Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,459
- 100,799
Huu utumbo wa bata hata hauleweki
Ndio michango ya wote wawili sijaisikia kabisa pamoja na kukaa kwenye tv kwa muda mrefu mitambo ilivyorudi,muda wao ukawa umeisha.Kama hii ni kweli hii nchi inawenye nao. Wengine tunasindikiza tu
Ngoja tusubirie huenda wakawa na sauti zao wakati wanahutubia.Zama za ccm zitapita
Tatizo wanapenda kusifiwa tu hawataki maoni mbadala.Hii hamu ya kusikiliza upande wa pili itawatesa sana ccm,mda utaongea
Kwa nini mitambo ikatwe kwenye zamu yao tu.Wale kuchangia Bungeni hadi stimu kwanza siyo hivihivi tu.
Inakera sana, wametunnyima haki ya kusikiliza maoni ya upande wa pili...Najua yasingeweza kubadilisha chochote lakini tungejua mtazamo wao kuhusiana na haya maazimio.Kama hii ni kweli, inasikitisha sana, hata sie waunga mkono Juhudi za JPM, tunasema hiyo sio haki, na ujinga unaofanywa na viongozi wa chama chetu.
Msitufanye hatuwezi washinda hawa wana UFIPA bila kutumia mabavu ya serekali. Mumeuharibu ushindani, tunawamiss Kikwete na akina Kinana, Makamba, Nape na wale viongozi waliokuwa wakitumia vichwa vyao.
Waoga sana yaani.!Daaa
Wakakata mitambo
Jamanii
Kiongozi lazima uwe na ngozi ngumu, ukiwa mwoga mwoga nchi lazima itakushinda.Huu ni Ubaguzi mbaya kuliko ata ule wa wazungu
Waoga mno yaaniHawataki maoni mbadala.
Na bado tunaambiwa upinzani ULISHAJIFIA!Hivi kwanini Magufuli huwa ni muoga wa hoja hivyo? Ana shida gani hasa!