Bunge la 12 Mkutano wa 16 Kikao cha 9, Septemba 6, 2024

Bunge la 12 Mkutano wa 16 Kikao cha 9, Septemba 6, 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kama kawaida, Bunge linaendelea muda huu na ni kipindi cha maswali na majibu ambapo wabunge wanauliza na mawaziri wanajibu hoja husika, tuwe pamoja kufatilia yanayojiri kutoka viunga vya mji wa Dodoma.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Uchukuzi kuendelea kulisimamia kwa karibu Shirika la Reli Tanzania (TRC) na kuhakikisha huduma za treni ya SGR zinaboreshwa.

Pia, Majaliwa ameagiza miundombinu ya mradi huo inaimarishwa ili uweze kudumu kwa muda mrefu. Kauli ya Majaliwa inakuja wakati baadhi ya wadau wakiwemo watumiaji wa usafiri huo wakipongeza huku wengine wakilalamikia huduma duni ndani ya usafiri huo.

Tayari Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Morogoro, ilibaini kuwepo kwa baadhi ya abiria wanaohujumu mradi huo kwa kulipa nauli pungufu na kuishauri TRC hatua za kuchukua kudhibiti hali hiyo.

Waziri Mkuu Majaliuwa amesema katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali itaendeleza sekta ya uchukuzi ambapo pamoja na mambo mengine itasimamia sekta ya reli ikiwemo ujenzi wa SGR na uendeshaji wake kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.



View: https://www.youtube.com/watch?v=4Xjcogy8Mak
 
Kama kawaida, Bunge linaendelea muda huu na ni kipindi cha maswali na majibu ambapo wabunge wanauliza na mawaziri wanajibu hoja husika, tuwe pamoja kufatilia yanayojiri kutoka viunga vya mji wa Dodoma


View: https://www.youtube.com/watch?v=4Xjcogy8Mak

Tangu hii nchi ilipopata Uhuru, naamini haijawahi kuwa na bunge la mchongo kama hili la 2020-2025. Binafsi hata sishangai kuona linavyo puuzwa na wananchi walio wengi.
 
Back
Top Bottom