Bunge la 12: Serikali yasema Wakazi wa Dar watasambaziwa huduma ya mabomba ya gesi

Bunge la 12: Serikali yasema Wakazi wa Dar watasambaziwa huduma ya mabomba ya gesi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Fuatilia kinachojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 15, Kikao cha 3, leo Aprili 4, 2024.


NAIBU WAZIRI: SERIKALI INA MKAKATI WA KUPELEKA GESI KATIKA NYUMBA 10,000 ZA DAR
DODOMA: Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amesema Serikali inatarajia kuongeza huduma ya matumizi ya Gesi Hasilia kwa wakazi wa Dar es Salaam na tayari kuna mpango wa kuifikisha katika nyumba 10,000 Jijini hapo.

Ameongeza “Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) imesambaza Miundombinu ya Gesi Hasilia katika nyumba 880 za Dar, imejenga Bomba la Gesi lenye urefu wa Kilometa 12.4 kutoka Mwenge hadi Mbezi Beach kupitia Barabara ya Bagamoyo na tayari viwanda viwili na hoteli sita vimeunganishwa na bomba hilo.”

Ametoa maelezo hayo Bungeni baada ya Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima kuhoji lini Serikali itaweka Bomba la Gesi kila nyumba kwa Wakazi wa Dar ili Wananchi wapate nishani nafuu.



Esther Bulaya: Serikali inachukua pesa kwenye mifuko ya hifadhi lakini hairejeshi
Esther Bulaya amezungumzia kuwa adha wanayopata wastaafu haswa kwenye janga la kikokotoo, Mahitaji yao ilikuwa kuchukua asilimia 50 kwa mkupuo. Bado kuna mlalamiko kwa madaktari, polisi, hizi ni pesa zao mafao wapate kwa asilimia 50 sio kupewa kwa Mwezi.

Mifuko yetu ina shida, serikali inachukua hela kwenye mifuko kwenye uwekezaji lakini hawalipi, hivyo kufanya mifuko hiyo kutokuwa stable. Tathimini za uwezekezaji hazifanyi vizuri, hiyvo hela hizo zikikopwa kwenye mifuko kwa ajili ya kuwekeza lakini hazina faida za kurudisha pesa hizo katika mifumo hio ya waajiriwa.

 
Mtoa maada siku nyingine jalibu kutuheshimu japo kinafiki umewaza waza Nini mpaka kutuletea talifa ya kamati kuu ya CCM inatuhusu Nini au wewe ndio Amos makalla umeamza kazi lasimi?
 
Haya ya mabomba maji yanavo pasuka ovyo ndo waje na ya gesi.
Jinsi navopata picha dar ikiwaka moto kama jiko la gesi.tena mna makala mwenezi wa CCM aka moto benga
 
izo gesi zitakazosambazwa majumbani itakuwa bure kimatumizi ama tutalipia kama ruku
 
Suala la usambazaji wa huduma ya Maji tu, Kuna watu Wana miezi 8 hawajapata huduma ya Maji ndiyo iwe ya gas?

Serikali iache kufanya mambo kisiasa badala yake wajikite kwenye kutatua kero za Wananchi wake.

Umeme Wenyewe sio wa uhakika Mwaka wa 63 huu tangu tupate Uhuru 🙌
 
Back
Top Bottom