ndugu yangu mtoa mada masikio unayo husikii hata na macho hayaoni? upepo mkali wote unavuma bongo huuoni? nani kati yetu hakuona au kusikia kilichompata Ben Saatisa, Azore, Lisse Mdudi na sasa DJ Makengeza? wote waliimba vizuri wimbo wa Kanyaga Kanyaga!!
hivi sera hizi za kununua wapinzani kuwalima risasi kuwapiga faini na tumbua tumbua yote wewe ungepewa kazi ya Mgogo Nduguyao ungeweza kuwapa nafasi wapinzani na kuiadabisha sirikali hii ya kibabe? huogopi kutumbuliwa wewe kwa pepa au risasi? wabongo mnaonaje tuache unafiki sasa tuanze kusema ukweli? sirikali iliyoko madarakani inatisha mno raia wote wameloa maji na wamejaa hofu kubwa mno ya maisha yao hasa wapinzani!!watu wote kimyaaaaa!!!ukiongea kupinga juhudi tu wanakusaka na kukupoteza!!! hiyo sijui Declaration of Human imebaki uzunguni hapa sasa ni mwendo wa kwata tu, pole sana wabongo tulikuwa huru miaka michache iliyopita uhuru wa mawazo umetoweka ghafla sote tumeingizwa jela!!
Bw Mgogo Nduguyao katimiza wajibu wake kupeleka jahazi la bunge upepo ulipompeleka si kule walikotakiwa kwenda, unataka kusema Bw Nduguyao hajitakii mema?? huyu mgogo ni kunguru mwoga kakimbiza ubawa wake!!