Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Wakuu
Katika mkutano wa 18 wa Bunge unaoendelea Jijini Dodoma, leo katika kikao cha 11, wabunge watasikia na kujadili taarifa za kamati mbili za kudumu za Bunge kwa kipindi cha kuanzia Februari mwaka jana, 2024 hadi Januari mwaka huu baada ya Kipindi cha Maswali na Majibu.
Kamati hizo ni ile ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na ile ya Elimu, Utamaduni na Michezo.
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Mhe. Daniel Sirro amesema katika kipindi cha kuanzia mwaka 2022 hadi 2024 jumla ya wananchi 1,113 wamepoteza maisha kutokana na ajali zilizosababisha na pikipiki kwa mchanganuo ufuatao;

Naibu Waziri Sirro: Ajali za Pikipiki zaua Watu 1,113 nchini kwa miaka Miwili
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani Mhe. Daniel Sirro amesema katika kipindi cha kuanzia mwaka 2022 hadi 2024 jumla ya wananchi 1,113 wamepoteza maisha kutokana na ajali zilizosababisha na pikipiki kwa mchanganuo ufuatao;
- Madereva wa Pikipiki waliopata ajali na kufariki 759
- Abiria waliopanda Pikipiki na kupata ajali na kufariki 283
- Watu waliokuwa wanatembea kwa miguu kando kando ya barabara au njiani ama walikuwa wanavuka barabara na kupata ajali kwa kugongwa na pikipiki na kufariki dunia ni 71