Bunge la bajeti 2011/2012 na yatokanayo

Bunge la bajeti 2011/2012 na yatokanayo

You may wish to understand that sytems in themselves do not curb corruption. Do you want us to believe that currently there no systems? Should your allegations be true, then Tz is a jungle!! No No.
The other question you could be asking is: how many, for example, daladala drivers wlll pay fifty tzs? The possibility is that they will not afford and because they will not afford they will pay less, and because they will pay less the money will find their way in the pockets of law enforcers or the drivers will end in prison.
Prudence seems to dictate that, fine should be affordable, feel pinch and make the defaulter refrain from similar acts.
Most of us notice what the police
do..,,..
Am talking of an ICT solution brother...a system that fines you but you do not give the cash to the traffic police!!! you go pay in their offices. Later we will incorporate this system to the m-pesa/zap/tigo-pesa services...you pay ur fines and your name is cleared in the database. Otherwise, the tracking devices will catch u...!
oooops, m talking too much ***THIS IS TOP SECRET***
and the thing is, it is being made by Tanzanians in Tanzania...stay tuned!
 
Na kama ukimalizana na trafiki kiaina, hiyo system itakuona? Try to think the fifty thousand against, let say the ten thousand!!!!
 
Samahani wakuu naomba kuuliza kama bunge linaendelea au liliahirishwa siku ile Mkulo alipomaliza kutusomea bajeti. Nauliza hivi kwasababu sisi wengine tunakaa vijijini ambako nyakati fulani huwa tunapata nafasi japo kwa muda mfupi kufuatilia mijadala kutoka mjengoni, kupitia luninga yetu pendwa ya Star TV iliyokuwa inaonyesha kila kitu live bila mchele mchele. Baadae TBC nao waliiga kutoka kwa Star tv, ingawa wao TBC wakawa hawaonyeshi kwa muda mrefu na hasa kukiwa na mijadala mikali mikali dhidi ya Serikali. Naomba mlioko huko Dom mtujuze kama waheshimiwa wapo mjengoni au walishasepa. Kama wapo ndo kusema Tv zimepigwa marufuku mjengoni, au kuna mabadiliko kwamba wananchi tumefutiwa haki ya kufuatilia mijadala ya mjengoni live!
 
imekuwa postponed hadi Jumatano tarehe 15/6/2011 kuanzia saa 3 kamili asubuhi.
 
Asante sana Mkuu kwa taarifa na kunitoa dukuduku.
 
Kwa kweli inasikitisha kweli budget ya mwaka huu,inasema italenga katika kuengeza kutoa posho na kulipa madeni ya serikali,hivi hayo madeni ya mikataba feki ilipe serikali au viongozi walioingia katika mikataba hio ?

Viongozi hutumia fursa ya kuiba pesa katika kuingia mikataba mibovu,hii ndio sera ya ccm,chukua chako mapema,ndio CCM,kama hamufamua watanganyika na wazanzibari,kinachonishangaza zaidi kwa nini wananchi hawafaidiki na budget hiii.

Kuna rasilimali munazo watanganyika mbona hamufaidki ? Niwape siri sasa,kwanza niwaulize rasilimali zenu hio migodi na gas inasimamiwa na serikali gani ? Tanganyika haipo,sasa zinasimamiwa na serikali ipi ? Katika makubaliano ya muungano hizi rasilimali hazimo,na wala sio za muungano,sasa jiulizeni ikiwa sio za muungano zinasiimamiwa na nani ?

Tumieni akili jamani watanganyika,daini serikali yenu ambayo itawaletea haki zenu na mutafaidikia,hapa katika muungano kuna kiini macho,kuna ulaji mkubwa unatumiwa na viongozi,moja ni rasilimali,kwa hio cha kufanya kwanza daini tanganyika irudi,ndio mudai katiba ambayo itawapatia fursa wananchi katika kujenga nchi na kupata fadhila za nchi na kufaidkika rasilimali zenu kwa faida yenu,na vizazi vyenu.

Bajeti hii imelenga sana kwa viongozi na upumbavu wao wa madeni feki,wewe ndo kwanza unahangaika kariakoo na hujui ni cha kufanya,rais haijui bei ya chai bei gani,wala panadol,hapa tanganyika unalipia maji,umeme, umeme wenyewe wa mgao,elimu unaliza,maji taka,hata bei ya kichwa wewe mwenyewe unalipa,sasa niulize hio bajeti wewe imekugusa vipi ?

Umepata elimu bure ,umepata matibabu bure ? Umepata maji bure ,hakuna ? kazi kwenu,nchi ipo mikononi mwenu,nyinyi ndio serikali wananchi,mukisema hatutaki basi hamutaki,waliwezaje tunisia nyie musiweze ?

Sisi wazanzibari tuko mbioni kupigania haki zenu na dola yetu tulionyang'anywa na muungano,ambao wanaofaidika ni watu wachache.
 
Thursday, 09 June 2011 23:37

Begi lililokuwa limebeba bajeti ya Serikali ambayo Chadema imeamua kuichana

Neville Meena, Dodoma

KAMBI ya Upinzani Bungeni imedai kwamba kuna upotoshaji mkubwa katika Bajeti ya Serikali iliyowasilishwa bungeni juzi na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, huku ikidai kwamba bajeti hiyo ni ya kulipa posho na madeni.

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Kambi hiyo mjini Dodoma na kusainiwa na Waziri Kivuli wa Fedha, Zitto Kabwe inabainisha kuwa upembuzi uliofanywa umebaini kuwapo kwa upotoshaji mkubwa wa kitakwimu na kimaudhui uliofanywa kwalengo la kuwajengea matumaini wananchi.

"Kambi ya Upinzani Bungeni imeshtushwa na kushangazwa na hatua ya Serikali kutenga zaidi ya robo ya bajeti kulipa madeni na kulipana posho (asilimia 27), asilimia 14 kulipa madeni na asilimia 13 kulipa posho mbalimbali," ilisema taarifa hiyo.

Miongoni mwa maeneo ambayo yanadaiwa kuwa na upotoshaji ni kiasi cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya kukabiliana na tatizo la umeme, ongezeko la jumla la Bajeti ya Serikali ikilinganishwa na ile ya mwaka 2010/11, posho mbalimbali, faini kwa madereva wazembe na ulipaji wa madeni ya Serikali.

