Bunge la Awamu ya 5 lilikuwepo kutimiza muundo wa nchi tu

Bunge la Awamu ya 5 lilikuwepo kutimiza muundo wa nchi tu

Kipenzi Changu

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
59,734
Reaction score
140,476
Katika umri wangu mdogo nimepata kulijua bunge la Spika Samuel Sitta, Mama Anne Makinda na sasa Job Ndugai.

Pamoja na changamoto za kubinya upinzani katika mabunge yaliyopita lakini angalau yaliweza kuwa wazi na kuisimamia serikali.

Kashfa mbalimbali zilizoibuliwa na wabunge kwa kushirikiana na CAG zilifanyiwa kazi na mijadala yake kuwa mikali. Mawaziri mafisadi walisemwa wazi bungeni na mamlaka za uteuzi zilitengua uwaziri au wahusika kujihudhuru.

Hali imekuwa tofauti kabisa katika bungeni la awamu ya 5. Bunge limewekwa kwenye friji limekuwa baridiiiii. Kuna nyakati huwa nasahau kama tuna bunge.Baadhi ya rafiki yangu wa nchi ya kigeni aliwahi kuniuliza Tz hakuna bunge?

Bunge limekosa kujitofautisha na serikali. Kwa maoni yangu naona kama lipo kukamilisha muundo tu,lakini sio kufanya kazi yake kusudiwa.

Ninaweza kusema bwana mdogo kama mimi ningekuwa spika ningefanya vizuri mara 80 ya spika Ndugai. Ndugai amekosa sifa hata za kuwa mjumbe wa mtaa.

Matokeo ya hali hii tunaiona kipindi hiki cha uchaguzi ambapo kila mtu anajiona anaweza kuwa mbunge. Firikia Shishi Baby, Steve Nyerere, Hamornize nk wameona wanatosha.
 
Ndugai ni mwanaCCM. Mwenyekiti wa chama chake ni Rais Magufuli. Na msimu huu Magufuli ndio ataamua nani agombee - nani asigombee ubunge wa CCM - wajumbe wa kamati kuu watakuwa wakiitikia tu; "sawa baba - eeh sawa mkuu - sawa mzee" Ndugai lazima afanye vile ili apewe nafasi.
 
Tunakoelekea bunge lijalo itakuwa afadhali ya mgonjwa huyu, hata wanao wachagua nao shida tupu nisawa na wote wagonjwa mnatafuta mmoja wenu asimame kuwachukulia dawa
 
Nimesikia vyombo vya habari vya Marekani na Uingereza kuwa bunge la China ni rubber stamp kulinganisha na mabunge ya kwao.
Sasa najiuliza kwanini China inakuwa na wabunge kama kazi yao ni kusema ndioo kila hoja ya serikali.
Je bunge la Tanzania kwa sasa limegeuka la China?
 
Tulikuwa tunavutiwa na bunge unaangalia kabisa, siku hizi hata sijuagi lipo lini limeisha lini labda nikute kwenye taarifa ya habari, ilikuwa maswali kwa PM lazima kuyafuatilia lakini hili mmmmm
 
Ni bunge lililofedhehesha nchi,katika historia ni bunge dhaifu lililotumika kinyume cha matakwa ya wananchi!!
 
Nimesikia vyombo vya habari vya Marekani na Uingereza kuwa bunge la China ni rubber stamp kulinganisha na mabunge ya kwao.
Sasa najiuliza kwanini China inakuwa na wabunge kama kazi yao ni kusema ndioo kila hoja ya serikali.
Je bunge la Tanzania kwa sasa limegeuka la China?

Huhitaji elimu ya juu kujua bunge hili ni rubber stamp. Ni kweli kabisa bunge hili ni kama hilo la China.
 
Naam, ulikua ni mhuri wa serikali tu, kila kilichopelekwa kilipita kama kilivyo, muda mwingi waliutumia kumwimbia nyimbo za mapimbio magufuli.

