Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt Dorothy Gwajima anatarajiwa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2025/26, jijini Dodoma leo.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima amewasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2025/ 2026 jijini Dodoma leo ambapo ameomba kupitishiwa bajeti ya jumla ya Sh76 bilioni.
Wabunge wakichangia mjadala wa kupitisha bajeti hiyo wamekuwa mbogo wakipinga matukio ya ukatili wa kijinsia, ubakaji na ukiukwaji wa maadili ya Kitanzania. Picha na Edwin Mjwahuzi