Hakuna mradi mpya wa umeme
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tamko la Serikali kwamba imetenga kiasi cha Sh537 bilioni kwa ajili ya kutatua tatizo la umeme, si kweli kwani kwa jumla Wizara ya Nishati na Madini, imetengewa Sh402.071 bilioni na kwamba hakuna mradi mpya wa umeme hata mmoja utakaoanzishwa.

"Fedha hizo zimegawanywa katika mafungu ya matumizi ya kawaida Sh76,953,934,000 na kwa upande wa bajeti ya maendeleo zimetengwa Sh325,448,137,000. Sh325 bilioni zilizotengwa kwa ajili ya maendeleo ya Wizara ya Nishati na Madini zinatosha kwa mradi mmoja tu wa umeme wa 160 MW, 100 Dar es Salaam na 60 Mwanza,"inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Zitto ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, alisema katika taarifa hiyo kuwa, kutokana na hali hiyo hakuna mradi mpya wa umeme unaoonekana katika bajeti hiyo na kwamba kauli ya Mkulo ililenga zaidi kuwajengea wananchi matumaini hewa na si hatua za kweli kumaliza matatizo ya umeme nchini.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, hakuna ongezeko lolote halisia la fedha katika bajeti ya mwaka huu, kwani kati ya Sh13.525 trilioni zilizotengwa, Sh1.901 trilioni, sawa na asilimia 14.06 ya bajeti yote ni kwa ajili ya kulipa madeni ya Taifa.

"Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha Serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki Sh11.624 trilioni ambazoni ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka unaomalizika wa 2010/2011," alisema Zitto katika taarifa yake hiyo na kuongeza: "Kwa kuzingatia kwamba thamani ya shilingi imekuwa ikishuka, bajeti iliyotangazwa ni ya kulipa madeni".

Bajeti ya posho sasa Sh987 bilioni
Kuhusu hatua za kupunguza posho, kiongozi huyo alisema hakuna ukweli wa kauli hiyo kwani Serikali imetenga kiasi cha Sh987 bilioni kwa ajili ya kulipa posho mbalimbali, fedha ambazo ni sawa na asilimia 13 ya bajeti nzima.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa kutokuwapo kwa nia ya dhati ya kupunguza posho, inaonekana katika hatua za kufanya marekebisho katika sheria ya kodi sura ya 332 ili kusamehe kodi ya mapato katika posho wanazolipwa wafanyakazi wa Serikali na wanaofanya kazi katika taasisi zinazopata ruzuku kutoka kwenye Bajeti ya Serikali.
"Hii inaonyesha kuwa kauli ya kufuta au kupunguza posho ilitolewa na Serikali ili kupumbaza wananchi, lakini haina udhati,"alisema.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa bajeti imeongeza mzigo mkubwa kwa wananchi kutokana na hatua yake ya kuongeza kiwango cha faini kwa madereva wazembe kutoka Sh20,000 hadi Sh300,000, na kwamba kiasi cha Sh50,000 kilichotangazwa na Waziri Mkulo juzi kinatofautia na maelezo kwenye vitabu vya bajeti.

Alisema hatua hiyo itawaathiri wananchi hasa vijana walioajiriwa ama kujiajiri katika huduma za usafiri na usafirishaji na kwamba kipengele hicho pia kinalenga kuuhadaa umma.

Serikali juzi ilitangaza hatua kadhaa za kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima katika mwaka wa fedha wa 2011/2012, lakini fedha za matumizi mengineyo, maarufu kama Other Charges (OC), zimeongezwa kwa asilimia 8.62 ikilinganishwa na Bajeti ya Serikali inayofikia ukomo tarehe 30 mwezi huu.

Fedha za OC katika bajeti mwaka ujao wa fedha ni Sh3.089 trilioni ikilinganishwa na kiasi cha Sh2.823 kilichotengwa katika mwaka wa fedha wa 2010/2011, likiwa ni ongezeko la Sh266.599 bilioni.

Fungu la fedha za OC ndilo hutumika kugharimia posho mbalimbali kwa watumishi wa umma na uendeshaji wa semina, warsha na makongamano pamoja na kugharimia safari za viongozi ndani na nje ya nchi.

Kafulila adai bajeti haijazingatia vigezo vya uchumi
Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila aliliambia Mwananchi katika viwanja vya Bunge kuwa, hali hiyo inadhihirisha kwamba bajeti iliyowasilishwa na Mkulo ililenga zaidi kutafuta kuungwa mkono kuliko kuzingatia vigezo vya kiuchumi.

"Kama mwaka wa fedha unaoishia mwishoni mwa mwezi huu fedha za OC ni kidogo kuliko zile ambazo zimetengwa mwaka ujao wa fedha, basi ni dhahiri kwamba hatuwezi kusema posho zitapunguzwa, hapa nadhani kuna tatizo,"alisema Kafulila.

Alisema fungu la fedha za OC lazima lipitiwe upya kwani fedha zilizotengwa ni zaidi ya kiasi cha fedha ambazo Serikali imeomba kutoka kwa nchi wahisani kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.

"Iwapo fedha za OC ni Sh3 trilioni na fedha za miradi ya maendeleo tunazoomba kutoka kwa wafadhili ni kiasi hicho hicho, utaona kwamba ni jambo la kushangaza, hapa kuna mambo mengi ya kuweka sawa,"alisema Kafulila, huku akibainisha kuwa bajeti hiyo ya Serikali si mbaya sana kwani imekumbuka umuhimu wa miundombinu ya usafirishaji.

Akiwasilisha bungeni juzi Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2011/12, Waziri Mkulo alibainisha hatua kadhaa za Serikali kudhibiti matumizi yasiyokuwa ya lazima akiahidi kupunguza posho zisizo na tija, safari za ndani na nje za viongozi na ukubwa wa misafara ya viongozi hao ili fedha husika ziweze kutumika kugharimia shughuli nyingine za maendeleo.

"...........Serikali itasitisha ununuzi wa samani za ofisi, hususan zile zinazoagizwa kutoka nje ya nchi, kupunguza malipo ya posho mbalimbali yasiyokuwa na tija, kupunguza matumizi ya mafuta kwa magari ya Serikali, kupunguza safari za ndani na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na ukubwa wa misafara na kuendelea kupunguza semina na warsha, isipokuwa pale inapobidi na kwa kibali cha Ofisi ya Waziri Mkuu..," alisema Mkulo.