Bunge la ndungai litakumbukwa kwa udhaifu wake.
Bunge la Awamu hii hakikuwa na Spika bali lilikuwa na Mwenyekiti wa Wabunge wa ccm
 
Udikteta tunaouruhusu nchini baadhi ya matokeo yake ni hayo.
 
ndugu yangu mtoa mada masikio unayo husikii hata na macho hayaoni? upepo mkali wote unavuma bongo huuoni? nani kati yetu hakuona au kusikia kilichompata Mo, Ben Saatisa, Azore, Roma, Manji, Lisse Mdudi , watu wa Kibiti , Maiti za Coco Beach na sasa DJ Makengeza? wote waliimba vizuri wimbo wa Kanyaga Kanyaga everibari sei Unoooo!!

hivi sera hizi za kununua wapinzani kuwalima risasi kuwapiga faini na tumbua tumbua yote wewe ungepewa kazi ya Mgogo Agwe Nduguyao ungeweza kuwapa nafasi wapinzani na kuiadabisha sirikali hii ya kibabe? huogopi kutumbuliwa wewe kwa pepa au risasi? huogopi kunyakuliwa na watu wasiojulikana?? huogopi kuuwawa?

wabongo mnaonaje tuache unafiki sasa na tuanze kwa mbaaaaaali kusema ukweli? sirikali iliyoko madarakani inatisha mno raia wote wameloa maji na wamejaa hofu kubwa mno ya maisha yao hasa wapinzani!!watu wote kimyaaaaa!!!ukiongea kupinga juhudi tu wanakusaka na kukupoteza!!! hiyo sijui Declaration of Human nanihii imebaki uzunguni tu hapa sasa ni mwendo wa risasi faini maji ya kuwasha na kwata tu, sote ni kwa lazima tuunge mkono juhudi japo mimi ni kijani sina shida na hilo nawasikitikia mno wale wa upande wa pili!! pole sana wabongo wote tulikuwa huru miaka michache iliyopita uhuru wa mawazo na kukusanyika uhuru wote umetoweka ghafla sote tumeingizwa jela!!

Bw Mgogo Nduguyao katimiza wajibu wake kupeleka jahazi la bunge upepo ulipompeleka si kule walikotakiwa kwenda, unataka kusema Bw Nduguyao hajitakii mema?? huyu mgogo ni kunguru mwoga kakimbiza ubawa wake!!kwa risasi hizi za mchana kweupeeee kule Dom hata ningekuwa mimi ndio Mhe Supika ningekunja mkia wangu kama mbwa koko!!! big up sana Mh Nduguyao!!!!Nani alisema wagogo hawana akili (wasina mahala)! wakati mgogo kama ana safari ya Dom to Dar na hana nauli we unapanda basi ye anachukua Zeze anaanza mwendo wa miguu huku akipiga zeze akiimba na kucheza Maduga we njoo nkutume Maduga we nje nkutume Maduga weeeee safari inaendelea akifika Kibaigwa anapanda fisi wake hadi mbezi anashushwa tahamaki mnaingia nae ubungo unabaki unashangaaaaa!!!!kwa taarifa tu wasiojua wagogo ni jamii ya watu wapole, wakarimu , waoga na watiifu na wanaongoza duniani kwa uwezo binafsi wa kutembea safari ndefu kwa miguu!!
 
ndugu yangu mtoa mada masikio unayo husikii hata na macho hayaoni? upepo mkali wote unavuma bongo huuoni? nani kati yetu hakuona au kusikia kilichompata Ben Saatisa, Azore, Lisse Mdudi na sasa DJ Makengeza? wote waliimba vizuri wimbo wa Kanyaga Kanyaga!!

hivi sera hizi za kununua wapinzani kuwalima risasi kuwapiga faini na tumbua tumbua yote wewe ungepewa kazi ya Mgogo Nduguyao ungeweza kuwapa nafasi wapinzani na kuiadabisha sirikali hii ya kibabe? huogopi kutumbuliwa wewe kwa pepa au risasi? wabongo mnaonaje tuache unafiki sasa tuanze kusema ukweli? sirikali iliyoko madarakani inatisha mno raia wote wameloa maji na wamejaa hofu kubwa mno ya maisha yao hasa wapinzani!!watu wote kimyaaaaa!!!ukiongea kupinga juhudi tu wanakusaka na kukupoteza!!! hiyo sijui Declaration of Human imebaki uzunguni hapa sasa ni mwendo wa kwata tu, pole sana wabongo tulikuwa huru miaka michache iliyopita uhuru wa mawazo umetoweka ghafla sote tumeingizwa jela!!

Bw Mgogo Nduguyao katimiza wajibu wake kupeleka jahazi la bunge upepo ulipompeleka si kule walikotakiwa kwenda, unataka kusema Bw Nduguyao hajitakii mema?? huyu mgogo ni kunguru mwoga kakimbiza ubawa wake!!
Duuh umetiririka hatari ...nduguyao [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom