Bunge la 12: Mkutano wa 8 kikao cha pili, Septemba 14, 2022
TUME YA KUCHUNGUZA MAUAJI YAKAMILISHA KAZI YAKABIDHI MAJIBU SERIKALINI
Tume iliyoundwa kuchunguza ongezeko la mauaji Nchini na kutoa mapendekezo imekamilisha kazi na imewasilisha majibu Serikalini.
Imeelezwa majibu yanafanyiwa kazi na kukiwa na umuhimu wa kufikisha kwa Wananchi Serikali itafanya hivyo.
Akijibu swali Bungeni, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Khamis Hamza Khamis kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni ametaja vyanzo vikubwa vya mauaji ni Wananchi kujichukulia Sheria mkononi, wivu wa mapenzi, migogoro ya ardhi, ulevi, imani za kishirikina.
Mpaka ripoti ije itoke mauaji yameshatokea mengi mengine yanayohutaji tume tena.