Sh3 trilioni kutoka nchi wahisani
Kadhalika majedwali ya ufupisho wa hesabu za bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/12 yanabainisha kuwa fedha za maendeleo zinazotarajiwa kutoka kwa nchi wahisani ni kiasi cha Sh3.054 trilioni. Kiasi hicho kinazidiwa kwa asilimia 18.9 sawa na Sh5.853 bilioni kikilinganishwa na fedha za OC ambazo ni Sh3.089 trilioni.

Katika bajeti hiyo, fedha zote zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya miradi ya maendeleo ni Sh4.925 trilioni, ambapo fedha za ndani ni Sh1.871 trilioni.

Mchanganuo mzima wa bajeti hiyo unaonyesha kuwa fedha za miradi ya maendeleo zilizotengwa ni sawa na asilimia 31 ya bajeti nzima, wakati fedha za matumizi mengineyo (OC) ni sawa na asilimia 32, mishahara asilimia 23, malipo ya madeni asilimia 8, madeni mengine asilimia 3 na riba ya madeni ya ndani na nje asilimia 3.
 
hapo sasa uelewa wa tanzania ni mdogo mno hivyo na washukuru wapinzani kwa kuliona hilo tusaidieni tuko pamoja wapiganaji juu kitaeleweka.
 
[TABLE="class: cms_table"]
[TR]
[TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="class: cms_table"]
[TR]
[TD]wakati Mh mbowe akifagilia bajeti ya mkulo mengi yajitokeza kiasi cha kutilia shaka umakini wako, next time bora uombe muda kwa waandishi wa habari wa kufanyia kazi jambo kabla ya kukurupuka na kujibu

Martin Malera, Dodoma

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[/TD]
[TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="class: cms_table"]
[TR]
[TD]WAZIRI wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, anadaiwa kulipotosha taifa kitakwimu na kimaudhui uliofanywa kwa lengo la kuwajengea wananchi matumaini hewa yenye kuonyesha serikali inawajali na kusikiliza matatizo yao.
Matumaini hayo aliyaonyesha kupitia hotuba yake ya bajeti ya mwaka 2011/2012 juzi ambayo ilionyesha kuwa kutakuwa na nafuu ya maisha wakati hali halisi haipo hivyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi wa kambi ya upinzani, Zitto Kabwe, na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika.
Katika taarifa yao iliyotolewa kwa niaba ya kambi ya upinzani, wabunge hao walisema wameshtushwa na upotoshaji huo ambao walisema una lengo la kuwapa wananchi matumaini hewa.
“Hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2011/2012 ina upotoshaji mkubwa, tuna uhakika ulifanywa kwa makusudi ili kuonyesha serikali inajali matatizo ya wananchi.”
Akiainisha maeneo aliyodai yamepotoshwa, Zitto alisema wakati waziri akitaja kipaumbele cha kwanza cha bajeti hiyo kuwa ni kumaliza tatizo la umeme na serikali imetenga sh trilioni 537, upembuzi uliofanywa na kambi ya upinzani kwenye vitabu vya bajeti (Kitabu Namba II na IV) vilivyotolewa na serikali yenyewe, umebaini kuwa Wizara ya Nishati na Madini imetengewa sh 402,402,071,000 kwa mujibu wa fungu la 58.
Alisema fedha hizo zimegawanywa katika mafungu ya matumizi kawaida sh 76,953,934,000 na kwa upande wa bajeti ya maendeleo zimetengwa sh 325,448,137,000.
Alisema sh bilioni 325 zilizotengwa katika bajeti ya maendeleo ya Wizara ya Nishati na Madini zinatosha kwa mradi mmoja tu wa umeme wa megawati 160 zikiwamo megawati 100 za Dar es Salaam) na 60 za Mwanza.
“Hakuna mradi wowote mpya wa umeme unaoonekana katika bajeti. Ni dhahiri kuwa kauli ya Mkulo ililenga zaidi kuwajengea wananchi matumaini hewa kuliko kuchukua hatua za kweli za kumaliza tatizo la umeme,” ilisema taarifa hiyo.
Eneo lingine la upotoshaji ni hili: wakati waziri na serikali anataka kuwaaminisha Watanzania kuwa bajeti ya mwaka huu imeongezeka kuliko ilivyokuwa ya mwaka 2010/2011, kambi ya upinzani inasema kuwa hakuna ongezeko lililofanyika.
“Bajeti iliyopita ilikuwa sh trilioni 11.6 wakati mwaka huu wa 2011/2012 serikali ina bajeti ya jumla ya sh trilioni 13.525…Kati ya fedha hizo za mwaka huu kiasi cha sh trilioni 1.901 ambazo ni sawa na asilimia 14.06 ya bajeti yote, kitatumika kulipia deni la taifa.
“Kwa mantiki hiyo, mtaona kuwa fedha kwa ajili ya kuendesha serikali pamoja na kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo zitabaki kuwa ni kiasi cha sh trilioni 11.624 ambazo ni sawa na fedha za bajeti ya mwaka wa fedha uliomalizika (Japo thamani ya shilingi imeanguka ukilinganisha na hali ilivyokuwa mwaka 2010/2011).”
Kutokana na hali hiyo, kambi ya upinzani imesema hii si bajeti ya maendeleo bali ni ya madeni.
Katika eneo la tatu la upotoshaji, kambi ya upinzani ilisema wakati waziri akisema bajeti ya mwaka huu itapunguza posho kama sehemu ya mkakati wa serikali wa kuthibiti matumizi, ukweli ni kuwa bajeti hiyo imetenga sh trilioni 2.987, sawa na asilimia 13 ya bajeti yote kwa ajili ya kulipa posho chini ya vifungu vinavyojulikana kama “Personnel allowances (non discretionary na In-kind”).
“Kwa hiyo, kauli ya Waziri Mkulo kuwa serikali itapunguza posho sio kweli. Tunautaka umma wa Watanzania usikubali kurubuniwa,” ilisema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, bajeti ya mwaka huu imewaongezea mzigo mkubwa sana wananchi na haswa wajasiriamali wadogo na vijana ambao wamejiajiri ama kuajiriwa kwenye biashara ya usafiri na usafirishaji.
“Tunasema hivyo, kwa sababu serikali katika bajeti vipaumbele vyake rasmi vya
bajeti ni kufanya marekebisho ya sheria ya usalama barabarani sura 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati mtu akiwa anaendesha gari yaani (Traffic Notification Fee), kutoka shilingi 20,000 hadi shilingi 300,000.

