli za Bunge leo, pamoja na mambo mengine, wabunge watapata fursa hiyo kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania.

Jumatano ya Agosti 27, 2026, Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ilimpendekeza Ndejembi ambaye ni Waziri wa Nishati kuwa Makamu wa Rais.

Ndejembi ambaye pia ni Mbunge wa Chamwino, Mkoa wa Dodoma anakwenda kuchukua nafasi ya Dk Emmanuel Nchimbi ambaye ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo.

Baada ya Bunge kudhibitisha, itabaki kuapishwa na kuanza majukumu mapya ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan.

 
Kwahyo hapo watasema yes wote 🤣🤣🤣 aiseee, hakuna mwenye uwezo wa kumdindia malkia hapo ***** atapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Back
Top Bottom