Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nani msemakweli - maneno ya mdomoni ya waziri Mkulo au taarifa iliyoandikwa na yeye mwenyewe? Ina maana hakusoma kilichoandikwa; je achukuliwe hatua gani?
84. Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Usalama Barabarani, Sura, 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati wa uendeshaji gari barabarani (Traffic Notification Fee) kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 300,000.
https://www.jamiiforums.com/busines...-watumishi-wa-serikali-na-mashirika-yake.html
Tafsiri yangu kutokana na kutotoza kodi kwenye posho za watumishi wa serikali na taasisi nyingine zinazopata ruzuku ya serikali ni kuwa "watawala wameungana na wafanyakazi wao na wanasiasa" kutekeleza sheria ya mapato ya mwaka 2004 kibaguzi. Nasema hivi kwa sababu mabadiliko hayo yatawahusu:
(i) Viongozi wakuu wa serikali ambao mbali na mishahara yao wana posho mbalimbali zinazozidi hata mishahara ambazo kwa mujibu wa sheria ya mapato ya mwaka 2004 zinatakia kulipiwa kodi lakini kwa kuwa wao ndio walioshika mpini wameamua kutokulipa kodi;
(ii) Wafanyakazi wa serikali na taasisi zake nao wanaungana na watawala kutokulipa kodi. Kwa tafsiri hii watajipangia mishahara midogo na sehemu nyingine kujilipa kama posho na hivyo kutokulipa kodi;
(iii) Wanasiasa - kutokana na vyama vya siasa kupata ruzuku ya serikali watawalipa watumishi wao posho badala ya mishahara na hivyo kutokulipa kodi kabisa.
Matokeo hasi ya mabadiliko haya ni kuwa
(a) Utendaji wa TRA kwenye kuhimiza ulipaji wa kodi za mishahara kwenye sekta binafsi hasa kwenye posho utapata upinzani, ilitakiwa wadai kodi wakionyesha mfano wa wao kulipa hizo kodi kinyume chake wao hawatalipa bali watawataka wafanyakazi wa sekta binafsi walipe. Wakati wa utawala wa Mh. Mwinyi, serikali ilifuta kodi kwenye posho na matokeo yake Mh. Mustafa anafahamu kwani Serikali ilikuwa na hali mbaya sana kifedha na
(b) Nia ya serikali kukuza sekta binafsi itafifishwa na rekebisho hili kwani nguvu kazi kubwa itapendelea kufanya kazi kule ambako watalipa kodi kidogo
(c) Kutakuwepo tofauti ya mapato kwa watu wa kada moja mfano nesi anayefanya kazi serikalini posho zake za night allowance hazitatozwa kodi lakini nesi ambaye yuko hospitali binafsi posho zake za night allowance zitatozwa kodi.
Mtazamo wangu ni kuwa rekebisho hili ni mtego mkubwa kwa wabunge wetu. Endapo watapitisha rekebisho hili, ina maana wako bungeni kwa maslahi binafsi kwani wao na vyama vyao ni sehemu ya watu watakaofaidika na rekebisho hili. Kwa upande mwingine, chama cha waajiri Tanzania na vyama vya wafanyakazi ambao si wa sekta ya umma ni wakati mwafaka kujitokeza na kupinga rekebisho hili kwa ajili ya ustawi wa nchi yetu.
Chadema ni kama mwanamke mjamzito akifanyiwa zuri kwake karaha akifanyiwa baya ndio tabu! Sasa mnataka Serikali ipuuze kila linalosemwa na Upinzani!