Lakini Waziri Mkulo katika hotuba yake aliyoitoa jana ukurasa 74, alitamka kuwa wataongeza kiwango cha faini hadi kufikia shilingi 50,000. Ni dhahiri kuwa kauli ya waziri ya kusema faini itafikia 50,000 wakati kwenye vitabu rasmi vya bajeti faini hiyo inaonekana itafikia 300,000, hivyo alilenga kuuhadaa umma na kuupotosha,” alisema.
Taarifa hiyo ilisema kambi ya upinzani imeshtushwa na kushangazwa na hatua ya serikali kutenga zaidi ya robo ya bajeti kulipa madeni na kulipana posho (Asilimia 27 - 14 kulipa madeni na 13 kulipa posho mbalimbali).
Kambi ya upinzani inajipanga kuwasilisha bungeni bajeti mbadala Juni 15, ambayo Zitto alitamba kwamba, itakuwa inajali maslahi ya Watanzania yenye lengo la kukuza uchumi wa vijijini na itajikita katika kupata vyanzo vipya vya mapato na kubana matumizi ikiwemo kufuta posho mbalimbali.
Juzi wakati Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, akisoma mapendekezo ya bajeti ya serikali kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2011/2012, aliliambia Bunge kwamba anapendekeza nyongeza ya kiwango cha faini kwa makosa ya usalama barabarani kutoka sh 20,000 za sasa hadi sh 50,000.
Lakini katika hotuba yake iliyochapishwa kwenye vitabu maalum na kusambazwa kwa wabunge, wanahabari na makundi mengine, ilisomeka kuwa amependekeza kiwango cha sh 300,000 badala ya sh 20,000.
“Mheshimiwa Spika napendekeza kufanya marekebisho ya Sheria ya Usalama
Barabarani 168 ili kuongeza ukomo wa kiwango cha faini inayotozwa kwa kufanya makosa wakati wa uendeshaji gari barabarani (Traffic Notification Fee) kutoka shilingi 20,000 hadi sh 300,000,” ilisomeka sehemu ya hotuba ya Waziri Mkulo.

Akizungumzia utata huo, Spika wa Bunge, Anne Makinda, alikiri kuwapo kwa mkanganyiko na kuahidi kuwa Waziri Mkulo atapeleka marekebisho ya usahihi wa faini hiyo.
“Kuna makosa, nadhani waziri ataleta marekebisho ya usahihi wa faini ya makosa ya barabarani,” alisema Spika Makinda.
Wakati Makinda akitoa kauli hiyo, Naibu Spika, Job Ndugai, alisema kwa sasa Bunge linatambua kile kilichoingia kwenye Hansard za Bunge kwamba ndio sahihi. “Waziri Mkulo alitamka kwamba faini ni sh 50,000. Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, hiki kitaingia kwenye kumbukumbu zetu. Kile kiasi cha sh 300,000, hatutakitambua hata kama kimo kwenye vitabu rasmi vya serikali.”[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Wana JF imekaaje hii??
 
Mbowe nadhani bado alikuwa na wenge la kukamatwa kama mfalme kisha kupelekwa kule Arusha ndio maana akasema vile. Kateleza kdogo..!?
 
Shujaa alikuwa na mambo mengi kichwani ukihusisha na kukamatwa na Polisi,ila tupo naye milele DAIMA,VIVA CHADEMA
 
Atlast mmenitia moyo kweli lilikuwa wenge la cops, budget etc ila imemsamehe kamanda wangu ila akanushe na kuwataka radhi watz walioshangilia baada ya kusikia kauli yake kuwa budget itamlinda mtz...
Shujaa alikuwa na mambo mengi kichwani ukihusisha na kukamatwa na Polisi,ila tupo naye milele DAIMA,VIVA CHADEMA
 
MBUNGE WAKO KAFANYA NINI KUPUNGUZA LUNDO HILI LA KODI ZA MAFUTA,kwanza mafuta yanapofika DAR hufika kwa gharama ya TSH 550/=@LITA, HUanza kupigwa kodi zifuatazo.
1.insurace 0.1% c&f
2.wharfage 1.6% of CIF+18% VAT
3.SUMATRA USD O.25 PER MT
4.Destination inspection 1.2 of FOB
5.TBS 0.25% of C&F TBS Application and testing
6.Tipper fees USD 0.15 PER MT,PLUS 18% VAT
7.OCEAN Loss (0.5% MSP,0.30% GO&IK)CIF
8.Demurrage (estimate) 3 days per vessel
9.Evaporation losses (0.5% MSP,0.30 GO% IK) CIF
10.Surveyors cost ($0.15/MT
11.Financing cost (1.750% CIF)
12.Fuel levy (Tsh 200/LT-petrol,disel)
13.Excise duty (petrol Tsh 339,Disel Tsh 314,kerosene 52@lita
14.EWURA Levy (petrolTsh 6.10,Disel Tsh 6.80. kerosene Tsh 7.1@LT.
15.OMC’S OVER head & margins (101.11/LT
16.Dealers margin (53.49/LT
17.LOCAL Transportation (Tsh 10.00/LT
18.Up country /Bridging transportation (Tsh 130/km/1000 LT
HUU ndi mfumo wa sheria ya kodi ya petrol,diesel na karosine wewe kama mtanzania unafanyaje hizi kodi zipungue?.timiza wajibu wako
 
huyu mbowe akapimwe akili bajeti imetimiza matakwa ya wananchi.mi sioni tatizo na hii bajeti na kwa hili CCM wameonyesha kutujali sisi wananchi ambao ni mahohehahe wakutupa.
 
