Waufukweni JF-Expert Member Joined May 16, 2024 Posts 5,383 Reaction score 18,776 Aug 28, 2026 #1 Bunge la Tanzania leo Ijumaa, Agosti 28, 2026 litapokea na kumthibitisha uteuzi wa Deogratius Ndejembi kuwa Makamu wa Rais. Kwa mujibu wa orodha za shughuli za Bunge leo, pamoja na mambo mengine, wabunge watapata fursa hiyo kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania. Jumatano ya Agosti 27, 2026, Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ilimpendekeza Ndejembi ambaye ni Waziri wa Nishati kuwa Makamu wa Rais. Ndejembi ambaye pia ni Mbunge wa Chamwino, Mkoa wa Dodoma anakwenda kuchukua nafasi ya Dk Emmanuel Nchimbi ambaye ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo. Baada ya Bunge kudhibitisha, itabaki kuapishwa na kuanza majukumu mapya ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan. View: https://www.youtube.com/watch?v=zmadQdGgSk4
Bunge la Tanzania leo Ijumaa, Agosti 28, 2026 litapokea na kumthibitisha uteuzi wa Deogratius Ndejembi kuwa Makamu wa Rais. Kwa mujibu wa orodha za shughuli za Bunge leo, pamoja na mambo mengine, wabunge watapata fursa hiyo kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania. Jumatano ya Agosti 27, 2026, Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ilimpendekeza Ndejembi ambaye ni Waziri wa Nishati kuwa Makamu wa Rais. Ndejembi ambaye pia ni Mbunge wa Chamwino, Mkoa wa Dodoma anakwenda kuchukua nafasi ya Dk Emmanuel Nchimbi ambaye ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo. Baada ya Bunge kudhibitisha, itabaki kuapishwa na kuanza majukumu mapya ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan. View: https://www.youtube.com/watch?v=zmadQdGgSk4
Mangala boi Member Joined Oct 18, 2025 Posts 89 Reaction score 303 Aug 28, 2026 #2 Sangapi itakuwa mkuu
AI BRAINFULL JF-Expert Member Joined Oct 31, 2019 Posts 2,122 Reaction score 5,319 Aug 28, 2026 #3 Kwaiyo bunge wao ni kuipitisha na kusibitisha tu wala sio YES OR NO?
Sozo_ JF-Expert Member Joined Jun 12, 2022 Posts 3,248 Reaction score 6,146 Aug 28, 2026 #4 Asante kwa taarifa
baz kaiza JF-Expert Member Joined Jan 27, 2015 Posts 14,971 Reaction score 18,641 Aug 28, 2026 #5 Tanzania hakuna Bunge
Kingsharon92 JF-Expert Member Joined Aug 10, 2015 Posts 8,560 Reaction score 12,277 Aug 28, 2026 #6 baz kaiza said: Tanzania hakuna Bunge Click to expand... Kuna genge la MAJANGIRI
comrade_kipepe JF-Expert Member Joined Jun 25, 2019 Posts 8,748 Reaction score 18,096 Aug 28, 2026 #7 Kwahyo hapo watasema yes wote 🤣🤣🤣 aiseee, hakuna mwenye uwezo wa kumdindia malkia hapo ***** atapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
Kwahyo hapo watasema yes wote 🤣🤣🤣 aiseee, hakuna mwenye uwezo wa kumdindia malkia hapo ***** atapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa.
A akili mwili mzima JF-Expert Member Joined Nov 13, 2025 Posts 2,662 Reaction score 5,558 Aug 28, 2026 #8 Kwa bunge hilo, hata ingekuwa ni Kingwendu angethibitishwa tu kuwa VC!.