Nina mchango kidogo juu ya bajeti yetu ya 2011-2012. Kama budget yetu imedhamiria kutumika kama chombo cha ku-stimulate or induce economic growth with equity (i.e. pro – poor growth), then our current budget is a failure. Imegeuka zaidi kuwa bajeti ya kushabikia ukuaji wa uchumi ambao kwanza ni matokeo ya soko huria ambalo wanaojidai nalo sio zaidi ya asilimia kumi (yani watanzania milioni 4); na pili, ukuaji huu wa uchumi haujatokana na mikakati thabiti iliyowekwa na serikali ili kukuza uchumi shirikishi kwa maana ya kwamba benefits to trickle down to the poor, badala yake, kwa kiasi kikubwa ni kwamba maskini (zaidi ya watanzania milioni 36) wakifaidika ni kwa bahati sana kwani kimsingi hawakulengwa (zaidi ya kutajwa tu); nitajaribu kuyafafanua baadae;
Bajeti ya mwaka huu imejadiliwa na mengi yameshasemwa kwahiyo sio hekima kuyarudia. Ningependa kuchukua nafasi hii kuwapongeza wale wote ndani ya CCM na upinzania ambao wamefanikisha bajeti hii kurudishwa ilipotoka ikafanyiwe marekebisho. Nitajaribu kugusia maeneo kadhaa tu kama ifuatavyo.
  1. Tumekuwa tunajipongeza sana kwamba tunavunja rekodi ya GDP growth rates mfano ile ya over 6.5% kati ya mwaka 2000 na mwaka huu wa 2010. Tunazidi kujidai kwamba GDP per capita yetu inakimbilia dollar 500 na eti hatupo mbali sana kufikia kuwa nchi ya Maendeleo ya kati (kama Africa ya kusini, Misri, Vietnam n.k) na sio nchi maskini tena kwani ili kuwa kwenye ligi ya Maendeleo ya kati, GDP per capita yako lazima ifikie $999. Kufikia GDP per capita ya kiwango hiki kwa mtindo wa kuachia mfano sekta ya madini (kwani ndio imekuwa kiini cha GDP growth since 2000) iendeshe mambo inavyotaka ili mradi pato la taifa liongezeke sio kazi ngumu kwani GDP per capita is an illusional measure of well – being ya wananchi ambayo inagawanya tu pato la taifa la mwaka kwa idadi ya watu (population). Ni muhimu tuachane na kipimo hiki cha ovyo cha Maendeleo cha World Bank kwani viongozi na watunga sera wetu wakijipanga kwa mtindo huu, hatutafanikisha malengo ya kufuta umaskini kwani hata hiyo GDP per capita ya dollar 500 ya leo sio kwamba ni wananchi wanapewa mifukoni bali ni reflection ya ongezeko la pato la taifa ambalo halimnufaishi maskini.
Mfano rahisi – mwaka jana tumeuza dhahabu yenye thamani ya dollar 1.5 billion. Thamani hiyo imechangia sana GDP yetu kukua lakini thamani halisi ya mapato ya nchi ni only 3% ya 1.5 billion dollars ambayo ni dollar milioni 45 tu. Angalia kule tarime, hakuna reflection hata ya mapato ya maskini wenzetu kule kwamba wamekuwa wanapata even dollar 50 mifukoni mwao kila mwaka kati ya hizo dollar 1.5 billion zilizozalishwa na rasilimali zao. So GDP per capita measures are flawed na tuachane nazo. Ukweli leo unabakia wazi kwamba asilimia 36% ya watanzania ni maskini wa kutupwa, hawana mbele wala nyuma, hii ni sawa na watanzania milioni 16, ambapo tukiamua kugawanya katika mikoa ambapo kila mkoa tuupe wastani wa wakazi milioni moja na nusu, basi tuna mikoa kumi ya Tanzania ambapo watu wake wote ni kama omba omba wa barabarani kwani hawana mbele wala nyuma. Additionally, watanzania zaidi ya asilimia 88 wanaishi chini ya dollar moja kwa siku ikiwa na maana ya kwamba zaidi ya watanzania milioni 35 kati ya milioni 40 na ushee, katika kila siku ya maisha yao, hawana zaidi ya shilling 1,500 au 1 USD mifukoni au kwenye fundo za khanga zao, huku gharama za maisha zikizidi kupanda. Wengi ya hawa ni vijana na kina mama.
Such persistence incidence of poverty inamaanisha kwamba bajeti zetu (sio hii tu) zimefeli to meet the development needs and development challenges of our country.
  1. Kwa kutazama haraka haraka, tuangalie, je bajeti ya 2011-2012 inataja key words muhimu kama hizi mara ngapi? Umaskini, Vijijini, Vijana, Watoto, Wanawake? Matokeo ni kama ifuatavyo:
  1. Umaskini imetajwa 7 times kwa juu juu sana;
  2. Vijijini imetajwa 3 times ingawa huko ndio kuna zaidi ya asilimia 65 ya watanzania. Vijijini imetajwa zaidi kuhusu utekelezaji wa southern agricultural growth wakati vijiji Tanzania vipo northen, eastern, na western pia.
  3. Watoto imetajwa only once na its only on watoto yatima na kijuu juu sana.
  4. Vijana imetajwa mara 3. Ikumbukwe kwamba vijana na watoto kwa sasa ni asilimia 70% ya watanzania milioni 40 na ushee. Mtindo wa kuwataja vijana kwenye bajeti mwaka huu chini na mikakati ya AJIRA, VETA, SIDO hauna tofauti kubwa sana na miaka iliyopita ambapo hakujazaa matunda yoyote ya maana kwani AJIRA, VETA na SIDO ni kama vile inaogopa vijiji kama ukoma. Kilichotofauti hasa hasa juu ya vijana na bajeti mwaka huu ni juu ya punguzo la kodi kwa vijana wanaojiajiri na biashara ya kuuza majokofu kama mkakati wa kuwaondoa toka kwenye umaskini. Punguzo la kodi kwa wafanyabishara wa majokofu ni kutona 25% to 10%. Mantiki ya kulenga wajokofu badala ya vijana machinga ni ngumu kuielewa kwani ajira ya vijana wengi ni machinga na wengi zaidi hawana ajira yoyote; majokofu yanalenga wenye matumizi ya umeme Tanzania ambao hawazidi asilimia 15 ya watanzania, na haizidi asilimia 4 ya watanzaa vijijini.
  5. Neno wanawake katika bajeti ya mwaka huu halijatajwa kabisa ingawa kumekuwa na mikakati ya kuwawezesha kina mama kiuchumi, kijamii, kisiasa (udiwani, ubunge, na sasa urais). Hata kuelezea masikitiko yangu juu ya hili suala la wanawake kutotajwa katika bajeti mama, kina mama ambao ndio nguvu kazi mashambani kuliko wanaume (wakulima), walezi wa watoto wetu, wapiga kura wenzi zaidi, naishiwa nguvu kabisa kulielezea.
Kuna three important standards against which tunaweza pima ubora wa bajeti yetu.
  1. Aggregate fiscal discipline;
  2. Resource allocation based on strategic priorities
  3. Efficient and effective utilization of resources.
Kama kawaida ya miaka meingine, bajeti ya mwaka huu imepwaya kwa kiasi kikubwa katika maeneo yote haya.
  • Watanzania pamoja na kuwa wanazidi kulipa kodi nyingi sana – measured as revenue to GDP ratio – ambapo sasa inakimbilia 18% huku serikali ikiweka malengo ya kukusanya kwa aslimia ya juu zaidi, watanzania have rarely gotten value for their money; Bajeti hii imezidi kupeleka fedha kidogo towards development expenditures kwani most of the funds zimezidi kwenda to recurrent expenditures (Mishahara na posho kwa watumishi wa serikali). Hii inakuja wakati huduma za msingi za kijamii bado ni duni na economic opportunities kwa maskini bado ni kikwazo; Leo hii asilimia ya watanzania wanaioshi kwenye umaskini uliopilitiza (ambao hawana tofauti na kuwa omba omba) 36% (au milioni 16); hali hii haijabadilika kwa miaka mingi sana; na kama tulivyokwisha ona, zaidi ya watanzania milioni 35 kati ya 40 na ushee wanaishi chini ya shillingi 1,500 kwa siku huku gharama za maisha zikizidi kupanda;
  • Budget deficit imezidi kuwa endemic kwani inapelekea deni kubwa sana la ndani ambalo serikali imekuwa likili entertain and which end up depressing uzalishaji nchini; deni hili mwananchi hana taarifa kwamba ina maanisha kwamba hata vitukuu vyake vitaishi maisha ya umaskini kama ya kwake kama hatua za haraka hazitachukuliwa;
  • Bajeti inatoa ishara zote kwamba imekuwa vigumu kwa national development goals to be realized. Bajeti inajichanganya sana kuhusu framework ipi ndio inapewa mkakati na resources na kwa kiasi gani na kwa muda gani ili kusaidia kupunguza umaskini. Tumeshindwa kabisa ku deal vizuri na masuala muhimu katika hili ambayo siri yake ni ndogo tu: a link between budgeting, policy and planning. Tuna framework za Maendeleo nyingi na haziendani wala kushirikiana kwa ukaribu, ni kama zinashindana. Mfano PRSP/PRGF/Mkurabita, Vision 2025, National Poverty Eradication Sratetegy (1998) etc etc zinazidi kutuchanganya na kupoteza resources zetu;
  • Disproportionate spending - kati ya matumizi ya kawaida na matumizi ya Maendeleo katika bajeti yetu limekuwa ni tatizo kubwa sana linalozidi kuchangia kuzorota kwa Maendeleo ya mtanzania. Kila mwaka fungu la Maendeleo ya kawaida (recurrent expenditures - kwa ajili ya mishahara, posho always ni kubwa sana compared to fungu kwa ajili ya maendeleo au la kuinua watanzania toka kwenye umaskini (kama vile elimu, afya, maji, miundombinu n.k). Tutalitzama hili kwa undani baadae kidogo;
  • Vile vile, misuse of public resources is still rampant kama inavyoanishwa wakati wote na CAG; anachokieleza kila CAG na ripoti zake kila mwaka, kitu amhacho watanzania wengi wanashindwa kuelewa ni kwamba - kila mwaka, the return we get kutoka kwenye kodi zetu ni way below acceptable level.
  • Sasa kwa sababu yameshachambuliwa mengi na wengine, mimi nitalenga kitu kimoja tu ambacho ni disproportionate spending - kati ya matumizi ya kuendeleza umaskini i.e. matumizi ya kawaida ya serikali/recurrent (yani mishahara, posho na marupurupu) versus matumizi muhimu kupunguza umaskini i.e. development expenditures (yani maji, afya, elimu, miundo mbinu, n.k).
Bajeti ya mwaka huu kama tulivyokwisha ona ni trillion 13.5; kati ya hizi, trillion 8.6 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida; kati ya hizi 8.6 trillion, 3.2 trillioni ni kwa ajili ya posho na misharaha ya watumishi wa serikali; hii ni karibikia asilimia 25% ya bajeti yetu yote (13.5 trillion) ya mwaka huu wa fedha 2010/2011;

Kwa ajili ya Maendeleo kama vile elimu, afya, maji, miundo mbinu, zimetengwa trilioni 4.9 tu kati ya bajeti nzima ya trilioni 13.5. Kwa maana nyingine na rahisi – wale waliokuwa na ajira rasmi serikalini na taasisi za umma wametengewa kama posho na mishahara shilling trillion 3.2 kati ya bajeti nzima ya 13.5 trillion and some of these funds zinatokana na mapato ya kodi wanazotozwa wakulima na kina mama wanaouza vitumbua barabarani; wakulima na maskini hawa wasio kwenye sekta rasmi, wao wanategemewa wanufaike na 4.9 trilioni kwa njia ya huduma za kijamii ambazo zinaishia kufaidiwa zaidi na wenye uwezo na pia walio mijini kwani huduma za kijamii vijijini ni nadra sana; vile vile pesa nyingi zinazotengwa kwa ajili ya huduma za kijamii imekuwa ni jadi kusikia zinayeyuka huko kwenye halmashauri zetu na wanaokula ni wale ambao wanafaidi lile fungu la 3.2 trilioni la mishahara na posho ambayo kwa kiasi kikubwa inatokana na kodi wanazotozwa maskini; na ndio wao waliopewa jukumu la kusimamia fedha na miradi ya Maendeleo yani zile 4.9 trilioni; matokeo huwa aidha hazifanyi shughuli iliyokusudiwa kutokana ukweli kwamba huduma nyingi zinapelekwa mijini wakati maskini wapo wengi vijijini au huduma hizi za 4.9 trillioni kwa kiasi kikubwa zinaishia kuwanufaisha watendaji ambao wanazichakachua. Suala hili limewekwa bayana na kamati ya bunge ya hesabu za serikali za mitaa inayoongozwa na Mh. Mrema na Mh. Iddi Azzan. Sababu mbili hizi ndio chanzo kikubwa cha the vicious cycle of poverty and corruption.

Katika bajeti ya 2011-2012, pia Waziri ametamka kwamba mkakati uliopo ni kuhakikisha ndani ya miaka minne (by 2015) tunapunguza external dependency ya budget yetu, lengo ikiwa kiwango hicho kisizidi asilimia 10% ya bajeti by 2015 (kwa sasa ni kama asilimia 36); swali la msingi hapa ni je, kwa hali hii ambayo maskini wanatengewa fedha kidogo kwahivyo kutoinuliwa kijamii na kiuchumi ili waweze kuchangia pato la taifa lao kwa kasi zaidi, wataendelea kunyonywa kupitia ongezeko la kodi wasizoona faida yake ili mradi tufanikishe lengo la kupunguza dependency ya donor funds on our budget by 2015? Sababu kama tunataka tuwe na bajeti ya kujitegemea, ni lazima tukijikite zaidi kuongeza mapato ya ndani. Je huku kutatokana na ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato ya serikali? Kwani hadi sasa hakuna ushahidi juu ya jitiaza ya ubunifu huu; kinachoonekana ni serikali kujaribu kuzikimbia sekta zinazogusa maslahi ya wawekezaji na pia kuzikimbia sekta ambazo inaziona ili kuzifanikisha ziwe zinachangia pato la taifa, zitaileta serikali gharama kabla ya mafanikio, ndio maana mwisho wa siku huwa ni kukimbilia kwenye vyanzo ambavyo vipo wazi, na visivyohitaji nguvu ya ziada zaidi ya kuviwekea rules and regulations mfano VAT; Na kama punguzo la dependency on donors juu ya bajeti zetu kufikia chini ya 10% by 2015 litatokana na kodi toka sekta ya madini ambapo tumekuwa tunapigania sana kodi toka kwenye madini ili tuanze kunufaika na rasilimali zetu, mbona suala hili halijaguswa katika bajeti?
Ni muhimu tueleweshwe zaidi juu ya mikakati hii ya kupunguza kuwategemea wahisani.

Tukirudi
nyuma kidogo katika historia ya nchi yetu, mawaziri wa fedha wa Mwalimu Nyerere walisifiwa sana kwa utendaji wao kwani walikuwa ni wataalamu, waelewa na waliojali na kuwatumikia wananchi – hawa walikuwa Amir Jamal, Paul Bomani na Edwin Mtei. Bajeti ya kwanza ya Tanganyika huru ilikuwa ni ile ya 1962/63 chini ya waziri Paul Bomani lakini iliyoanza kwa kazi nzuri ilikuwa ni ile ya mwaka 1963/4 chini ya marehemu Amiri Jamal. Bajeti yake ya T.sh milioni 939 ilisifiwa sana kuwa ya kwanza na ya aina yake kwa maana ya kwamba matumizi ya serikali yalikuwa chini ya mapato ya serikali na hazina had a surplus of 1 million shillings zikiwa hazijapangiwa matumizi yoyote kwa kipindi chote cha 1963/1964. This is what we call fiscal discipline. Kwa miaka ya sasa nidhamu kama hii ni haba kwani imekuwa ni tabia ya watendai wetu wakishirikiana na wahasibu wao kuhakikisha salio lolote lililobakia katika idara mbali mbali linatafutiwa matumizi hata kama sio ya lazima ili bajeti mpya ikija fedha nyingine ziingie; huku ni kudumaza Maendeleo; Tumesikia mara nyingi watunza fedha (wahasibu wa taasisi na idara kadhaa) wakijipangia matumizi mengi ya ovyo ili akaunti zao ziwe tupu bajeti mpya ikiwadia; kwa watu hawa, wanaona kama vile ni kosa au dhambi kubwa sana kubakisha au kurudisha hazina salio lolote. Na ni kawaida sana kwa hazina nao kutofuatilia kwa umakini. Tukumbuke masalio ya bajeti kama haya yanatokana na kodi inayolipwa na maskini ambao wao hutengewa trilioni 4.9 katika bajeti indirectly kupitia huduma za kijamii wakati wanaoifilisi bajeti na wanaofuja hela zao ni watendaji waliotengewa 3.2 trilion ambazo zinaenda moja kwa moja mifukoni mwao kama misharaha na posho; role of public expenditure reviews ni muhimu sana hapa;
Tukirudi katika historia, mwaka 1964/65 Amiri Jamal akiwa bado waziri wa fedha, i, pia aliweka rekodi ya kipekee kwa mwaka huo wa fedha. Tulikuwa na bajeti ya paundi million 35. Matumizi ya kawaida yalikuwa paundi 12.4 milioni na yale ya Maendeleo yakiwa 22 milion pounds; Hii ilikuwa ni bajeti ya kwanza ya Maendeleo kwani ilikuwa ni ya kwanza na ya pekee ambapo matumizi ya Maendeleo yalizidi yale ya kawaida. Asilimia 63 ya bajeti ilikwenda kwenye matumizi ya Maendeleo na asilimia kama 37 ndio ilikwenda kwenye posho na mishahara. This is a typical fiscal discipline. Today, hii ratio ni the opposite.

Edwin Mtei akiwa waziri wa fedha kati ya mwaka 1976 – 1979 alihakikisha kwamba fungu la Maendeleo na lile la matumizi ya kawaida kama mishahara na posho hayatofautiani sana pamoja na kwamba kulikuwa na challenge kwamba public sector was the only employer at that time na sera ilikuwa full employment – kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi ni lazima afanye na apate kazi was the order of the day; Chini ya Mtei, kwa wastani, fungu la Maendeleo lilikuwa sio chini ya asilimia 42 katika kipindi chake chote alipokuwa waziri wa fedha; Baada ya enzi hizi za Amir Jamal na Edwin Mtei, hatujawahi tena kuwa na bajeti inayomweka maskini at the centre. Mawaziri wa fedha wa Nyerere hawa wawili walifanikisha hilo kwa kiasi kikubwa. Na ni wakati huu ambapo tuliona mtanzania akipata Maendeleo makubwa ya kijamii kama vile elimu na afya; changamoto kubwa ilibakia katika Maendeleo ya kiuchumi; We remain to wonder what if Mwalimu Nyerere angeamua kutumia rasilimali kama madini, kwa umakini na Uzalendo aliokuwa nao, sio siri kwamba maendeleo ya uchumi kwa mtanzania yangeboreshwa zaidi;

Chini ya Mwinyi, longest serving minister wa fedha alikuwa ni Msuya (kwani Malima, Kibona na JK walikaa muda mfupi); wakati wa Msuya kati ya 1985 na 1990, kwa wastani, maskini walitengewa asilimia 21 ya bajeti (ukifananisha na wastani wa karibia asilimia 40 wakati wa Nyerere). Kipindi cha baada ya 1985 maskini alitupwa kuliko kipindi chochote cha historia ya nchi yetu kiasi cha kuifanya Tanzania kuwa nchi ya tatu toka mwisho kwa umaskini duniani. Kipindi cha Mheshimiwa Mkapa waziri wa muda mrefu alikuwa Daniel Yona (kwani Mbilinyi na mramba walikaa muda mfupi); Yona alijaribu kurejesha maskini to the centre kwani allocation ya budget for development ilipanda kidogo na kufikia wastani wa 30% of the total budget.
Leo hii tumefikia hatua muhimu kwani wabunge wetu walimeona tatizo lililopo katika bajeti zetu kwani imekuwa ni utamaduni kuwa na porojo juu ya maskini bila ya vitendo;
Ili bajeti yetu kwa 2011-2011 iwe credible, inahitaji to meet the following:
  1. Kwanza na awali ya yote, lazima ituonyeshe how the poor were involved in the preparation process kwani budgeting is all about revenue and expendire – ni vizuri tujue upande wa pili wa revenue ambao ni wa walipa kodi walishirikishwa vipi katika kuweka priorities n.k;
  2. Pili, lazima budget iwe based on sound economic forecasts and targets, sio ubabaishaji (.e.g. inflation on bidhaa muhimu, GDP growth, poverty reduction targets) combined with robust resource inflow forecast;
  3. Tatu, lazima pawe na harmonization, alignment, transparency and predictability of donor funds; hapa kumekuwa na kuyumba sana;
  4. Nne, lazima budget iwe na framework that provides greater flexibility of policy and affordable expenditure plans; pia budget iwe forward thinking in terms of policies and expenditure plans;
  5. Tano, kuwepo na budget execution system that aligns actual and planned spending; inasemekana kuna tabia ya serikali kutumia au kuchota fedha katikati ya mwaka under the window ya dharura; kama ni kweli, hili liachwe; window hii itumike only when patatokea unforeseen and unpredictable conditions;
  6. Sita, budget lazima iwe performance oriented – it should encourage strategic allocation of resources at all levels and emphasize on efficiency and effectiveness in allocation and use of resources;
  7. Saba, there has to be an incentive framework with rules that are predictable and processes that change behaviours za watendaji hususan wasimamizi wa fedha za maendeleo; the budget should not only promote compliance among watendaji, but pia commitment na dedication;
  8. Nane, budget ikuze transparency and access to information as well as mechanism for accountability;
  9. Tisa, bajeti lazima iwe trustworthy – it should minimize tofauti kati ya fedha zitazotengwa kwa ajili ya Maendeleo and the actual expenditures kwani hili huwa ni tatizo kubwa katika bajeti zetu nyingi; tumeona mifano mingi ambapo wizara zinatengewa fedha kiasi gani lani actual expenditures zinakuwa short na hizo fedha hazirudi hazina na wanaozifuja hawachukuliwi hatua zozote za kisheria;
  10. Na kumi Bajeti lazima iwe na three Cs – Commitment, Clarity and Consistency;
If we want our budget to be at the service of the poor, inahitaji a practical medium term process for budget allocation TO PLAN CHANGES IN STRATEGIC PRIORITIES and a public expenditure management capacity TO ENSURE THAT PLANS ARE EXECUTED. The failure to properly coordinate planning and budgeting functions imekuwa a fundamental weakness in Tanzania. Tunatumia the Medium Term Expenditure Framework (METF) towards this end to focus on strategic priorities in the medium term but bado hatujafanikiwa vya kutosha. MTEF is a necessary tool for budget credibility. MTEF ni framework mpya baada ya kuondokana na ile ya zamani ambapo bajeti zilikuwa based on a year to year basis. MTEF is a multi-year framework.
The MTEF should become a comprehensive document covering all sources of revenue and all public sector expenditures in Tanzania. Tatizo huwa linajitokeza kwamba sometimes the central Government has very incomplete information for instance on donor aid, significant revenue resources are off-budget and not centrally reported, resulting in an MTEF which gives only a partial picture of total public expenditure. Donors nao huwa wanachangia mapungufu katika MTEF, so it is extremely important for donors to respect the MTEF disciplines, watoe reports on their commitments thus enabling their spending to be prioritized as part of the MTEF process, even if, for reasons of accountability, wakiendelea to retain their own disbursement procedures.

In order for public expenditure to better serve the poor, pande zote mbili meaning serikali na upinzani need to realize that ‘POLITICAL WILL' to confront difficult choices is necessary but not sufficient; public expenditure needs to be aligned to more effective public expenditure management, macroeconomic and budget stability. A budget system that turn policy analysis into actual cash releases to implement the intended policies need to be in place.
An effective link between policy and budgeting is necessary. Kuwa na budget ambayo inakuwa implemented as planned will not lead into policy effectiveness if budget plans do not reflect priorities. This budgeting failure occurs hapa Tanzania especially when kunapokuwa na weak linkages kati ya budgeting and policy making, such as when they are conducted in separate institutions, or separate structures in the same institution, au when haziwi linked on time.

Mwisho kabisa, policies should be linked directly to the needs and priorities of the poor. Bajeti ya mwaka huu lazima ije na a detailed framework on how the priority sectors of Umeme, Maji, Miundombinu, Kilimo + Umwagiliaji and expansion of private were chosen together with the performance review based on earlier allocation of resources towards these sectors;
Ni muhimu wawakilishi wetu bungeni wasisahau ya kwamba they have the final say and responsibility for making our budget iwe pro- poor in a sustainable manner;
 
Back
Top Bottom